Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Wanabodi,

Leo, naendelea na zile mada zangu fikirishi za KMT, Kwa Maslahi ya Taifa。Somo la leo ni la kitu kinachoitwa “Kibali”。
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike, naanza na Outline
  1. Kibali ni nini?
  2. Kibali ni cha kazi gani?
  3. Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
  4. Kibali Kinatolewa na nani?
  5. Kibali Kinatolewa kwa nani?
  6. Anyepewa Kibali Anajua Kuwa ana Kibali?.
  7. Utamjuaje Mtu Mwenye Kibali?
  8. Nyerere, Mwinyi na Mkapa, Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.
  9. JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Hakikukamilika, Kilifutwa.
  10. Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
  11. Tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu ili kisifutwe? au tumuachie mwenyewe?
  12. Hitimisho na A Way Foward 2025
1. Somo la Kwanza: Kibali ni nini?

2. Somo la Pili: Kibali ni cha kazi gani?

3. Somo la Tatu: Kibali Kinatolewa na Nani?

4. Somo la Nne: Kibali Kinatolewa kwa Nani?

5. Somo la Tano: Anyepewa Kibali Anajua Kuwa Ana Kibali?. Utamjuaje Mtu mwenye Kibali?.

Somo la Sita: Nyerere, Mwinyi na Mkapa, JK Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.

7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa kwa Kufutwa Akapewa Samia

8. Somo la Nane: Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?

Somo la Tisa: Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au Tumuachie Mwenyewe na Kibali Chake?

10 Somo la Kumi: Hitimisho na A Way Forward 2025
Kuhusu Kibali cha Kutawala Tanzania, Rais Samia ana kibali!.
Kwa vile kibali Rais Samia alichoingia nacho hii 2021-2025 ni kibali cha JPM alichonyanganywa akapewa Samia ili kuimalizia ngwe ya Magufuli, sijui kama mtoa vibali anaujua ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ndio maana licha ya JPM kuingia kumalizia kipindi chake cha pili kwa mserereko, Mtoa vibali alikifuta kibali cha JPM. Japo lengo la msesereko ni jambo zuri na lengo zuri la kuondoa duplicity kwenye mchakato wa usaili wa ushindani wa wagombea urais ambao walisailiwa ili kumpata the best, Rais Samia yeye hakusailiwa urais kwa ushindani, kwa vile ameupata urais kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu, ni kibali kimemuepushia na ushindani, hivyo 2025 ndiye mgombea wa CCM wa mserereko wa kubembea.

Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukamuulizia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia 2025-2030, then ni mimi ndiye niliye ambiwa kitu kuhusu HII issue ya 2025, wakati muafaka ukiwadia, na yeye mwenyewe ataambiwa na mtoa vibali.

Mungu Ibariki Tanzania.

Asanteni sana!.

Paskali
Kwani wewe ndio unatoa na kukagua vibali vya mtu kuwa Rais?

Usijipe kazi ambayo hujatumwa Wala hujaomba kumsaidia mtoa kibali.
 
Samia ni rais pekee katika marais waliiongoza nchi ambaye hapendwi na anaowatawala na hana ushawishi wowote.. tazama hata hotuba zake utafikiri anahutubia mwenyekiti wa kitongoji.. miaka michache iliyopita kuna kiongozi aliteka hadhira ya watanzania na kila ilipofika jioni watu walijazana kwenye tivii kusikiliza hotuba zake.
Magufuli alifanikiwa kuua uhuru wa vyombo vya habari, na akawa mzuri kwenye propaganda na kudhalilisha watu. Akateka ufahamu wa masikini wengi, hivyo alipendwa na wajinga wengi. Ndio maana ilipofika wakati wa uchaguzi ilibidi apore uchaguzi maana hakuwa na uhakika wa kukubalika kwake. Na angelogwa aheshimu uchaguzi angekutana na matokeo ya kuumiza moyo wake.
 
