Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Hapana jamani Mramba amezidi kiburi hakujali hata wakubwa wake.Inakuwaje anajiamulia maamuzi makubwa bila kutaka ushauri hata kwa Waziri? Anajiona bado yuko awamu ya NNE.Kheri ya mwaka mpya Mramba umetusumbua sana weeeee.
 
Kwa kweli huyu Dr.Mwinuka aliyeteuliwa anastahili cheo hicho,kwa wanaomfahamu huyu jamaa ni mchapakazi hatari mwenye hofu ya Mungu
Sasa hawa wahadhiri mbona wanaisha pale UDSM😵😵😵
 
Hii INA maana moja tu ktk nchi hii anae jua ni yeye tu! Wengine wote hawajui wanapaswa kumuuliza kwa kila kitu. Yeye ndie msaafu wa nini kifanyike
 
Magu, umebakiwa na kazi moja tu katika tumbua jipu...
Sasa ifuate zamu ya mkurugenzi mkuu wa DAWASCO.. Inahitajika damu mpya pale ili shirika liweze kusonga mbele...
Tanesco bado sana hichi ni kiharara tu kakiminya
 
Wivu na hasira zilizochanganyikana na umaskini hizi

wapate faida kwanza ndio wajipe umeme bure...

ila kupandisha mabei ovyo ndio source ya kutumbuliwa...

nitajie kampuni au shirika lolote duniani linalogawa huduma bure kipindi ambapo linapata hasara...

only in tanzania
 
Anaiachaje bodi ya Tanesco sasa?anaacha kuzuia mabillion yanayolipwa kwa IPTL kila leo kwa jasho la kodi yetu anaenda kumuondoa mramba?

Kuendesha nchi kwa ubaguz wa udini na ukabila hakuna mwisho mwema

..duh!

..tra alifukuza bodi akamuacha mkurugenzi mkuu.

..tanesco amefukuzwa mkurugenzi mkuu bodi ya wakurugenzi imeachwa.

..sasa tukisema nchi inaendeshwa kwa mihemko tutakuwa tumekosea?

..halafu anakwenda kuyazungumzia mambo haya
KANISANI!!
 
tatizo sio hizo unit 700 kwani hata zikipigwa panga kama hakuna mfumo mzuri bado shirika hasara...
 
Mkuu ongezea .....pia wana mishahara mikubwa plus marupurupu kibao na mianya ya rushwa ya nguvu
 
Kumekua na Wimbi la Kuteua Wahadhiri ambao hawajawahi hata kukaa Ofisini zaidi ya Kuzoea Ku deal na Coursework za wanafunzi

Shida mteuaji mwenyewe naye ni mshika chaki hivyo nadhani ana imani kubwa na washika chaki.
 
Kwa kweli huyu Dr.Mwinuka aliyeteuliwa anastahili cheo hicho,kwa wanaomfahamu huyu jamaa ni mchapakazi hatari mwenye hofu ya Mungu
"Mchapakazi hatari" una maanisha nini mkuu?
 
Mwinuka????? Dah haya bwana... Ila katoa fadhila kwa Wahaya ili kesho abwate weee na mambo mengine yaende!! Mwinuka ni mchanga mno na hajawahi kuwa mbunifu hata kidogo.! Hapana!! Mwinuka Tito hapana!!!!!
Sio kila postninahotaji ubunifu, huyo mrambi aliyekuwa mbunifu ni kili alichokifanya zaidi ya kuliingiza shirika katika madeni na kubuni watumiaji ndio walipe, kwa sasa tanesco waziri hisika anao utaalamu na uzoefu wala haitajiki mkurugenzi pale, mtu muhimu ni fundi wa service line endapo kutatokea dharura. Safi mheshimiwa raisi, mungu ibariki Tanzania.
 
Mikutano yote wananchi walipinga ila ewura na tanesco wamepandisha kimyakimya
 
Hapo ndo unaona makali ya JPM ukimpa pande hakuachi.
Na Magufuli keshawajulia anajuwa mnapenda kumuona akifukuza fukuza watu ili mwendelee kumuita "Jembe" mkijakushtuka 2020 hana alichofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…