Somo la Pili
2. Kibali ni cha kazi gani?
Kibali ni cha kutimiza lile jukumu la kibali ulichopewa,kama tulivyoona kwenye somo la kwanza, kuna vibali tofauti vya kufanya mambo tofauti tofaouti, ukipewa kibali cha ndoa,inatimiza majukumu ya ndoa,ukipewa kibali cha kufanya biashara,unafanya biashara kwa mujibu wa leseni yako。
Kuna vibali vingi,hadi vibali vya kuua,licence to kill,hata mtu anayehukumiwa kunyongwa,hukumu hiyo haitekelezwi hadi mkuu wa nchi asaini death warrant ndipo anyongwe
Hivyo hata kibali cha kutawala nchi,unatawala kwa mujibu wa kibali chako
japo kibali cha kutawala nchi kimetolewa kwa mujibu wa katiba,anayepewa kibali hicho anapewa na YEYE na anapaswa sio tuu kufuata katiba,bali pia kutimiza madhumuni ya YEYE alIyempa kibali hicho,alimdhamiria afanye nini,kibali chake ni cha nini na kwanini ni yeye na sio mtu mwingine yeyote?
Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
Kama nilivyoeleza, kibali kinatolewa kwa madhumuni kusudiwa, au kuna vibali vya kazi maalum, task force, ukiisha ikamilisha kazi, unakuwa rewarded accordingly, kibali kimekamilika na kazi ya kibali hicho inakuwa imekwisha.
Musa kibali chake kilikuwa ni kuwakomboa tuu wana wa Israel kutoka utumwani Misri, alipokamilisha kazi ya kuwaondoa na kuwasafirisha mpaka nchi ya ahadi, kibali chake kikakamika, yeye hakuingia nchi ya ahadi, alitwaliwa, na kibali cha kuwaingiza nchi ya ahadi, kikatolewa kwa mtu mwingine.
Kwa vile kibali, ni kibali cha kazi maalum kwa mtu maalum, ukiwa ni mtu mwenye kibali, usipokitumia kibali hicho kikamilifu, kibali hicho kinafutwa!.
Ufutaji wa vibali au ufutwaji wa vibali, hufanyika kwa namna mbili
1. Ufutwaji wa uwezo wako, kufutwa, mtu alikuwa mfanyabiashara mkubwa maarufu na tajiri, anafilisika hadi kubaki apeche alolo!. Mtu alikuwa msanii mzuri, mwanamuzi mzuri, mchezaji mzuri, ghafla uwezo wake unashuka, anajikuta anatupwa nje ya gemu.
2. Ufutwaji wa kibali wa aina ya pili ni kwa wewe kufutwa kwenye uso wa dunia, kwa kutwaliwa!, kama inavyotokea kwa wengi wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana. Musa, Kanumba, Sembuli, Mbaraka Mwishehe, Shaaban Robert, John F Kennedy, Bruce Lee, JPM na wengine wengi, wameitwa kurejea kwa Muumba wao.
P.