Gazeti la pili kwa uuzaji nchini Hispania El País limechapisha habari isemayo "John Magufuli the African Bolsonaro" kutokana na njia anayotumia kupambana na janga la virusi vya corona. Gazeti hilo limetaja viongozi kama Donald Trump (Rais wa Marekani) na Jair Bolsonaro (Rais wa Brazil) kama viongozi waliokataa kuchukua hatua madhubuti dhiti ya virusi vya corona.
Gazeti hilo limemtaja Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania kama kinara wa Africa kwa ukaidi, limetoa shutma kwa Rais Magufuli kwa kugoma kutoa taarifa kuhusiana na idadi ya visa na vifo vya ugonjwa huu tishio duniani. Wameongezea kwa kuponda mbinu mbali mbali kama maombi, na upimaji wa sampuli za mapapai na mbuzi katika kugundua mapungufu ya maabara ya Taifa.
Hata hivyo gazeti hilo limemsifu Rais Magufuli kwa uwezo wake wa kuchapa kazi na kutokupokea rushwa na ujenzi wa miundo mbinu mingi wakati akilitumikia taifa kama Waziri wa Ujenzi.
Source:
John Magufuli, o Bolsonaro africano
Maoni yangu: Taarifa hizi si nzuri kwa sekta ya utalii na hata biashara, japokuwa tuna mapungufu katika vita hii lakini hakuna taifa lisilo na mapungufu kila moja kuna sehemu limeteleza natumaini serikali litafuatilia nini ni chanzo kwa vyombo hivi kutufanya tuonekane wazembe na kudhihakiwa na kupakwa sifa mbaya.
Lazima tujiulize ni nini kipo nyuma ya tuhuma hizi? Hii ni vita na kama alivyosema Mh. Rais leo kuna kitu zaidi lakini hawezi kukisema sasa.