Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Mkuu,

Siasa si hasa kilichomo moyoni na akilini!!!

Hekima kwa WATU kuhusu KIBALI hii hapa
Kutoka 11:3 “Bwana akawapa watu hao KIBALI MACHONI PA WAMISRI. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”
Hekima kwa WATAWALA kuhusu KIBALI hii hapa
Mwanzo 39:21 “Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, AKAMPA KIBALI machoni pa mkuu wa gereza.
22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya”
1Samweli 16:22 “Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana AMEONA KIBALI machoni pangu”.
1Samweli 27:5 “Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona KIBALI MACHONI PAKO na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?”
Esta 5:2 “Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye AKAPATA KIBALI machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo”
'VICARIOUS LIABILITY' kwa mtawala hataikwepa kwa vyovyote vile kutokana na matendo maovu ya wasaidizi wake akishuuhudia bila kuchukua hatua za kuwawajibisha. Aliyepo hana kibali Mungu amemkataa
 
Kabla hata sijamaliza kusoma naomba niseme yafuatayo:

1.Haikuwa mpango wa Mungu Rais Magufuli kufariki kabla ya kumaliza kipindi chake. Lakini kibali chake kilifutwa kutokana na makosa matatu makubwa:
a) Kubaka uchaguzi
b) Kuruhusu umwagikaji wa damu za watanzania
c) Kutumia Kanisa kama jukwaa la kisiasa na kukosoa uongozi wa Kanisa akiwa kanisani.
2. Mama Samiah amepewa nafasi ya kurekebisha yale ya Magufuli na kuleta Katiba mpya. Lakini inavyoonekana kaamua kupita njia ya Magufuli. Hivyo, anavuta yaliyompata Magufuli yampate pia.
 
Kabla hata sijamaliza kusoma naomba niseme yafuatayo:

1.Haikuwa mpango wa Mungu Rais Magufuli kufariki kabla ya kumaliza kipindi chake. Lakini kibali chake kilifutwa kutokana na makosa matatu makubwa:
Kwa vile mtoa vibali ni Mungu mwenyewe, anapotoa kibali fulani fulani kwa mtu fulani fulani, ama husema nae, ama husema direct, kwa wanaojaaliwa neema ya kuisikia sauti yake, ama husema nae, kupitia wengine, ama sometimes hasemi kabisa, hivyo no one can say for sure kibali cha JPM ni kibali cha nini!.

Pili Mungu ndie muumba, na ndie hutwaa, anapotwa, ni Mungu pekee hujua kwanini amemtwaa fulani, hakuna binadamu ana uwezo wa kujua for sure kwanini JPM alitwaliwa mapema,
a) Kubaka uchaguzi
b) Kuruhusu umwagikaji wa damu za watanzania
c) Kutumia Kanisa kama jukwaa la kisiasa na kukosoa uongozi wa Kanisa akiwa kanisani.
Hizi ni speculations tuu, nashauri tusihukumu ili tusije kuhukumiwa Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!, ila kwa sisi Wakristo, kwa vile tunaokolewa kwa neema, nimeelezwa neema ya wokovu ilimshukia JPM, Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
2. Mama Samiah amepewa nafasi ya kurekebisha yale ya Magufuli na kuleta Katiba mpya. Lakini inavyoonekana kaamua kupita njia ya Magufuli. Hivyo, anavuta yaliyompata Magufuli yampate pia.
Kwenye hili, nimeshauri nyie mliojaaliwa kukijua kibali cha JPM na kibali cha Samia, msaidieni kwanza kwa kumjulisha kibali chake ni cha nini, na cha muda gani, na mkimuona anakwenda kinyume cha kibali chake msaidieni kumrekebisha aenende kwenye mstari.
Mimi pia nasaidia saidia kwa kuwaekekeza wasaidizi wake wasaidie Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

P
 
KIFUTWE HARAKA!
 
Akiwaendekeza machawa kibali kitafutwa
Mkuu Benny Haraba , Machawa hawana tatizo kabisa!,, she is a human being, kazi ya machawa ni kumpeti peti tuu, mfano Dotto Magari hata mimi nampenda, wanamfurahisha mama, ana smile, raha ya mwanamke ni kufurahishwa, machawa hawana madhara kabisa, hatari ni wasaidizi wake wasiomsaidia, wasio mwambia ukweli, na wahafidhina wasiotaka mabadiliko!.
Naunga mkono hoja.
P.
 
Msomi wetu pasco
 
Mkuu Meya, Mayor Quimby ,naunga mkono hoja。

P
 
Changamoto ambayo nimeona kwenye jamii zetu za kiafrica ni kwamba wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri kizalendo, (kwa nafsi), a.k.a kujizima data kwa kutumia tabia ya unyumbu wa kisiasa ambapo wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri kwa nafsi kwababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani ama chama dola kwa masilahi binafsi au kwa kuigiza uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Ingekuwa vizuri kama ungejibu maswali yako ili kuwapa wachangiaji ufafanuzi, maana na maudhui ya ulichomaanisha.
Mkuu Baba wa Wote Father of All ,uliharakisha tuu ,
Je rais ni kabali cha nini?
limejibiwa。
Ni kibali cha ufisadi, uongozi bora, ufamilia, bora uongozi, uadilifu, mamlaka nk?
limejibiwa。
Je ni kibali kilichomo kwenye katiba au cha kujitengenezea?
limejibiwa。
Je kibali hiki kinatumika wapi na kwa muda gani?
limejibiwa。
Je nani anatoa hiki kibali na kwa sifa zipi?
limejibiwa。
Je kama rais ni kibali na kibali ni rais au ni nini?
Rais ni kibali,maana yake Mungu ndie huweka serikali za mataifa,na kutoa kibali cha mtu kuwa kiongozi wa nchi,hivyo viongozi wote ni vibali,lakini vibali ni kutoka kwa Mungu!。
Je sifa za kibali ni zipi na kwa vigezo vipi?
limejibiwa。
Naona nisiteke uzi wako mwanangu, ila kuna mengi yanapwaya kama siyo. kukosekana kabisa.
Mengi ya maswali yako yamejibiwa,kama una mengine uliza,nitakujibu
p。
 
hili tumelizungumza humu Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
p
 
Jiwe hakuwa na kibali,
Mkuu Ngongo ,JPM alikuwa na kibali,cha ile awamu ya kwanza, aligombea na watu 62,hivyo kitendo tuu cha yeye kupita ni kibali tosha!。 Angalia tarehe ya bandiko hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Kwavile kibali kina muda, inawezekana kibali chake ni cha awamu moja,hivyo ile awamu ya pili akaonekana kana ame force,hivyo awamu ya kwanza ilipoisha,kibali chake kikaisha muda wake na ku expire。Ndio maana kwa 2025 tukashauri Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! hapa tunamaanisha 2025 tunakwenda na Mama but only if kama ana kibali!。
kama angekuwa na kibali ni kwanini aliiba uchaguzi.
Hakuna uthibitisho wowote kuwa aliiba uchaguzi,ule ulikuwa ni udhalimu na niliutolea angalizo Elections 2015 - Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!
P
 
7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa kwa Kufutwa Akapewa Samia
Huku hayo yakijiri, wengine wanaandika hivi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…