Magomeni Kota - TBA fungulieni njia mbadala wakati huu wa ujenzi wa barabara

Magomeni Kota - TBA fungulieni njia mbadala wakati huu wa ujenzi wa barabara

Crucifix

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Posts
1,655
Reaction score
592
Ni hivi, barabara zote za kuelekea barabara ya Morogoro zina marundo ya vifusi. Geti pekee kwa wakazi wenye magari la kuingia Magomeni Kota ni lile lililo mkabala na Turiani Sekondari. Kwa maelekezo ya TBA na walinzi wake, geti hilo sharti lifungwe saa 6 usiku.

Hawa ni watu na siyo mifugo wa kupangiwa muda wa kurudi nyumbani. Wakati huu ambapo kifusi kimerundikwa barabarani kwa zaidi ya wiki sasa na haijulikani kitasambazwa lini, toeni ruhusa ya kutumika kwa njia mbadala badala ya kila siku watu kugombana na walinzi.

Wewe mkurugenzi wa TBA upo tayari kuharibu gari lako kwa kulipoandisha juu ya kifusi kila siku ili ufike kwako?

Tumieni akili.
 
Kwa hiyo tatizo ni kifusi au tatizo ni geti kufungwa saa 6 usiku?
 
Back
Top Bottom