Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Wanabodi,

Leo, naendelea na zile mada zangu za kwa maslahi ya taifa。Leo naendesha somo la kitu kinachoitwa “Kibali”
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike,naanza na Outline
  1. Kibali ni nini?
  2. Kibali ni cha kazi gani?
  3. Kinatolewa na nani?
  4. Kinatolewa kwa nani?
  5. Sifa za Kibali ni Kisipotumika,kinafutwa!
  6. Je Rais Samia ni Kibali?
  7. Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?
  8. Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
  9. Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au tumuachie mwenyewe?
  10. A Way Foward 2025
Paskali
Samia kibali chake kinaisha 2035 inshallah, baada ya katiba mpya 2025 ndio anaanza muhula wake wa miaka kumi....
 
Wanabodi,

Leo, naendelea na zile mada zangu za kwa maslahi ya taifa。Leo naendesha somo la kitu kinachoitwa “Kibali”
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike,naanza na Outline
  1. Kibali ni nini?
  2. Kibali ni cha kazi gani?
  3. Kinatolewa na nani?
  4. Kinatolewa kwa nani?
  5. Sifa za Kibali ni Kisipotumika,kinafutwa!
  6. Je Rais Samia ni Kibali?
  7. Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?
  8. Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
  9. Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au tumuachie mwenyewe?
  10. A Way Foward 2025
Paskali
Kwani Katiba iliyopo inasemaje kuhusu hicho KIBALI ???!!

Tanzania inafuata Katiba !
Ndio maana watu wajanja wakasema-
Locuta causa finita ! 🙏🙌

Au nasema uongo ndugu zanguni ???!!
 
Samia ni rais pekee katika marais waliiongoza nchi ambaye hapendwi na anaowatawala na hana ushawishi wowote.. tazama hata hotuba zake utafikiri anahutubia mwenyekiti wa kitongoji.. miaka michache iliyopita kuna kiongozi aliteka hadhira ya watanzania na kila ilipofika jioni watu walijazana kwenye tivii kusikiliza hotuba zake.
 
Mungu siyo mungu please
Hii ndio shida yetu watanzania, is the word (God/god) a common noun or proper noun if we want to get linguistic on what deserves a capital letter.

Not to mention was he/she the main theme of my responseh, for that word to be a marking point?

You can cannot waste your time on analysing text with nonsense, that is not how lecturers mark academic writings.
 
Somo la Kwanza
  1. Kibali ni nini?
Kibali ni ruhusa ya kufanya japo fulani,ambalo ili ulifanye ni lazima upate kibali au ruhusa kutoka mamlaka husika。Kibali cha kikuu cha kwanza kwa binadamu baada ya kuumbwa ni kibali cha uhai,kibali cha kuishi na kibali cha kuumba binadamu wengine。Baada ya hapo ni kibali cha kufanya kila kinachofanyika。Kibali kwa mwanamke kuwa mama na mwanaume kuwa baba,ni kupevuka,kibali cha kujenga familia ni kuoa,kibali cha kujenga nyumba ni kumiliki ardhi,kibali cha kufanya biashara ni kuwa na leseni,kibali cha kusafiri nje ni kuwa na passport,kibali cha kuingia nchi fulani ni kuwa na visa, hivyo vibali viko vya aina nyingi。

Kuna aina kuu mbili za vibali,vibali vya kidua,hivi ni vibali ambavyo kila mtu anaweza kuomba na kupewa kama business licence,passport,visa,kugombea uongozi,kupigiwa kura kushinda uongozi na kuwa kiongozi。

Kuna vibali ni vipawa,karama na vipaji kutoka kwa Mungu mwenyewe,hapa hauombi wewe,unazaliwa nacho ama unatunukiwa,

Kibali ninacho kizungumza kwenye uzi huu ni kibali cha karama na kipawa cha kutawala nchi,kuwa mkuu wa nchi。
P
 
Mungu siyo mungu please
Kukusaidia tu na wenzako kwenye kukutoa kwenye dhana potofu uliyonayo.

Kwenye academical marking kwa nchi za wazungu that’s not how they assess your work.

If they gonna give you an essay question or a report to write, it’s the methodology, structure and theories applied in justifying your answer that matter the most.

Quit with this idea ya kudhani A/H matters that much in marking or usage of Capital letters in where you think it ought to be used,

Those are not the main points in academic markings, they don’t matter that much (may be 5%) of the work.
 
