Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Mie ningependa kukusaidia mkuu kwenye proposal yako..lol...

suggestion;

1.Police wawe trained kugundua mtu anayeumwa na kumtoa alipo na kumpeleka hospital/safe place.

2.Hospitali za watu wa magonjwa ya akili ziongezwe Tanzania, nakumbuka zamani ilikuwa ni Mirembe na Muhimbili hospitali, ndio hospitali pekee za watu wenye matatizo ya akili, hizi hazitoshi ,kama watu wanne mmoja ana kichaa,this means watu million moja katika million nne za watu wanaoishi Dareslaam wana magonjwa ya akili,je hospitali za wagonjwa hawa ni ngapi Dareslaam tu peke yake??..hili lifanyiwe kazi na serikali...

3.Anzisha Charity(nilikua na hili wazo likanishinda kiutendaji..lol )..yenye help line,uitangaze kwa bidii..watu wakiona mtu yuko hatarini kwa sababu ya matatizo ya akili,then wanapiga hio number..na kupelekwa safe place(hili tegemea na wasanii pia,watatumia huu mwanya,LOL)

4.Iandikie serikali kuikumbusha ina wajibu kama yalivyo magonjwa mengine kama kisukari kupiga kampeni(awareness) ya matatizo ya akili, watu waje forward kupata msaada wasiende kwa waganga na wengineo…

1.
blessed blessed nitakushirikisha naona we have same calling!!
 
Write your reply...haya matatizo jamani ni ya kusikia kwa mwengine tu mimi Nina mdogo wangu anaumwa mwaka wa sita Sasa na keshalazwa hospital muhimbili zaidi ya miezi miwili na hakupata nafuu Bado tuna hangaika nae kwenye hospital na madaktar bingwa wa matatizo ya akili na kwenye Dua ila Bado anaumwa japo huwa Kuna kipindi mara moja moja anapataga nafuu na kuweza kufanya shughuli zake kikamilifu
 
Nilivyokuwa naanza kuumwa nilikuwa najua na naelewa kila kitu; sema nilikuwa mwisho naona nipo sahihi kwenye yote ninayofanya ndo nikaja gundua kichaa hajitambui usimsikilize mtu aliyechanganyikiwa bali mpelekeni hospital akapige dawa; ila cha kushangaza nilivyofika muhimbili nilizidiwa zaidi maana nilipoteza fahamu kabisa kwa mda wa wiki mbili na zaidi; watu wanakuja naongea nao; nawatukana; ila zote ni story maana sikuwa na ufahamu kabisa mpaka niliporydiwa na ufahamu nikawa unakumbka matukio kabla sijafikia muhimbili na baada ya fahamu kunirudia
mmh, pole sana ndugu yangu. kweli hujafa hujaumbika lolote linaweza kutokea🙄
 
Write your reply...haya matatizo jamani ni ya kusikia kwa mwengine tu mimi Nina mdogo wangu anaumwa mwaka wa sita Sasa na keshalazwa hospital muhimbili zaidi ya miezi miwili na hakupata nafuu Bado tuna hangaika nae kwenye hospital na madaktar bingwa wa matatizo ya akili na kwenye Dua ila Bado anaumwa japo huwa Kuna kipindi mara moja moja anapataga nafuu na kuweza kufanya shughuli zake kikamilifu
Dah poleni Mungu ni mkubwa azingatie dawa
 
Write your reply...haya matatizo jamani ni ya kusikia kwa mwengine tu mimi Nina mdogo wangu anaumwa mwaka wa sita Sasa na keshalazwa hospital muhimbili zaidi ya miezi miwili na hakupata nafuu Bado tuna hangaika nae kwenye hospital na madaktar bingwa wa matatizo ya akili na kwenye Dua ila Bado anaumwa japo huwa Kuna kipindi mara moja moja anapataga nafuu na kuweza kufanya shughuli zake kikamilifu
Msichoke kwenda makanisa yenye upako wa kimungu @ manabii wengi sana Mungu anaweza watumia kuwasaidia; naendelea kutumia dawa huku mnajaribu kumpeleka kwenye maombi kwa dar sehemu ambazo wanaweza kumhudumia anaweza akajaribu Ecg church under apostle mtalemwa/ shallow ministries under prophet Frank; arise shine under apostle mwamposa; ABC ministries under kagumila mwenge; akuzam mministry biafra under reverend Amri etc (ila kama upo interested mkuu sio lazima sana ila kama una shida najua unatafuta njia ambayo italimaliza kabisa keep goin mkuu)
 
