Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Bavicha bhana!Nilitaka kuja na andiko kama lako uzuri umeniwahi Acha nichangie kwako.
"MBOWE ALIA NJAA" ni sentensi inayoonesha Mbowe amekosa chakula kutokana na kukosa uwezo kiuchumi wa kukipata. Wafanyakazi wanàpokosa kulipwa mshahara miezi 2 au 3 wanapolalamika tunasema wanalia njaa maana wamekosa uwezo wa kulisha familia zào. Lakini Kwa hili la Mbowe ni tofauti, nimesoma gazeti jingine limeandika "MBOWE ALALAMIKA KUTOPEWA CHAKULA MCHANA KWA MIEZI 5" angalau inaleta maana. Lakini lingine limepotosha zaidi Kwa kuandika "MBOWE AKOSA CHAKULA MIEZI 5" na nimeona hata baadhi ya watu mitandaoni Wenye milengo ya ovyo àmbao hawana kawaida ya kutafuta undani wa habari wameanza kumtukana Mbowe wakimwita mpuuzi na mzushi eti binadamu anawezaje kuishi miezi 5 bila kula? Waandishi na wahariri mna nafasi kubwa ya kuielekeza Jamii au kuipotosha. Kwa hili sehemu kubwa mmepotosha watu na kuwapa nafasi wasiojiweza kifikra kutukana watu bila sababu.
Si ndio uhuru wenyewe wa habari huu?