Pamoja na kukusihi usome bila 'prejudice' kuona hoja za wengine, napenda nikujibu swali lako kama ifuatavyo
1. Endapo kupandisha hadhi za hospitali hakuna effect katika accessibility ya huduma za afya, basi haingekuwa na maana ya kuzipandisha hadhi! Hii ni kwa mujibu wako
2. Kupandisha hadhi ya hospitali ni suala la kitaalamu likizingatia vigezo vinavyopaswa.
Miongoni mwa vigezo hivyo, ni wataalam hasa specialists na vifaa.
Si jambo la kisiasa, kuamka asubuhi na kutangaza Hospitali X ni ya rufaa kama tawi la chama kuwa ofisi ya mkoa asubuhi moja kwa matakwa ya kisiasa
Huduma zetu kama alivyosema
Mchambuzi ni primary , secondary na tertiary. Tetiary ndiyo referral hospital.
Utakubaliana nami ya kuwa Hospitali za mikoa hazina hadhi ya kuwa referral
a)Hazina wataalamu wa kuzi qualify kama referral Hospitals
b)Hazina vifaa vnavyoweza kukidhi haja ya referral hospital
Mgonjwa akitoka kituo cha afya kwenda Hospitali ya Wilaya, likely atakuwa na referral ya Clinical Officer. Huko Wilayani atakutana na Assistant Medical office (AMO).
Naye anaweza kumfanyia referral Hospitali ya mkoa. Hapo ndipo tatizo lililpo
Hospitali za mikoa bado zina upungufu wa Medical officers( Dr) na mgonjwa atapata huduma ya Clinical officer au AMO na kwa bahati Dr. Hakuna Specilists
Hata kwa zile zenye Specialists, bado wanafanya 'clinical work' kwasababu hawana vifaa vya kuwawezesha kutenda kazi zao.
Mathalani, mgonjwa aliyepewa referral kwa matatizo ya maumivu makali ya tumbo akiwa mja mzito, kuna differential diagnosis nyingi nyuma yake
Inawezakana kuwa ni ruptured appendicitis au ectopic pregnant
Huko mikoa X-ray hazifanyi kazi na haziwezi kutoa diagnosis kwasababu kazi yake ni imaging, na inapokuwa suala la soft tissue ni useless.
Vifaa vinavyoweza kutoa mwanga au diagnosis ni kama Ultra sound au MRI.
Hospitali ngapi zina vifaa hivyo nchini achilia za mikoa?
Wataalam katika ngazi ya Clinical officer au AMO hawana uwezo wa kufanya invasive therapy kwasababu ni nje ya wigo wao(isipokuwa simple procedure kwa AMO)
Ikitokea Medical officer anafanya kazi hiyo, naye anaweza kukutana na kikwazo.
Kwanza, atategemea history na clinical examination na pengine ku opt Laparotomy.
Hapo inaweza kumlazimu atafute Obstetric and Gynaecology (OBGY) specialist aje kutoa ushauri au kufanya complicated procedure kama Hysterectomy ikitokea.
Je, specialists wa OBGY wapo wangapi mikoani?
Mfano wa pili, huko mikoani kuna archaic x-ray tech ambayo ina limitations nyingi katika diagnosis. Ni Hospitali ngapi za mikoa zina technology Zaidi ya hiyo?
Hoja hapa ni kuwa kupandisha hadhi hospitali kwa matamko ya kisiasa ni kutoa 'false hope' Ukweli,Hospitali za mikoa hazina hadhi hiyo, na kuzipa hadhi ni kuwadanganya wananchi.Ni kuwa limiti wasipate huduma haswa za hadhi ya referral hospital.
Ni kuwanyima accessibility kwa kuwadanganya
Kumbuka, Hospitali za mikoa zinapata mgao wa resource kama za rufaa, je ni kipi bora, kuziimarisha katika huduma au kuzipandisha hadhi ili zi compete na referral Hospital katika limited resources tulizo nazo zikitoa huduma below stnd?
Nikusikilize kwanza