Hawa waliopiga kura online poll walikuwa wapumbavu km ww ?
 
Attachments

  • 20240430_093958.jpg
    20240430_093958.jpg
    81.3 KB · Views: 2
  • 20240430_093319.jpg
    20240430_093319.jpg
    41.1 KB · Views: 3
Kwani wewe ndio unatoa na kukagua vibali vya mtu kuwa Rais?
Mkuu Sunki,@the sunk cost fallacy 2,mimi ni muelimishaji umma,kuelimisha wengine kile ninachokijua ili kuwasaidia na wao wakijue。
Usijipe kazi ambayo hujatumwa Wala hujaomba kumsaidia mtoa kibali.
Mimi sio mtu wa kutumwa bali kujituma,na kujitolea,lengo sio kumsaidia mtoa kibali bali mpewa kibali!。

Kabla ya bandiko hili,wewe ulijua kuhusu kibali?。
P
 
Wanabodi,

Leo, naendelea na zile mada zangu fikirishi za KMT, Kwa Maslahi ya Taifa。Somo la leo ni la kitu kinachoitwa “Kibali”。
Kufuatia Watanzania waliowengi hawapendi kusoma vitu virefu,mada hii naileta kwa vipande vipande hadi ikamilike, naanza na Outline
  1. Kibali ni nini?
  2. Kibali ni cha kazi gani?
  3. Sifa za Kibali: Kikitumika Kinakamilika, Kisipotumika, Kinafutwa!
  4. Kibali Kinatolewa na nani?
  5. Kibali Kinatolewa kwa nani?
  6. Anyepewa Kibali Anajua Kuwa ana Kibali?.
  7. Utamjuaje Mtu Mwenye Kibali?
  8. Nyerere, Mwinyi na Mkapa, Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.
  9. JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Hakikukamilika, Kilifutwa.
  10. Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?
  11. Tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu ili kisifutwe? au tumuachie mwenyewe?
  12. Hitimisho na A Way Foward 2025
1. Somo la Kwanza: Kibali ni nini?

2. Somo la Pili: Kibali ni cha kazi gani?

3. Somo la Tatu: Kibali Kinatolewa na Nani?

4. Somo la Nne: Kibali Kinatolewa kwa Nani?

5. Somo la Tano: Anyepewa Kibali Anajua Kuwa Ana Kibali?. Utamjuaje Mtu mwenye Kibali?.

Somo la Sita: Nyerere, Mwinyi na Mkapa, JK Walikuwa na Vibali, Vikatumika na Kukamilika.

7. Somo la Saba: JPM alikuwa na kibali, Japo Kilitumika, Kilikatishwa kwa Kufutwa Akapewa Samia

8. Somo la Nane: Je Rais Samia ni Kibali?, Je Anajitambua kuwa yeye ni kibali?Anakitumia Kibali chake Ipasavyo?

Somo la Tisa: Tumsaidie ili atimize matakwa ya kibali chake kikamilifu au Tumuachie Mwenyewe na Kibali Chake?

10 Somo la Kumi: Hitimisho na A Way Forward 2025

Kuhusu Kibali cha Kutawala Tanzania, Rais Samia ana kibali!.
Kwa vile kibali Rais Samia alichoingia nacho hii 2021-2025 ni kibali cha JPM alichonyanganywa akapewa Samia ili kuimalizia ngwe ya Magufuli, sijui kama mtoa vibali anaujua ule utaratibu wa mserereko wa CCM, ndio maana licha ya JPM kuingia kumalizia kipindi chake cha pili kwa mserereko, Mtoa vibali alikifuta kibali cha JPM. Japo lengo la msesereko ni jambo zuri na lengo zuri la kuondoa duplicity kwenye mchakato wa usaili wa ushindani wa wagombea urais ambao walisailiwa ili kumpata the best, Rais Samia yeye hakusailiwa urais kwa ushindani, kwa vile ameupata urais kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu, ni kibali kimemuepushia na ushindani, hivyo 2025 ndiye mgombea wa CCM wa mserereko wa kubembea.

Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukamuulizia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia 2025-2030, then ni mimi ndiye niliye ambiwa kitu kuhusu HII issue ya 2025, wakati muafaka ukiwadia, na yeye mwenyewe ataambiwa na mtoa vibali.

Mungu Ibariki Tanzania.

Asanteni sana!.

Paskali
Nani alitoa kibali cha ujenzi wa ghorofa la kariakoo hadi likaua watu vile??????
 
CCM huwa hawashindi uchaguzi, kwa maana nyingine HAWACHAGULIWI hujiweka kwa NGUVU. Hayo ya vibali mnajua nyie mi sioni kama anakibali chochote, HAKUCHAGULIWA kaingia kwa mlango wa nyuma. Unasemaje anakibali, anakitoa wapi?

Ungesema anatafuta hicho kibali, 2025 akipate, ningekuelewa.
 
CCM huwa hawashindi uchaguzi, kwa maana nyingine HAWACHAGULIWI hujiweka kwa NGUVU.
Mkuu Nanye,@nanye go,sii kweli,CCM inachaguliwa na Watanzania,ila kishindo chake cha ushindi wa asilimia 99% ni ushindi wa advantage,ya chama dola kinashindana na vyama makapuku,matokeo ni CCM hana mshindani,ni CCM only and only CCM!。
Hayo ya vibali mnajua nyie mi sioni kama anakibali chochote,
Ana kibali!,kitendo tuu cha mtu kuchomoka,kisha unakuwa wewe,hicho ni kibali tosha!
HAKUCHAGULIWA kaingia kwa mlango wa nyuma.
Sio kweli,Samia alichaguliwa na Watanzania wote as a set,Urais wa Tanzania,hauchagui mtu mmoja tuu rais, unachagua a set ya urais yenye watu wawili,kila kura iliyomchagua JPM, pia ilimchagua Samia, hivyo hakuingia kwa mlango wa nyuma,ameingia kwa kudra tuu ya Mwenyeenzi Mungu hiyo kudra ndicho kibali chenyewe!hivyo sii kweli ameingia kwa mlango wa nyuma,ila likitokea la kutokea kabla ya 2025,kisha VP wa sasa akaukwaa,hapo ndio VP, atakuwa ameingia kwa mlango wa nyuma。
Unasemaje anakibali, anakitoa wapi?
Kitendo tuu cha yeye kuwa ni kibali tosha ambacho amekipata kwa kudra ya mtoa vibali!。
Ungesema anatafuta hicho kibali, 2025 akipate, ningekuelewa.
Nimesema kibali kina timeframe,duration,kwa mujibu wa katiba yetu,kibali cha katiba ni full two terms za 10 years,mtoa vibali alitoa full terms kwa Mwinyi,Mkapa na JK,lakini kwa JPM,ni ama alitoa kibali cha a single term ya kipindi kimoja,hivyo JPM alipomaliza term ya kwanza ,kibali chake kikaisha,kika expire, hivyo 2nd term aliforce, ndio ikawa vile!。

Ama kibali cha JPM,pia kilikuwa ni cha full term,lakini kuna mambo JPM aliyafanya sio,hivyo mtoa vibali akakasirika aka revoke kibali cha JPM,kwa kuki withdraw kwa kukifuta,ndio ikawa vile!。