Somo la Kwanza
  1. Kibali ni nini?
Kibali ni ruhusa ya kufanya japo fulani,ambalo ili ulifanye ni lazima upate kibali au ruhusa kutoka mamlaka husika。Kibali cha kikuu cha kwanza kwa binadamu baada ya kuumbwa ni kibali cha uhai,kibali cha kuishi na kibali cha kuumba binadamu wengine。Baada ya hapo ni kibali cha kufanya kila kinachofanyika。Kibali kwa mwanamke kuwa mama na mwanaume kuwa baba,ni kupevuka,kibali cha kujenga familia ni kuoa,kibali cha kujenga nyumba ni kumiliki ardhi,kibali cha kufanya biashara ni kuwa na leseni,kibali cha kusafiri nje ni kuwa na passport,kibali cha kuingia nchi fulani ni kuwa na visa, hivyo vibali viko vya aina nyingi。

Kibali ninacho kizungumza kwenye uzi huu ni kibali cha kutawala nchi,kuwa mkuu wa nchi。
P
Kibali husika kwenye swala hili ni KURA, na kura halali tunaipataje? Ni kuwa na tume huru ya uchaguzi, na si vinginevyo.
 
Somo la Pili
2. Kibali ni cha kazi gani?

Kibali ni cha kutimiza lile jukumu la kibali ulichopewa,kama tulivyoona kwenye somo la kwanza, kuna vibali tofauti vya kufanya mambo tofauti tofaouti, ukipewa kibali cha ndoa,inatimiza majukumu ya ndoa,ukipewa kibali cha kufanya biashara,unafanya biashara kwa mujibu wa leseni yako。

Kuna vibali vingi,hadi vibali vya kuua,licence to kill,hata mtu anayehukumiwa kunyongwa,hukumu hiyo haitekelezwi hadi mkuu wa nchi asaini death warrant ndipo anyongwe

Hivyo hata kibali cha kutawala nchi,unatawala kwa mujibu wa kibali chako
japo kibali cha kutawala nchi kimetolewa kwa mujibu wa katiba,anayepewa kibali hicho anapewa na YEYE na anapaswa sio tuu kufuata katiba,bali pia kutimiza madhumuni ya YEYE alIyempa kibali hicho,alimdhamiria afanye nini,kibali chake ni cha nini na kwanini ni yeye na sio mtu mwingine yeyote?

Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
Kama nilivyoeleza, kibali kinatolewa kwa madhumuni kusudiwa, au kuna vibali vya kazi maalum, task force, ukiisha ikamilisha kazi, unakuwa rewarded accordingly, kibali kimekamilika na kazi ya kibali hicho inakuwa imekwisha.

Musa kibali chake kilikuwa ni kuwakomboa tuu wana wa Israel kutoka utumwani Misri, alipokamilisha kazi ya kuwaondoa na kuwasafirisha mpaka nchi ya ahadi, kibali chake kikakamika, yeye hakuingia nchi ya ahadi, alitwaliwa, na kibali cha kuwaingiza nchi ya ahadi, kikatolewa kwa mtu mwingine.

Kwa vile kibali, ni kibali cha kazi maalum kwa mtu maalum, ukiwa ni mtu mwenye kibali, usipokitumia kibali hicho kikamilifu, kibali hicho kinafutwa!.

Ufutaji wa vibali au ufutwaji wa vibali, hufanyika kwa namna mbili
1. Ufutwaji wa uwezo wako, kufutwa, mtu alikuwa mfanyabiashara mkubwa maarufu na tajiri, anafilisika hadi kubaki apeche alolo!. Mtu alikuwa msanii mzuri, mwanamuzi mzuri, mchezaji mzuri, ghafla uwezo wake unashuka, anajikuta anatupwa nje ya gemu.
2. Ufutwaji wa kibali wa aina ya pili ni kwa wewe kufutwa kwenye uso wa dunia, kwa kutwaliwa!, kama inavyotokea kwa wengi wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana. Musa, Kanumba, Sembuli, Mbaraka Mwishehe, Shaaban Robert, John F Kennedy, Bruce Lee, JPM na wengine wengi, wameitwa kurejea kwa Muumba wao.
P.
 
Somo la Pili
2. Kibali ni cha kazi gani?
Kibali ni cha kutimiza lile jukumu la kibali ulichopewa,kama tulivyoona kwenye somo la kwanza, kuna vibali tofauti vya kufanya mambo tofauti tofaouti, ukipewa kibali cha ndoa,inatimiza majukumu ya ndoa,ukipewa kibali cha kufanya biashara,unafanya biashara kwa mujibu wa leseni yako。

Kuna vibali vingi,hadi vibali vya kuua,licence to kill,hata mtu anayehukumiwa kunyongwa,hukumu hiyo haitekelezwi hadi mkuu wa nchi asaini death warrant ndipo anyongwe

Hivyo hata kibali cha kutawala nchi,unatawala kwa mujibu wa kibali chako
japo kibali cha kutawala nchi kimetolewa kwa mujibu wa katiba,anayepewa kibali hicho anapewa na YEYE na anapaswa sio tuu kufuata katiba,bali pia kutimiza madhumuni ya YEYE aluyempa kibali,alimtaka afanye nini,kibali chake ni cha nini na kwanini ni yeye na sio mtu mwingine yeyote?
P
Ufafanuzi who is YEYE ?!
GOD or something else ??!
 
Back
Top Bottom