Magu, Mwanza: Rais Samia ashiriki Tamasha la Utamaduni, Mila na Desturi za Tanzania, atawazwa kuwa Chifu wa Machifu

Hongereni kwa kumpa jina sahihi "Hangaya" yaani peupe, pasipo na kitu, n.k
 
1.Kwa wasukuma,hakuna chifu wa kike.
Ni danganya-toto tu.
2.Halafu mbona mechi ya Taifa stars jana walikataa mashabiki sababu ya korona?
 
RAIS SAMIA NI NYOTA INAYONG'AA

Ukweli haujifichi, ilikuwa ni swala la muda tu Tanzania na Duniani kote kuona nyota kuu inayong’aa kwa Rais wetu kipenzi Mama wa Vitendo Samia Suluhu Hassan.

Leo umoja wa Machifu wamedhihirisha hilo katika tukio la kipekee sana huko Bujora Mwanza ambapo kwa pamoja umoja huo wa machifu wamempa Rais Samia jina la HANGAYA yaani nyota inayong’aa.

Hii ni siku chache tu baada ya Umoja wa Mataifa kupitia Benki ya Dunia kuidhinisha kiasi cha takriban Dola za Marekani 567 kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kupambana na athari zilizotokana na UVIKO 19

Nyota ya Rais Samia inaangaza Afrika na Dunia nzima, Tarehe 04 mwezi huu Rais Samia alitajwa miongoni mwa wanawake bora Duniani kutoka Afrika wenye ushawishi mkubwa zaidi.

Chini ya uongozi wa Chifu HANGAYA Tanzania inaenda kuwa kilele cha utalii Afrika kupitia filamu ya Royal Tour ambayo Starling ni Rais mwenyewe, the Master-mind, Amiri Jeshi Mkuu, Mama wa Vitendo Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania.

Nyota ya mama inafanya maajabu, Amani imetawala nchini, Miradi ya kimkakati inakwenda kwa kasi, wakulima wa cacao wanashangilia, ni fahari kuishi Tanzania.

Chifu HANGAYA, hapoi, yeye anasema Kazi Iendelee
 
Huyo sio nyota inayong'aa bali ni kimondo kilichoungua
 
Mkuu maisha mtaaani magumu Sana, vitu bei iko juu mno.
Biashara zitakufa
 
Hivi kuna ma chifu wa kike? Haya yote ni maigizo ya kusahaulisha tozo za kijinga zinazoendelea.
 
Mama Samia raisi wetu amepewa jina zuri la matumaini kwa kadiri ya lugha yetu ya kusukuma si tu sifa ya nyota hiyo kua nyota ingaayo Ina nyongeza kua nyota hiyo huchomoza karibu na asubuhi baada ya usiku yaani dalili ya mapambazuko hujulikana "hangaya"nyota ya asubuhi" morning star nyota hiyo ndiyo hung'aa Tena jioni Kama "jitanga bazugi" yaani hung'aa kabla ya wapishi ni sifa hizo watemi wamechagua jina la nyota ya asubuhi(hangaya)
 
Huyu mama anachezewa sasa nina mashaka na usalama wake, TBS wameipima viwango hiyo ngozi!?
 
Masizi em mtuambie Sera ya viwanda tumeiacha?
He, saivi Sera ni matamasha na filamu kufurahisha watalii?
Nikama hatujui tunataka nini?? Inasikitisha sana tunavyopiga makitaimu na kusifia maujiii maujinga
 
Kapendeza BWANA ,alipenda Sana Mabutu faa ngozi ya chui ,ila simanishi anatabia Kama za yule mwamba tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…