JPM tutakukumbuka daima!
Kumbuka tu siku za kumuaga JPM alipofariki ndiyo utajua kwa kiasi gani alipendwa na wengi.
Wachache wenye nguvu hadi leo wanaendea kufinance movement ya kumtweza JPM, mwaka moja baada ya kufariki!
Ni kitu kinachoshangaza kwamba kuna vyama vya siasa wametenga muda na fedha za kuendelea kumchamfua mtu aliyekwish fariki zamani!
Sababu, alisimamia ukweli uliokubalika sana na wengi, kwa hiyo vyama hivyo vinavyoendeshwa kwa uongo na propaganda chafu vinaelewa si chochote ukilinganisha na aliyoamini na kusimamia Magufuli.
Kwa hiyo kwa akili zao suluhu ni kumchafua ili wapate ahueni ya kutokosolewa kwa mifano mkzuri ya JPM!
Na kwa sababu wenye sauti kwenye vyombo vya habari ni wachache, wana set agenda zisizoendana na matatizo na matamanio ya wengi!
Fikiria kipindi cha Magu, sukari ikipanda kwa shilingi 300 kelele za nyumbuzu nchi nzima na hata vyombo vya kimagharibi!
Sasa hivi maisha yamekuwa magumu sababu bei za vitu zimepanda mnooo, lakini usikii wale waliokuwa wanaongoza kwa kelele wakisema lolote!
Bei ya petroli juu, mafuta ya kula imepaa, vifaa vya ujenzi ni balaa, nk,
Magu stood for masses, na aliahidi yuko tayari kufa kwa ajili yao! Msimamo haukubadilika hadi mauti.
Alikuwa kiongozi mwenye maono na alisimamia utekelezaji kwa juhudi na ubunifu wa hali ya juu.
Jina la Tanzania lilipaaa kwa wapenda maendeleo ya kweli.
Na katika kufikia ndoto zake hakucheka na wakwapua mali za nchi, wawe watanzania wenzetu au mashitika ya kinyonyaji ya nje!
Wengi hatukushangazwa na propaganda za vyombo vya habari vya mabeberu kumpaka matope Magu, ndivyo wsnavyofanya kila kukicha!
Rest in Peace uncle Magu.