Magu, Mwanza: Rais Samia ashiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi za Tanzania, atawazwa kuwa Chifu wa Machifu

Angeenda DC inatosha, matumizi mabaya ya fedha za umma
Magufuli kila tukio alikuwa akifanya yeye ikiwa ni pamoja na kuzindua stendi na masoko vitu ambavyo wala havikuhitaji hata kuzinduliwa na mtendaji wa kata lakini wala hamkusema,utaumia bure tambua tu kuwa aliyepewa kapewa wewe mwenzangu na mie utaishia kusaga lami.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan asimikwa rasmi kuwa Mkuu wa Machifu Tanzania leo tarehe 08 Septemba, 2021 katika Viwanja vya Redcross Kisesa, Magu Mkoani Mwanza na amepewa jina la HANGAYA lenye maana ya Nyota Angavu.
 
Ningependa kusikia mwakani machifu wa makabila mengine nao wanafanya tamasha kama hili! Tamasha linasemekana limeandaliwa na umoja wa machifu Tanzania na wsmemtawaza kuwa chifu mkuu wa machifu!

Utamaduni wetu huwa hakuna chifu mwanamke, labda malikia. Mwakani kabila jingine likifanya tamasha nalo likamtawaza kuwa chifu mkuu wa Tanzania! Ninaona kama vile tamasha limeandaliwa na machifu wa usukumani tu na lilihusu utamaduni wao tu.
 
Ofisi yake ya kienyeji itakuwa wapi huko usukumani? 😁
 
Yaani huko mwanza wao ni uchifu ndio wanacho weza akienda wa chadema utasikia amesimikwa chifu akienda wa CCM utasikia amesimikwa chifu

Haya mambo ya wanasiasa ni magumu kuyaelewa
 
Posho ya kuwa chifu kwa mwezi ni tsh. ngapi?

Anyway kuna kuwaga na marupurupu yoyote??
 
Kweli kua uyaone. Haya mambo ya kuvaa kaniki hadharani yanaashiria nini? Tena toka kwa waganga???
 
Kuna platform huko wanamnanga chief Hangaya na picha za Royal Tour...

Watu wa branding wamechafua picha.
 
Tangu lini wasukuma wakawa na chief mwanamke ?

Acheni kunajisi tamaduni za watu.
 
Huyu mama hata akija kuwawekea mabunda ya pesa milangoni mwenu bado mtamchukia tu, chuki si kitu kizuri hata kidogo, inamtafuna mtu taratibu na madhara yake atayapata mwenye chuki na si mchukiwa
Tena hao ni bavicha. Sijui Wana shida gani na Mhe. Rais Mama Samia
 
Rais na waziri mkuu wanazidi kukusanya watu hawajali korona lakini wakijaribu wapinzani wanakamatwa Mara moja!
 
Wasukuma wanautaratibu wa uongozi wa Mila ndiyo maana watemi bado wanaheshimika makabila mengine yalisha kuwa westernized.Karibuni usukumani mjifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…