Kwenye medani ya uongo na uzandiki mbona hana mpinzani huyo. Anapita bila kupingwa wala hafanyi hata kampeni (CV yake inambeba kishenz).
● Alituambia tuwachange bukoba wahanga wa tetemeko waliovunjiwa nyumba zao. Tukajikaza kiaskari na kujibana watanzania kuwachangia. Waulize kama waliona hata Sh 100 ya ujenzi wa nyumba zao.
● Alituambia kila mwalimu atapewa Laptop. Waulize kama amepewa hata mmoja.
● Alituambia kila kijiji atawapa Millioni 50 kwaajili ya kufanya maendeleo na uchumi. Waulize kama waliiona hio hela.
● Alituambia wafanyakazi sekta za umma/walimu, wataongezewa mishahara na madaraja kabla hajaondoka. Waulize kama wameongezewa hizo nyongeza za mishahara na madaraja (Labda madaraja ya ubungo na mfugale ndio wameyaona).
● Alituambia tutalipwa hela ndefu kwenye fidia ya makinikia. Kila raia noah moja moja. Waulize kama mabeberu walitoa hio hela.
● Alituambia Tanzania tutatoa misaada kwa wazungu, sisi ni "DONA KANTRI". Hakuna cha donna wala sembe, ni mwendo wa hali ngumu mpaka skin tight kupwaya mitaani.
● Alituambia serikali yake kutakua hakuna wizi wala ufisadi, na atakefanya ufisadi wa hela basi zitamtokea tundu lolote. Mbona yeye na kina Ole Sabaaya na Makonda walifisadi nchi na kuiba.
● Kwenye kutupa idadi za samaki, watoto wa samaki pamoja na mayai yao kwenye Ziwa Victoria na Baharini. Wala tusipagusie kabisa, tuache hio issue siku ingine.
Yule mzee sio kabisa. Siku alivyofukiwa mpaka malaika watoa kichapo waliokua likizo, ilibidi waitwe kazini kwa dharura kumpokea.