Màana ukienda hospitalini utaambiwa ni ugonjwa was akili unasababishwa na msongo wa mawazo, ukienda makanisa ya walokole utaambiwa ni suala la kiroho
Kuna mchungaji alikuwa anamuombea bi mkubwa. Shida iliyotokea ni bi mkubwa alisafiri kwenda mkoani kusafisha makaburi. Ya familia huko.
Sasa aliporejea naona zile purukushani za pikipiki huko milimani katika kusalimia ndugu na jamaa. Akawa ameshitua mwili wake eneo la mbavu na misuli ya mgongo.
Unajua unapofanya movement yoyote ya ghafla ghafla, misuli lazima ifanye kuvimba au ili kuprotect skeleton yako ambayo inaprotect organs zako za ndani.
Sasa alienda hospital akapewa dawa za inflammation jambo ambalo lilikuwa ni kosa sababu yeye hajapata kesi ya inflammation alipata kesi ya muscle contraction au misuli kuvimba yaani mfano ukipigwa rungu kwa nguvu hapo kwenye mkono utavimba kinachotokea hapo ndani ya mwili wako kumetokea inflammation hilo eneo la uvimbe yaani kwa ndani kwenye msuli ulipopigwa.
Ila ukifanya mazoezi kwa nguvu isivyo kawaida yako misuri inaweza vimba pia lakini hapa itakuwa ni misuli yako imekakamaa au contractions imetokea na utahitaji dawa ya relax misuli ili iache kuuma na urudi sawa.
Sasa bi mkubwa walimpa dawa na kumchoma sindano za inflammation hazikumsaidia maumivu ya misuli yakaanza kupanda kwa kasi kuelekea shingoni. Akaanza kupata maumivu ya kichwa eneo la misuli ya shingo.
Akaenda kwa mchungaji, akaanza kupewa sasa maombi mchungaji anamwambia kuwa alienda huko makaburini anaona kuna roho zilimvaa na zimekasirika kwann hayupo kwenye ibada ya mizimu ndizo zinamuandama na atahitaji maombi ya wiki na kufumba.
Sasa nilipokwenda msalimia ndio nikakuta hizo story. Nikamwambia niletee dawa ulizotumia. Aliponionyesha nikaelewa tatizo lipo wapi. Nikatoka muda huo huo nikaenda Upanga haraka nikaenda mnunulia dawa za kurelax misuli haraka nikamleta akameza mchana ule akalala maana hakuwa poa hata kuketi. Muda mrefu.
Akaamka na usiku baada ya chakula cha jioni akameza alipoamka asubuhi siku ya pili kaamka fiti kama sio yeye aliyekuwa anashindwa hata kuongea vizuri kwa maumivu.
Nikamwambia hawa watu wenu wa makanisani muwe nao makini sana. Wengi wao hawajui wanachokisema wanapiga ramli tu kama waganga wa kienyeji.