Kinachonipa moyo ni ile hali yangu ya kupona kabisa na kuweza tekeleza majukumu yangu vizuri na huwa nikipita muhimbili nakutana na jamaa niliokuwa nao hospital clinic moja maana kuna siku maalum yaa clinic nikiona wanaendelea na dawa nami Mungu ameniponya kabisa; najua si kwa kuwa ni bora kuliko wao ila ni kwa neema tu

Pole sana na hongera kwa kupona njoo inbox nakuPM
 
Màana ukienda hospitalini utaambiwa ni ugonjwa was akili unasababishwa na msongo wa mawazo, ukienda makanisa ya walokole utaambiwa ni suala la kiroho
Sababu zipo nyingi mkuu; muhimbili kila siku wanAfundisha sababu; za magonjwa na namna ya kujizuia na kujikinga nayo..kuna kitengo change kabisa
 
Hii ishu ya mtu kuona na kusikia visivyooneka nayo iko kundi gani.
 
Nina shangazi yangu anayo hii hali. Changamoto au chanzo baada ya diagnosis kufanyika ni kwamba miaka ya nyuma alikuwa kwenye kitengo serikalini akawa anapiga sana Pesa mwaka 2000 hapo tu.

Alikuwa kwa siku akirejea na kibunda kidogo basi ni laki saba au tano. Ila mara nyingi anarudi la milioni 3, milioni 2 , milioni 5, alikuwa anapata pesa chafu sana.

Wenzake aliokuwa nao kitengo kimoja miaka hiyo wamejenga na wanamaisha na biashara zao saa hii ukikutana nao utasema ni wastaafu wa uwaziri mkuu au benki ya dunia. Wapo njema sana na wanamaisha.

Shida kwake ni alikuwa na matumizi makubwa yasiyo na future kwake. Kiasi kwamba pesa ikawa inaisha kwa kasi. Kaka yake ambaye ndie mshua alimkazia sana kumwambia ajenge mjengo aachane na upuuzi wa maisha ya kupanga ndipo kwa kujilazimisha akanunua eneo na kujenga kama kumridhisha kaka yake ila hakuwa na dhamira hiyo hata kidogo.

MUNGU wa ajabu sana. Alipomaliza ujenzi muda si mrefu kama miaka miwili mshua akavuta. Na yeye baadae kidogo kama miaka mitatu mambo yakaanza kwenda kombo kazini ikiwamo kusimamishwa kazi.

Bahati nzuri alikuwa na akiba akaiweka kwenye finishing ya nyumba akahamia haraka maana alikuwa bado kapanga na nyumba yake alikuwa anakaa ndugu alimuacha aishi kupalinda na nyingine akafungua duka za bidhaa mbili ili kujilinda.

Mwisho wasiku duka zikafilisika akawa benchi sana pesa ikakata kabisa.

Hiyo hali imeanza kumpata kuanzia miaka ya 2016. So anapitia hali ngumu sana. Alipata total mental break down na baada ya kumpeleka hospital akapata matibabu ya dawa za kumpa usingizi ule wa masaa mengi na akafanyiwa counseling ndipo akaanza kufunguka hizo details.

Kwasasa anatumia hizo dawa za antidepressants ili pale kichwa kinapoanza kwenda speed basi dawa zinazima ubongo na kuuchosha ili asiwaze mambo mengi awaze kulala kichwa kiwe kizito.

Huwa naenda sana kwake kwa wiki at least mara 5 kupiga naye story sana na kumpa mipango ya mjini ile story tu basi at least unamuona anajisikia normal. Na huwa ananipigia simu kuwa amenipikia bata , au kuku au chakula chochote ninachopenda then lazima nitaenda kula hata kama ni saa sita usiku nitapita nile then niondoke.

Kwa ambacho nimegundua ni akili yake haijakubaliana na ukweli kuwa yale maisha mazuri yameshapotea na ile fursa haipo tena kwake, na hakutumia muda ule vizuri kujiboresha na kujiwekeza alikuwa anakula life tu na marafiki au partner matapeli.

Sasa akili bado inamlazimisha kurudi alipokuwa ili arekebishe yale makosa na hapo ndipo msongo wa mawazo unamtokea na kumpelekesha kumpa hali kama ya ukichaa.

