Kobello,
Mara ni opinions, mara ni theories. Is an “opinion” synonymous to a “theory?”
Kama ‘opinions’ zangu zipo kwenye articles na vitabu vingi tu, wewe ‘facts’ zako unazitoa wapi? They are not grounded from theory and practice?
Maajabu haya.
Kwanini unaendelea kukwepa nilichowasilisha na kukuhoji kuhusu allocation objectives vis a vis practice, hasa jinsi gani serikali inakiuka kile ilichopitisha yenyewe?
Unaposema bora zipewe allocation powers, is that your opinion? Is this argument available in a variety of papers and books or its your ground theory?
Unapenda kukimbilia hoja nusu nusu nusu kwa sababu lengo lako hapa sio kuja kuelewa, kueleweshana na kuelimishana bali kuja kutoa vijembe na lugha za kejeli kwa nia kuvuruga na kuchafua mjadala ili kufurahisha wakubwa zako huko CCM. Suala la LGAs ambazo zina - face discrepancies in tax bases nilizijadili kwa kina pamoja na kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike. Zipo baadhi ambazo zina matatizo haya, na hiyo isiwe sababu for you to generalize mambo.
Unaposema kwamba ingekuwa bora kuzipa LGAs taxation powers kama tungekuwa advanced ni kujichanganya tu. Zipo LGAs zenye uwezo, nyingi tu, na iwapo fiscal autonomy ingekuwa expanded ingepelekea competition, growth, hence welfare kwa wananchi katika jurisdictions husika.
Tax compliance katika LGAs inaweza kuongezeka kama kuna fiscal devolution kwa sababu tax outcomes will be felt locally badala ya sasa ambapo hata kodi ya majengo within a LGA, serikali kuu inaitolea macho.
Hauwezi kuona ukweli tunaojadili humu na utaendelea kuuponda kwa sababu unaingia humu kwa kofia ya Ukada tena wa chama (CCM) kilichoshindwa kuletea wananchi mabadililo kwa miaka 50 ya uhuru, lakini badala kukubali kushindwa ili taifa lisonge mbele, mnapigana kufa na kupona kuaminisha watanzania kwamba
kama imeshindikana chini ya CCM, basi haiwezekani nje ya CCM.
Unahangaika sana. Nimekueleza kwamba zipo LGAs ambazo zilikuwa zina uwezo to meet their financial needs by up to 80%, na kama tungekuwa serious with devolution, zingeweza hata kufikia 100% kukidhi mahitaji yao. Lakini badala yake serikali imekuwa ikiendeleza mkakati wake wa kuzibana kwa kuzipora vyanzo vya mapato ili ziwe tegemezi kupitia central government transfers/grants. Nikuulize:
Halmashauri kama vile Ilala, Kinondoni, Moshi, n.k, kwa akili isiyo na kilevi na macho makavu unataka kutuaminisha mchana kweupe kwamba hizi bila kusaidiwa na central government kwa zaidi ya 70% hazitaweza kujihudumia? Seriously?
Hivi kweli unaelewa maana ya Bureaucracy?
Tukizipa LGAs taxation/revenues powers:
-Itazisaidia ziweze kuja na mipango na mikakati kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe kwa jinsi wanavyoona inafaa. Hilo hamtaki, na unaendelea kujadili viroja vya allocation powers wakati hata hizo mmezivuruga. Whats been practiced isn’t what was envisaged by the same government/ccm. Nilijadili hili huko juu.
-With taxation powers, itakuwa ni rahisi kwa halmashauri zetu kutambua (identify) fursa zilizopo katika mazingira yao.
-Itazipatia LGAs uwezo to utilize
rasilimali nyingi tu ambazo leo hii zinawazunguka lakini faida yake inachumwa na Dar-es-salaam kama sio Dodoma.
-Itasaidia LGAs to identify ‘competitive advantage on which development can be based. Suala hili litapelekea maendeleo kuwa ‘locally driven’ badala ya kuwa driven and determined by external agents (hasa bureaucrats waliopo Dar-es-salaam na Dodoma) ambao from experience ya kipindi chote cha uhuru, mara nyingi huwa more pre-occupied na vipaumbele vingi na pia wasio na uelewa wa kutosha kuhusu potential local development katika halmashauri zetu mbalimbali.
Hapa pia nikuulize:
Hivi Waziri wa Tamisemi (JPM – kwani maana ya waziri wa nchi, waziri ni Rais) anawezaje kuamua kufuta sherehe za uhuru na kuelekeza bajeti husika kwenda Mwanza? Mwanza na uhuru kuna uhusiano gani?
