Magufuli aliniongezea 70,000/= Kwa kupunguza paye, Samia kaniongeza 20,000/= Kwa asilimia 23.3%

Makelele hayaishi kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake

Hizo ni hoja tu kutafutia sababu. Ila mtaani vibaka wameongezeka na maisha ni magumu. Havihusiani hayo.
 
Nimepata nyongeza kubwa ya mshahara wakati wa Magufuli kuliko wakati wa Samia japo wakati wa Samia asilimia ni kubwa.

Sina mengi ya kuongeza lakini naendelea kumshukuru Hayati DR.John Pombe Magufuli , Mungu amlaze mahali pema, tutakukumbuka daima
Mimi nliongezewa mshahara wangu kwa maramoja enzi za mwenda zake nlikuwa nakula 900k ghafla ikapanda hadi 1.8m. Namshukuru sana huyu mzee ndo maanannampenda sana
 
Hakika, watumishi ebu tuwe na shukrani na kidogo tulichopewa mara nyingi annual increments sio pesa ya maana naya kuitegemea, pia inategemea uwezo wa nchi kiuchumi kwa wakati huo, cha muhimu na cha kukipigania ni Upandishwaji wa Madaraja ambao ni haki ya kila mtumishi kila baada ya miaka 3 au 4 ambacho mama amekifanya soon baada ya kuingia madarakani, wengine walionyimwa fursa hii zaidi ya mara moja kipindi kilichopita wamepewa mpk Upandishwaji wa mseleleko! Tukienda mbali zaidi mama amefuta Ile 6% ya retention fees kwa wanifaika wa Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu iliyowekwa kinyume na mkataba uliyoingiwa baina ya Bodi na wanafunzi kabla, hii ilikuwa mwiba na unyonyaji mkubwa kwa wanufaika walioanza kukatwa, kwa mfano deni linalozidi labda 45 million Makato yake kwa mwaka hayazidi au yanalingana na hiyo 6% ya retention fees hii ilifanya mnufaika kuendelea kudaiwa bila kupunguza deni ingawa anakatwa 18% ya mshahara wake ghafi kila mwezi! Tuna haja ya kumshukuru Mama kwa haya aliyoyafanya ndani ya Mwaka 1 tu, tuendelee kumuombea na nina Imani atatufanyia mazuri uko mbeleni.
 
Wenzako wana nyongeza ya chini ya 13,000.
 
Mimi namshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kuniondolea Tshs. Milioni 7 ya VRF kupitia HESLB.

#Tushukuru kwa kila jambo#
Hauko peke yako Mkuu mimi ilifikia wakati sijisumbui kusoma balance ya deni kwenye salary slip maana halipungui, (hii ni kwa wenzangu na mie tuliosoma course zenye gharama na waliosoma nje ya nchi)sasa juzi from no where wakati nakagua hiyo increment nakuta figure ya kushangaza ambayo hata nikijikakamua ndani 2years naweza kulilipa! Kwa mtindo uliobuniwa na awamu iliyopita deni langu na wengine kama mimi lilikuwa la kustaafu nalo halafu linakatwa kwenye stahiki za kustaafu.Nakumbuka kuna watu wengi kwenye kada yetu waliopanga kuacha kazi kwa sababu hiyo.
 
Yaani natamani kulia nikimbuka JPM na mazuri aliyokuwa anawafanyaia Watanzania na Tanzania. Sasa nchi ipo kwa wanyang'anyi maana hata kidogo tulichonacho wanatunyang'anya eti TOZO!!
 
Bora na wewe mtoa mada umeongewa hiyo 20.

Wengine hatuja ongezewa hata sumni.

Mama anaupiga mwingi sana. Mitano tena.
Na namhakikishia nitampigia kura aendee kuongoza
 
Wewe una furahi mkulima analia watu tuliacha kulima mahindi tumepanda parachichi ndio inalipa mahindi hayakuwa na soko kipindi cha magu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…