I hope baada ya miaka kadhaa atakubaliana na hali na kukaa sawa. MUNGU kama atanisaidia nikiwa vema nataka niongee nae nimtengee kiasi cha pesa aende mbuga za wanyama, halafu atembee mikoa hata mitano mikubwa akae na kutazama mazingira ya tofauti ale vyakula vya huko na kununua bidhaa yaani utalii wa ndani kisha arejee nimtafutie kitu cha kumkeep busy kidogo ili awe na focus kwenye maisha badala ya kuwa na hizi fikra za msongo wa mawazo muda wote.

Namkubali sana shangazi yangu maana ana huruma sana. Na kipindi hicho mimi nilikuwa mdogo sana ila nina uhakika ingekuwa miaka hii na yeye ndio angekuwa njema vile basi kijana ningekula sana maisha na ningekuwa napata sana sapoti yake ila ndio hivyo tena nimekua na kukuta ameshafilisika. So inabidi tu kumsapoti kwa hali yake na mimi hali yangu.
 
Mie mwenyewe nina mashaka na akili yangu.
Kila mtu kuna muda huwa anaingia ile Maniac au psychosis phase ya maisha sasa itategemea na uimara wa ubongo wako na mazingira uliyopo utaweza kutoka au kupatwa na tatizo likawa kubwa zaidi.

Tazama kuna muda unaweza tamani kufanya jambo la kijinga kama kutamani kujirusha ghorofani, kumchapa kofi mtoto kichanga ambaye analia lia hovyo, au ukatamani kumjibu mtu mzima jibu kali ili umkate wenge.
 
Hivi ugonjwa wa akili ni msongo wa mawazo au mkono wa mtu? Na je tofauti ya hzo mbili ni nini?
Ingawa watu wanapenda kusema mikono ya watu yaani ushirikina then huwa nahoji basi ulaya kuna wachawi sana na wanarogana sana.

Maana kule hizi changamoto za matatizo ya akili ni nyingi kushinda sehemu yoyote ile.

Kwa upande wangu, changamoto za kiakili ni matokeo ya mifumo ya maisha.

Miaka ya nyuma vijana na mabinti walikuwa chini ya uangalizi wa wazazi so jambo lolote wangeenda kwa mzazi kwanza kupata muongozo. So hii iliwafanya wasiwe na mambo mengi kichwani.

Imagine leo kuna binti anapata stress nusu ya kupata ukichaa kisa kukosa Ndoa na mahusiano ya kueleweka na hatimae umri unaenda hana familia wala ndoa. Hapa lazima akili zimruke. Ila hili tatizo zamani halikuwapo kabisa sababu wazazi walisimamia show yote. Same kwa vijana wanapotaka kuoa wanapitia changamoto sana siku hizi tofauti na zamani.

Zamani wanandoa wanakaa kikao na wazee kusuluhisha changamoto za mahusiano yao na hii ilipunguza sana marumbano na mifarakano hata kama mtu alikuwa na viburi na jeuri hazikufua dafu mbele ya wazee maana alikaripiwa na kusemwa kama sio kusutwa kwa tabia zake za hovyo na kupewa amri ya kubadilika ama angetengwa na familia na ukoo.

Ila sasa mtu anatabia za hovyo wazazi wanashauri juu juu bila kuweka adhabu au mkwara mzito wenye maagizo yanayotaka utekelezaji na sio kubembelezana na hata muhusika akionyesha kutotekeleza maazimio kwa asilimia 100 basi huwa hakuna sanctions miaka hii. Matokeo yake watu wanaishi wakideal na maumivu, hasira, huzuni, kutoridhika, na hii huchangia kuleta shida kwenye ufanisi wa akili.
 
Màana ukienda hospitalini utaambiwa ni ugonjwa was akili unasababishwa na msongo wa mawazo, ukienda makanisa ya walokole utaambiwa ni suala la kiroho
Kuna mchungaji alikuwa anamuombea bi mkubwa. Shida iliyotokea ni bi mkubwa alisafiri kwenda mkoani kusafisha makaburi. Ya familia huko.

Sasa aliporejea naona zile purukushani za pikipiki huko milimani katika kusalimia ndugu na jamaa. Akawa ameshitua mwili wake eneo la mbavu na misuli ya mgongo.

Unajua unapofanya movement yoyote ya ghafla ghafla, misuli lazima ifanye kuvimba au ili kuprotect skeleton yako ambayo inaprotect organs zako za ndani.

