Magufuli aliniongezea 70,000/= Kwa kupunguza paye, Samia kaniongeza 20,000/= Kwa asilimia 23.3%

Magufuli aliniongezea 70,000/= Kwa kupunguza paye, Samia kaniongeza 20,000/= Kwa asilimia 23.3%

Nimepata nyongeza kubwa ya mshahara wakati wa Magufuli kuliko wakati wa Samia japo wakati wa Samia asilimia ni kubwa.

Sina mengi ya kuongeza lakini naendelea kumshukuru Hayati DR.John Pombe Magufuli , Mungu amlaze mahali pema, tutakukumbuka daima
Upuuzi mtupu timu MATAGA
 
Umeongezewa ngapi kwa kupanda madaraja mwaka jana kisha jumlosha na hiyo asilimia.Majibu tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza tambua kuwa Mimi sio chawa, pili Mimi sio mnafiki ukweli lazima usemwe kuwa mama anaupiga mwingi, kaingia madarakani ndani ya miezi mitatu nikapanda daraja ambalo lilikuwa na ongezeko la kiasi Cha shilingi 170,000,kamaliza mwaka kaniongezea kiasi Cha sh 55,000 Sasa bado Ni kae
Nalia Lia?,mama anajitahidi kwa kiasi chake.

Tutamuelewa mama tukiacha kumlinganisha na watu wengine,na pia pale tutakapo tambua kuwa mama ndiye rais wetu na hakuna mwingine na tuko naye Hadi mwaka 2030.

Mitano tena kwa mama samia
Kwa mazingira cheo hiko umeona kama offer, na nyongeza ya 55K imekupumbaza kabisa yani
 
Yule jamaa alinfurahisha kwa namna alivyojuw kulinda vitu, hasa vyakula na mahitaji mengine madogomadogo ambayo kimsingi ndio hugusa wengi (Ngoja nitumie mchele kama mfano).

Kitendo cha Mchele kuganda bei ya 1000-1200 kwa miaka miwili (2020-2021) bila kujali wakati wa mavuno au laah kilinifanya nimkubali sana kwenye food security, kibembe alipoingia tu huyu bibi ndani ya miezi 6 ukafikia 2000/= hapo ndo nilipoanza kushtuka kuwa tunakoelekea ni kubaya.

Ukitaka kutawala vizuri bila kelele hata kama ni mwizi basi hakikisha hauwabinyi watu watu kwenye mahitaji yao ya kila siku (hasa vyakula na viambata vyake) kwasababu hapo ndipo unapogusa hisia za wengi kwa wakati mmoja.

Utakuta mtu analipwa 500000Tsh, ila mtu huyohuyo akiwa na 10000 mkononi bado haitoshi hata kwa mahitaji ya siku moja, emagine ukinunua mchele 2Kg kwenye 5000 unabakiwa na 1000 ambayo haitoshi hata kununua mafuta nusu fanta, haya 10K imeisha hivyo[emoji23].

Sasahivi ni wakati wa mavuno ila gunia la mahindi utalinunu kwa 120k-130k, ikifika december au january tutalinunua kwa 200K, mafuta 5Ltrs 40K, daah[emoji23]. Halafu mtu anakuja kutetea eti mfumuko wa bei ni dunia nzima, nimetoka ZAMBIA mwezi uliopita wanaisha life zuri sana, hata Uganda tu hapa hakuna huo mfumuko wa kijinga kweye vyakula.

Haya maisha utayaona mazuri ukiwa mfanyaniashara (ingawa sera nazo ni mbaya), ila kwa watumishi wa umma mtavaa mno suruali moja kwa miezi[emoji23].
Wakati huo mkulima kilo 1 ya mchele aliuza 600 na 700 na wakati huo kalima heka 1 kwa 800000.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha wewe huwa huwezi kujadili bila hamaki, na kila siku ukiniquote huwa na kwambia kinachokusumbua ni umasikini wako ndiomaana upi kila sehemu kutetea upuuzi wa huyo bibi yako SHH.

