Magufuli aliniongezea 70,000/= Kwa kupunguza paye, Samia kaniongeza 20,000/= Kwa asilimia 23.3%

Magufuli aliniongezea 70,000/= Kwa kupunguza paye, Samia kaniongeza 20,000/= Kwa asilimia 23.3%

Nimepata nyongeza kubwa ya mshahara wakati wa Magufuli kuliko wakati wa Samia japo wakati wa Samia asilimia ni kubwa.

Sina mengi ya kuongeza lakini naendelea kumshukuru Hayati DR.John Pombe Magufuli , Mungu amlaze mahali pema, tutakukumbuka daima
Mimi nliongezewa mshahara wangu kwa maramoja enzi za mwenda zake nlikuwa nakula 900k ghafla ikapanda hadi 1.8m. Namshukuru sana huyu mzee ndo maanannampenda sana
 
Mkuu kwanza tambua kuwa Mimi sio chawa, pili Mimi sio mnafiki ukweli lazima usemwe kuwa mama anaupiga mwingi, kaingia madarakani ndani ya miezi mitatu nikapanda daraja ambalo lilikuwa na ongezeko la kiasi Cha shilingi 170,000,kamaliza mwaka kaniongezea kiasi Cha sh 55,000 Sasa bado Ni kae
Nalia Lia?,mama anajitahidi kwa kiasi chake.

Tutamuelewa mama tukiacha kumlinganisha na watu wengine,na pia pale tutakapo tambua kuwa mama ndiye rais wetu na hakuna mwingine na tuko naye Hadi mwaka 2030.


Mitano tena kwa mama samia
Hakika, watumishi ebu tuwe na shukrani na kidogo tulichopewa mara nyingi annual increments sio pesa ya maana naya kuitegemea, pia inategemea uwezo wa nchi kiuchumi kwa wakati huo, cha muhimu na cha kukipigania ni Upandishwaji wa Madaraja ambao ni haki ya kila mtumishi kila baada ya miaka 3 au 4 ambacho mama amekifanya soon baada ya kuingia madarakani, wengine walionyimwa fursa hii zaidi ya mara moja kipindi kilichopita wamepewa mpk Upandishwaji wa mseleleko! Tukienda mbali zaidi mama amefuta Ile 6% ya retention fees kwa wanifaika wa Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu iliyowekwa kinyume na mkataba uliyoingiwa baina ya Bodi na wanafunzi kabla, hii ilikuwa mwiba na unyonyaji mkubwa kwa wanufaika walioanza kukatwa, kwa mfano deni linalozidi labda 45 million Makato yake kwa mwaka hayazidi au yanalingana na hiyo 6% ya retention fees hii ilifanya mnufaika kuendelea kudaiwa bila kupunguza deni ingawa anakatwa 18% ya mshahara wake ghafi kila mwezi! Tuna haja ya kumshukuru Mama kwa haya aliyoyafanya ndani ya Mwaka 1 tu, tuendelee kumuombea na nina Imani atatufanyia mazuri uko mbeleni.
 
Hayati Magufuli alikuwa ana nia njema na Taifa hili, ila wahuni wachache hasa waliokuwa karibu nae wakamzunguka wakamtoa kafara..

Kwa jinsi gharama ya maisha ilivyopanda, sikutegemea huyu mama aongeze elfu 20 tu..

Hakika Magufuli ataendelea kukumbukwa na watu wenye akili njema..
Wenzako wana nyongeza ya chini ya 13,000.
 
Mimi namshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kuniondolea Tshs. Milioni 7 ya VRF kupitia HESLB.

#Tushukuru kwa kila jambo#
Hauko peke yako Mkuu mimi ilifikia wakati sijisumbui kusoma balance ya deni kwenye salary slip maana halipungui, (hii ni kwa wenzangu na mie tuliosoma course zenye gharama na waliosoma nje ya nchi)sasa juzi from no where wakati nakagua hiyo increment nakuta figure ya kushangaza ambayo hata nikijikakamua ndani 2years naweza kulilipa! Kwa mtindo uliobuniwa na awamu iliyopita deni langu na wengine kama mimi lilikuwa la kustaafu nalo halafu linakatwa kwenye stahiki za kustaafu.Nakumbuka kuna watu wengi kwenye kada yetu waliopanga kuacha kazi kwa sababu hiyo.
 
Hayati Magufuli alikuwa ana nia njema na Taifa hili, ila wahuni wachache hasa waliokuwa karibu nae wakamzunguka wakamtoa kafara..

Kwa jinsi gharama ya maisha ilivyopanda, sikutegemea huyu mama aongeze elfu 20 tu..

Hakika Magufuli ataendelea kukumbukwa na watu wenye akili njema..
Yaani natamani kulia nikimbuka JPM na mazuri aliyokuwa anawafanyaia Watanzania na Tanzania. Sasa nchi ipo kwa wanyang'anyi maana hata kidogo tulichonacho wanatunyang'anya eti TOZO!!
 
Bora na wewe mtoa mada umeongewa hiyo 20.

Wengine hatuja ongezewa hata sumni.

Mama anaupiga mwingi sana. Mitano tena.
Na namhakikishia nitampigia kura aendee kuongoza
 
Yule jamaa alinfurahisha kwa namna alivyojuw kulinda vitu, hasa vyakula na mahitaji mengine madogomadogo ambayo kimsingi ndio hugusa wengi (Ngoja nitumie mchele kama mfano).

Kitendo cha Mchele kuganda bei ya 1000-1200 kwa miaka miwili (2020-2021) bila kujali wakati wa mavuno au laah kilinifanya nimkubali sana kwenye food security, kibembe alipoingia tu huyu bibi ndani ya miezi 6 ukafikia 2000/= hapo ndo nilipoanza kushtuka kuwa tunakoelekea ni kubaya.


Ukitaka kutawala vizuri bila kelele hata kama ni mwizi basi hakikisha hauwabinyi watu watu kwenye mahitaji yao ya kila siku (hasa vyakula na viambata vyake) kwasababu hapo ndipo unapogusa hisia za wengi kwa wakati mmoja.

Utakuta mtu analipwa 500000Tsh, ila mtu huyohuyo akiwa na 10000 mkononi bado haitoshi hata kwa mahitaji ya siku moja, emagine ukinunua mchele 2Kg kwenye 5000 unabakiwa na 1000 ambayo haitoshi hata kununua mafuta nusu fanta, haya 10K imeisha hivyo[emoji23].

Sasahivi ni wakati wa mavuno ila gunia la mahindi utalinunu kwa 120k-130k, ikifika december au january tutalinunua kwa 200K, mafuta 5Ltrs 40K, daah[emoji23]. Halafu mtu anakuja kutetea eti mfumuko wa bei ni dunia nzima, nimetoka ZAMBIA mwezi uliopita wanaisha life zuri sana, hata Uganda tu hapa hakuna huo mfumuko wa kijinga kweye vyakula.


Haya maisha utayaona mazuri ukiwa mfanyaniashara (ingawa sera nazo ni mbaya), ila kwa watumishi wa umma mtavaa mno suruali moja kwa miezi[emoji23].
Wewe una furahi mkulima analia watu tuliacha kulima mahindi tumepanda parachichi ndio inalipa mahindi hayakuwa na soko kipindi cha magu
 
Back
Top Bottom