Magufuli alikuwa muongo sana

Alichozungumza hapa ni kweli, japo sio kipindi cha JK, lakini kuna wakati miaka ya 96 hivi walikuwa wanachelewa sana kupokea mshahara. Mfano wik iliyopita ndio unakuta wamepokea ya mwez uliopita. (Wa 5) ilikuwa kawaida.

Mkuu miaka hiyo iliathiriwa na teknolojia, mishahara ilikuwa inachukuliwa dirishani na zisafirishwe toka Benki Kuu, kwanini isichelewe
 
Ni lini mishahara ililipwa tarehe 15 au 20 ya mwezi unaofuata?

Mimi sikumbuki aisee kwenye utawala wa Kikwete sikumbuki nasisitiza kama kuna mtu anakumbuka aniambie.
View attachment 1831163
Angeendelea miaka mitano tena, angebadili katiba na kuwa rais wa maisha.
Kina Bulembo, Sanga na hata Ndugai walishaanza kupiga ndogondogo kubadili katiba.
 
Utapigana na marehemu mpaka lini? Je! Ukimshinda marehemu unataka zawadi gani?
Aliposema nitawajengea flyover Dsm ni muongo! Aliposema nitajenga mji wa serikali Dodoma! Aliposema tutajenga mtambo wa umeme rufiji ni muongo! Alposema elimu bure ni muongo. Tusidhalilishe hayati haitusaidii sana kimaadili. Tuwe na kiasi kwenye kauli sote ni waja wake.
 
Alisema pia nchi yetu haina corona na kuwa ata mapapai yameonekana na corona kwa mujibu wa vipimo vya maabara
 
Nimesoma mpaka kwenye elimu bure nikaacha kusoma
 
Magu alikuwa mtu wa fix sana.. alisema Saddam Hussein ni rais wa Kuwait, mara tunajenga kwa hela za ndani wakati amekopa kuliko marais wote waliopita , kakuta deni la nchi ni trillion 36 ( ndani ya miaka 55 ya uhuru) yeye amekopa mpaka trillion 61( Trillion 25 peke yake, na tena ni ndani ya miaka mitano tu). Sijui angemaliza miaka 10 angekopa sh ngapi! Chizi kweli lile
 
Aliposema tunajenga kwa fedha za ndani wakati anakopa kila uchwao alikuwa mkweli? Kama mkweli deni liketoka wapi?

Wenzie mbona wamejenga vitu vikubwa tu na vinakumbukwa hadi leo hii mbona hawakuwa na sifa na matangazo kama alivyo kuwa anataka yeye? Kufanya machache kwa ukweli hakumuondolei kuwa alikuwa muongo.
 
Mpaka kuna wakati nikikumbuka amekufa, najiuliza hivi ni kweli amekufa yule muuaji ama naota! Alikuwa anatupeleka kuzimu, na mbaya zaidi alikuwa anatengeneza mazingira aongezewe muda wa kutawala kupitia kwa chizi lingine la mirembe, " atake asitake!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…