-Kuzipatia LGAs taxation powers kutafanikisha mipango mingi ya maendeleo ambayo ni shirikishi (participatory development projects) kwa sababu LGAs zitakuwa na resource and motivation zaidi ambapo mipango ya maendeleo itahusisha wadau mbalimbali kuja na ‘collective vision’ kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe - ‘local development’. Vile vile kutawapatia fursa wadau husika kuja na makubaliano juu ya ‘common goals’ pamoja na mikakati ya kufanikisha malengo husika. Tafiti nyingi zinzendelea kuonyesha kwamba ‘participation of local communities’ katika mikakati ya maendeleo husaidia sana kupunguza kasi ya umaskini.
What a contradiction. On the other hand,
wanaweza afford kununua insurance, but on the other hand
hawatakuwa na uwezo wa kulipa kodi kwa ajili ya kufanikisha kile kile. Mbabaishaji ni mbabaishaji tu.
Haujajibu swali, ulichowasilisha ni vurugu tu mostly kwa makusudi to derail the issue at hand. Tafadhali rudi na jibu la moja kwa moja.
Upeo wako unatuonyesha kwamba hata mambo mengine ya msingi umetumwa kuja kuyapinga. Katika hili, kwanini awali ulikuwa unakataa hoja za
Nguruvi3?
Kwahiyo unataka kutuambia kwamba matumizi makubwa ya fedha za serikali kibajeti yapo ngazi za chini za mfumo wa afya kuliko ngazi za juu?
‘Freedom’ hapa una maanisha kitu gani?
Usijaribu kuvuruga hoja kwa takwimu. Whether its 18%, 5%, 0.001%, hiyo ndio tunayoijadili kwa maana ya budget allocation ya serikali katika sekta ya Afya.
Pia awali nilijadili hoja kwamba LGAs zina jukumu la kukusanya not more than 10% ya mapato ya serikali lakini zina jukumu la kuchangia matumizi ya serikali kwa zaidi ya 20%, umekimbia huo mjadala.
Pia suala la allocation unaendelea kukataa ukweli baina ya kilicho dhamiriwa wakati wa utambulishaji wa allocation system vis a vis kinachotekelezwa sasa. Nilieleza jinsi gani Serikali kuu imeacha kufuata allocation system iliyoibun na ambayo iliamini kwa dhati kwamba italeta tija. Since then, kinachoendelea ni natifua tifua tu kupitia ofisi ya rais.
Usisahau kwamba grants nyingi zinazoenda ngazi za chini zinakuwa attached na conditionality na serikali kuu, on how to spend the funds. Kwahiyo unapoendelea kung’ang’ania kwamba allocation powers zipo huko chini ni kuendelea kung’ang’ania hoja mufilisi.
Usijifanye hauelewi swali langu.
Nilikuuliza swali husika baada ya hoja yako mufilisi ambapo ulisema hivi:
Nirudie tena, zipo LGAs ambazo zilikuwa na uwezo wa kukusanya karibia 80% ya mapato yanayohitajika kufanikisha matumizi kwa ajili ya maendeleo. Lakini baadae, uwezo husika ukaporwa na central government kwa nia ya kuzigeuza kuwa tegemezi kwa serikali kuu. Ninarudia tena swali langu, je:
· Hii deficit ya sasa katika LGAs husika inatokana na hizo LGAs kushindwa to fund themselves???
Umemalizia vizuri kwamba its just your opinion. Vinginevyo ukweli wa hoja zako hauonekani, na haujawahi kuonekana zaidi ya ukweli kwamba katika kila mjadala, ujira wako ni kuitetea CCM on Jamiiforums.
Kwenye deni la taifa umefinyanga finyanga umeshindwa, ukakimbia. Haujanirudia na hoja mbadala nyingi tu katika suala hilo.
Kuhusu Afya, hauwezi kuona jipya kwa sababa as I indicated earlier, mtazamo wenu CCM ni finyu sana na uliojaa ujuaji mwingi. Kwa vile mmeshindwa kwa miaka 50 kuinua maisha ya watanzania, basi upande mwingine wa hoja ‘hauna jipya’.
Mimi sipo humu kutafuta thousand of views. Kama it was all about seeking a quantitative discussion (and not qualitative), ningeweka bandiko kwenye ‘jukwaa la siasa’, and you and I know kwamba kwa kufanya hivyo, uzi huu ungekuwa umeenda mileage kubwa but ‘to nowhere’.
Ukweli ni kwamba you only emerge pale interest zenu zinapoguswa, that’s when they unleash you. Nje ya hapo, you are a disappearing act.
Hoja zetu ni Mwiba mkali, vinginevyo usingepoteza muda wako kuja humu.
Kila wakati nikipandisha uzi, wakubwa wako wananipigia simu, wengine ambao wapo kimsukule kama wewe humu wananitafuta inbox na kwenye email.
Yea right!