NB;Wanaoumia ni mama zenu huko vijijini (hasa wenye watoto masikini na mafukara kama wewe), usiniulize nimejuaje kuwa wewe ni masikini.
Maskini kama wewe ndio kutwa kulalama kama chura msimu wa mvua..

Na bado mama atazidi kukaza na cha kumfanya huna..

Narudia tena kukwambia kama ulitegemea kufaidika na jasho la mkulima imekukata,jipange ukalime Ili uje uuze Mazao Kwa bei ya chini..

Endelea kujifariji kwa kujichekesha huku ukiugulia ndani Kwa ndani
 
Rais anatakiwa afanye Mambo bila kujari watu watasema Nini , na kamwe hawezi kuwafurahisha wote, na binadamu ni kiumbe mtata sana Ni ngumu kujua Ni Nini anataka.

Mama kaingia madarakani watumishi wengi ikiwemo Mimi tulipanda madaraja kwa fujo, hajakaa sawa kaweka annual increment lakini bado watu wanalalama, sasa afanye lipi tumuelewe.?

Mitano tena kwa #mama samia
Walalamikaji ni kundi fulani la wachache waliokula sana bata awamu ya tano. Siku hazigandi.
 
Attachments

  • 20220216_225742.jpg
    20220216_225742.jpg
    20.8 KB · Views: 6
Rais anatakiwa afanye Mambo bila kujari watu watasema Nini , na kamwe hawezi kuwafurahisha wote, na binadamu ni kiumbe mtata sana Ni ngumu kujua Ni Nini anataka.

Mama kaingia madarakani watumishi wengi ikiwemo Mimi tulipanda madaraja kwa fujo, hajakaa sawa kaweka annual increment lakini bado watu wanalalama, sasa afanye lipi tumuelewe.?

Mitano tena kwa #mama samia
Chawa!
 
20220723_145441.jpg

Nipo naikula hii 20 niliyopewa na SSH.Me vyovyote tu itakavyokuwa poa tu.

"Maisha hayana maana " E .Kezilahabi
 
Walizaliwa, tukazaliwa na wanazaliwa mwisho wa yote sote tutakufa na tutasahau yote '

Ndivyo awazavyo mwanasiasa.

Politics is an art or science of possible🤣🤣
 
Nimepata nyongeza kubwa ya mshahara wakati wa Magufuli kuliko wakati wa Samia japo wakati wa Samia asilimia ni kubwa.

Sina mengi ya kuongeza lakini naendelea kumshukuru Hayati DR.John Pombe Magufuli , Mungu amlaze mahali pema, tutakukumbuka daima
Hujui hata wanaposema kima cha chini hujui unaweweseka weweseka tu hapo.
Kamfufue uzikwe wewe
 
Nimepata nyongeza kubwa ya mshahara wakati wa Magufuli kuliko wakati wa Samia japo wakati wa Samia asilimia ni kubwa.

Sina mengi ya kuongeza lakini naendelea kumshukuru Hayati DR.John Pombe Magufuli , Mungu amlaze mahali pema, tutakukumbuka daima
Tshs 70,000 kwa miaka sita ?
 
Mkuu kwanza tambua kuwa Mimi sio chawa, pili Mimi sio mnafiki ukweli lazima usemwe kuwa mama anaupiga mwingi, kaingia madarakani ndani ya miezi mitatu nikapanda daraja ambalo lilikuwa na ongezeko la kiasi Cha shilingi 170,000,kamaliza mwaka kaniongezea kiasi Cha sh 55,000 Sasa bado Ni kae
Nalia Lia?,mama anajitahidi kwa kiasi chake.

Tutamuelewa mama tukiacha kumlinganisha na watu wengine,na pia pale tutakapo tambua kuwa mama ndiye rais wetu na hakuna mwingine na tuko naye Hadi mwaka 2030.

Mitano tena kwa mama samia

Wewe umepanda daraja, sisi wengine huku ambao tulinufaika na bei ndogo ya vitu tufanyaje? Wewe hilo daraja na bei kupanda kuna potential increase in your income?
 
Back
Top Bottom