Ili kuharibu taifa lolote, anza kwa kuharibu mfumo wake wa elimu. Mfumo wa elimu wa Tanzania kwa sasa unawaandaa vijana kuwa wafanyakazi wa serikali au taasisi binafsi, jambo ambalo limepelekea wengi wao kuishi maisha duni huku wakisubiri ajira kutoka serikalini na kwenye taasisi binafsi. Takwimu za serikali kutoka mwaka 2021 zinaonesha kuwa vijana milioni 1.7 hawana ajira, sawa na asilimia 12.2 ya nguvu kazi ya vijana milioni 14.2 wenye uwezo wa kufanya kazi. Hii ni kwa mujibu wa jalida la Swahili Times (Vijana milioni 1.7 Tanzania hawana ajira).
Ili Tanzania iepukane na hali hii, ni muhimu kubadilisha mtaala wa elimu unaomfanya kijana kutegemea kuajiriwa na badala yake, kuanzisha mtaala mpya unaomhamasisha kijana kujiajiri. Mtaala huu mpya unapaswa kukidhi mahitaji ya karne ya 21 kwa kuweka mkazo kwenye masomo ya msingi yanayohusu taifa, huku ukiibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.
Kwa mfano, wanafunzi wanaweza kufundishwa masomo ya kawaida sambamba na masomo ya vipaji kama vile:
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
• Usanifu wa mifumo ya kompyuta
• Uundaji wa programu
• Mtandao wa kompyuta
• Usalama wa mtandao
• Uchambuzi wa data
Ujenzi:
• Uhandisi wa ujenzi
• Usanifu majengo
• Usimamizi wa miradi ya ujenzi
• Teknolojia ya ujenzi
• Ujenzi wa barabara na madaraja
Kuchomelea:
• Uchomeleaji wa chuma
• Uchomeleaji wa mabomba
• Uchomeleaji wa alumini na metali nyingine za mwangaza
• Uchomeleaji wa umeme
Uhandisi wa Mitambo:
• Matengenezo ya mitambo
• Usanifu wa mitambo
• Uundaji wa mashine
Umeme:
• Ufundi wa umeme wa majumbani
• Ufundi wa umeme wa viwandani
• Ufundi wa vifaa vya elektroniki
Ufundi Magari:
• Matengenezo ya magari
• Uhandisi wa magari
• Teknolojia ya magari ya umeme
Huduma za Afya (Sayansi kimu):
• Uuguzi
• Utabibu
• Teknolojia ya maabara za afya
Kilimo:
• Kilimo cha mimea
• Ufugaji wa wanyama
• Kilimo cha kisasa
Mitindo na Ususi:
• Ushonaji nguo
• Ubunifu wa mitindo
• Ususi wa nywele
Utalii na Ukarimu:
• Usimamizi wa hoteli
• Uongozaji wa watalii
• Upishi
Biashara na Uhasibu:
• Uhasibu na fedha
• Usimamizi wa biashara
• Masoko
Sanaa na Ubunifu:
• Uchoraji
• Ubunifu wa ndani
• Usanii wa michoro
Mwanafunzi anatakiwa kusoma masomo ya kawaida kama vile Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Maarifa ya Jamii, Sayansi, Stadi za Kazi, Sanaa na Michezo, Maarifa ya Afya na Michezo, Elimu ya Dini, pamoja na somo moja la fani anayoitaka kuanzia awali mpaka chuo kikuu. Hii itamfanya mwanafunzi awe bora katika fani husika tangu akiwa mdogo, hivyo kumjengea ujuzi na kujiamini katika maisha yake na kumwezesha kuendesha maisha yake bila kutegemea ajira.
Katika kipindi cha miaka 20, Tanzania itaweza kuona matunda ya mabadiliko haya ambapo tutakuwa na wahitimu waliofundwa kupitia mtaala mpya. Hata wale ambao hawataendelea na elimu ya juu, wataweza kujiajiri kutokana na fani walizosoma na vipaji walivyokuzwa. Mfumo huu wa elimu utaleta mapinduzi makubwa kwa kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira na kupunguza umasikini nchini.

Upvote
2