Hakuna binadamu ajuaye kibali cha mtu mwingine isipokuwa mtoa vibali,wala hakuna binadamu ajuaye sababu za mtoa kibali kuvuta kibali cha JPM,hivyo ili kumsaidia huyu aliyepo ,asije kufanya makosa ya kupelekea kibali chake kufutwa,ndio kama hivi tunaendesha elimu ya vibali humu kwa ushauri wa kumuepusha na vitendo vinavyoweza kupelekea kibali chake kufutwa Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karmah Aliposema hajawahi kuua, tukapiga darasa humu Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Kuhusu kibali chake kwa 2025
Kwenye mahojiano na Kikeke, aliposema 2025, twende na mwanamke, tumemuunga mkono ila tukazumzia kuhusu kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Sasa sijui kama kwa vile ni mimi ndie niliulizia kuhusu kibali cha Rais Samia kwa 2025-2030, then ni mimi ndiye niliye ambiwa HII kitu kuhusu 2025, wakati muafaka ukiwadia, na yeye mhusika mwenyewe ataambiwa!。

Hahaha, wewe falsafa zako zimepindapinda, Kama kibali ni uhai, basi anacho. Kuishi ni fursa woote tumepewa mara moja, na woote tutakufa mara moja. Hivyo vitu viwili wote tuliopo tuna/tuta sare.

Nilidhani Kibali ni RIDHAA ya wananchi, ano WATAWALA. Hiyo HANA bado na kataa, kwasababu hta biblia inakataa, ndiyo maana hata mume namke siyo kitu kimoja linapokuja swala la ufalme wa mbingu. Biblia inasema hata kama mmelala kitanda kimoja wewe na mwenzako/Shemeji yetu, linapokuja swala la hukumu kila mmoja atahukumiwa kivyake na siyo as a set.

Dhambi za JPM hapaswi kupewa SSH, na za SSH hapaswi kupewa JPM, kila mtu ana zake, zile zilikuwa za JPM huyu naye alipaswa aandae makao yake, upya ili apande zake na achume zake, hii ni lift tu, siyo sawa ABIRIA kumiliki GARI la mtu aliye pata ajali na akafariki. Unaweza kulinunua lakini huwezi kulimiliki eti tu kwa sababu mwenye gari alipofariki ulikuwa naye.

Huyu Rais alipata free ride, lakini baada ya aliye mwenye dhamana kuondoka huyu alipaswa akae muda mfupi kuandaa Uchaguzi huru, HAPASWI KUKALIA KITI KWA MUDA MREFU, anapaswa Ashike ku ratibu UCHAGUZI mwingine yani transition government. Lakini yeye na wenzake wakaona ni FURSA sasa, KACHUKUA kama vile ni CHAKE.

Hapaswi kusaidiwa atafute chake kwa nguvu zake mwenyewe.
 