Sasa alienda hospital akapewa dawa za inflammation jambo ambalo lilikuwa ni kosa sababu yeye hajapata kesi ya inflammation alipata kesi ya muscle contraction au misuli kuvimba yaani mfano ukipigwa rungu kwa nguvu hapo kwenye mkono utavimba kinachotokea hapo ndani ya mwili wako kumetokea inflammation hilo eneo la uvimbe yaani kwa ndani kwenye msuli ulipopigwa.

Ila ukifanya mazoezi kwa nguvu isivyo kawaida yako misuri inaweza vimba pia lakini hapa itakuwa ni misuli yako imekakamaa au contractions imetokea na utahitaji dawa ya relax misuli ili iache kuuma na urudi sawa.

Sasa bi mkubwa walimpa dawa na kumchoma sindano za inflammation hazikumsaidia maumivu ya misuli yakaanza kupanda kwa kasi kuelekea shingoni. Akaanza kupata maumivu ya kichwa eneo la misuli ya shingo.

Akaenda kwa mchungaji, akaanza kupewa sasa maombi mchungaji anamwambia kuwa alienda huko makaburini anaona kuna roho zilimvaa na zimekasirika kwann hayupo kwenye ibada ya mizimu ndizo zinamuandama na atahitaji maombi ya wiki na kufumba.

Sasa nilipokwenda msalimia ndio nikakuta hizo story. Nikamwambia niletee dawa ulizotumia. Aliponionyesha nikaelewa tatizo lipo wapi. Nikatoka muda huo huo nikaenda Upanga haraka nikaenda mnunulia dawa za kurelax misuli haraka nikamleta akameza mchana ule akalala maana hakuwa poa hata kuketi. Muda mrefu.

Akaamka na usiku baada ya chakula cha jioni akameza alipoamka asubuhi siku ya pili kaamka fiti kama sio yeye aliyekuwa anashindwa hata kuongea vizuri kwa maumivu.

Nikamwambia hawa watu wenu wa makanisani muwe nao makini sana. Wengi wao hawajui wanachokisema wanapiga ramli tu kama waganga wa kienyeji.
 
Nimewahi ugua ugonjwa wa akili nikiwa mtu mzima ila kwa neema ya Mungu nimepona kabisa na naamini Mungu ndiye amenipigania mpaka sasa; nilikuwa navua nguo barabarani; napiga watu; natukana; naongea mambo hayaeleweki; nimekutana na mauzauza; ila Mungu ameniokoa na kukua hujafa hujaumbika; ila imenifanya kuwa imara kiimani, kikubwa cha kujua kwanza ugonjwa wa akili ni ugonjwa kama magonjwa mengine, mgonjwa wa akili ajijui kama ni mgonjwa, mgonjwa wa akili anaweza ongea/muumiza mtu yeyote pasipokujua anakosea; msaada mkubwa nilipatiwa na madaktari wa muhimbili kuna kitengo maalumu kabisa kwa ajili ya wagonjwa wa akili;
Kwa sasa ni mwaka mmoja tokea nimeacha dawa zao, nina mpango wa kwenda kumsalimia Dr wangu wiki hii
Ulikuwa diagnosed na tatizo gani la kiakili?!
 
Nimewahi ugua ugonjwa wa akili nikiwa mtu mzima ila kwa neema ya Mungu nimepona kabisa na naamini Mungu ndiye amenipigania mpaka sasa; nilikuwa navua nguo barabarani; napiga watu; natukana; naongea mambo hayaeleweki; nimekutana na mauzauza; ila Mungu ameniokoa na kukua hujafa hujaumbika; ila imenifanya kuwa imara kiimani, kikubwa cha kujua kwanza ugonjwa wa akili ni ugonjwa kama magonjwa mengine, mgonjwa wa akili ajijui kama ni mgonjwa, mgonjwa wa akili anaweza ongea/muumiza mtu yeyote pasipokujua anakosea; msaada mkubwa nilipatiwa na madaktari wa muhimbili kuna kitengo maalumu kabisa kwa ajili ya wagonjwa wa akili;
Kwa sasa ni mwaka mmoja tokea nimeacha dawa zao, nina mpango wa kwenda kumsalimia Dr wangu wiki hii
Usiache...dawa..hali itarudi kama.zamani

Dawa za mngonjwa wa akili anatumia hadi anakufa
 
Back
Top Bottom