Hahaha, wewe falsafa zako zimepindapinda,
Mkuu Nanye,@nanye go,japo sikubaliani na hoja zako,lakini niko very impressed na uwezo wako wa kujenga hoja。
Kama kibali ni uhai, basi anacho. Kuishi ni fursa woote tumepewa mara moja, na woote tutakufa mara moja. Hivyo vitu viwili wote tuliopo tuna/tuta sare.
true
Nilidhani Kibali ni RIDHAA ya wananchi, ano WATAWALA. Hiyo HANA bado na kataa,
Kataa tuu,lakini nimefundisha kuna vibali vya aina mbili,kibali cha juu kwake YEYE
na cha chini cha dunia hii。 Kibali cha kwanza ni kibali cha juu,kibali chake
YEYE,ukiisha pata kibali chake,machoni pake,ni kibali hicho kinakufungulia kibali cha chini cha katiba,kupigiwa kura kuchaguliwa,na kushinda kwenye uchaguzi kwa ridhaa ya wananchi。
kwasababu hta biblia inakataa, ndiyo maana hata mume namke siyo kitu kimoja linapokuja swala la ufalme wa mbingu.
Ni kweli kwenye ufalme wa Mbingu,ni kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe。Hata kibali,kila mtu ana kibali chake。
Biblia inasema hata kama mmelala kitanda kimoja wewe na mwenzako/Shemeji yetu, linapokuja swala la hukumu kila mmoja atahukumiwa kivyake na siyo as a set.
This is true kwa hukumu tuu,lakini mkiisha uganishwa na mwenza wako,mnakuwa mwili mmoja,mume au mke akipata kibali mmoja wenu ni wote mmepata ila mwenye mamlaka ya kukitumia ni mmoja tuu,wewe uliyepewa!。
Dhambi za JPM hapaswi kupewa SSH, na za SSH hapaswi kupewa JPM, kila mtu ana zake,
Hii ni kweli na niliisha endesha somo hili humu kuwa Rais Samia asihukumiwe kwa makosa ya mtangulizi wake。
zile zilikuwa za JPM huyu naye alipaswa aandae makao yake, upya ili apande zake na achume zake,
Naunga mkono hoja,hata akina sisi hilo tulishauri
hii ni lift tu, siyo sawa ABIRIA kumiliki GARI la mtu aliye pata ajali na akafariki. Unaweza kulinunua lakini huwezi kulimiliki eti tu kwa sababu mwenye gari alipofariki ulikuwa naye.
naunga mkono hoja
Huyu Rais alipata free ride, lakini baada ya aliye mwenye dhamana kuondoka huyu alipaswa akae muda mfupi kuandaa Uchaguzi huru, HAPASWI KUKALIA KITI KWA MUDA MREFU, anapaswa Ashike ku ratibu UCHAGUZI mwingine yani transition government.
Naunga mkono hoja,and this is how it should have been,tumeingia vyama vingi kwa katiba ya chama kimoja!
Lakini yeye na wenzake wakaona ni FURSA sasa, KACHUKUA kama vile ni CHAKE.
No sii yeye bali hivyo ndivyo katiba yetu ilivyo elekeza。 Fursa ni 2025 - 2030,ambapo mimi nimemuunga mkono kama amepewa kibali Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Hapaswi kusaidiwa atafute chake kwa nguvu zake mwenyewe.
No way,Tanzania sio nchi ya mtu mmoja au ya chama kimoja,Tanzania ni ya Watanzania wote,hivyo we all have a duty of good citizenship kuisaidia nchi yetu na watu wake wakiwemo viongozi wetu。
P
 
Mimi namshauri hiyo 2025 asigombee. Maana kwa hali ilivyo mpaka sasa, sioni kama ana hicho kibali.
Mkuu shemeji Tate, Tate Mkuu ,kwanza naheshimu maoni yako,kibali cha 2025 kinatolewa 2025,kwa vile kinatolewa na YEYE, kikitolewa utakiona kwa matokeo。

Mtu akishakuwa na kibali,hata kama unamuona hana uwezo,anapata uwezo,hivyo usiwe na shaka,mimi kwa upande wangu,mambo ya 2015,niliisha elezwa kwenye HII kitu,
P
 
Kibali kimeshafutwa
Mkuu Mlibe,@mliberali,kibali kipo,kikifutwa mtu anafutika。
huwezi apa kwa Mungu kuilinda katiba alafu baada ya muda mfupi ukaanza pelekeshwa na madalali wa mafisadi ili kulinda maslahi yao tu. Badala ya nchi
Kiukweli this is weakness,kibali kilichopo ni cha mpaka 2025,kuhisu 2025~2030 nimeelezwa HII kitu。
P
 
Paschal, kuwa mkweli tu usizunguke , Bi mkubwa nchi imemshindwa na imekamatwa na wahuni haiwezekani kwa Kiongozi Makini , raia wanalalamika UTEKAJI, mauaji ,uchumi kuanguka n.k yeye hajali , na akitoka kuzungumza anaharibu kabisa , kiufupi hana uwezo wa kutuvusha , Wananchi kwa Sasa hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao bali Dola ndio inachagua , Je hapo Kuna nchi? Hapo Kuna Rais ?

Kibali kishafutwa unasubiriwa utekelezaji tu

Kiufupi nchi kwa Sasa inajiendea tu
 
Back
Top Bottom