Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Wanazunguka zunguka tu Mkuu miaka nenda miaka rudi kubadilisha watendaji mbali mbali wa TANESCO, lakini tatizo la kweli la mikataba waliyoingia ya kifisadi hawataki kabisa kuligusa. Mikataba ya IPTL ambayo mpaka leo bado inaendelea. Mikataba mbali mbali na makampuni ya ufuaji wa umeme nchini kwa kutumia gesi ya nchini. Hawa wanatumia gesi ya Tanzania lakini cha kushangaza umeme wao wanawauzia TANESCO kwa bei kubwa sana tena kwa dollar! Yote hata wanayakwepa hawataki kabisa kuyagusa.

Watabadilisha watendaji wakuu wa TANESCO hata mara mia kwa mwaka lakini TANESCO tatizo lao kubwa ni mikataba ya kifisadi iliyosainiwa kuanzia awamu ya Mkapa, Kikwete na ambayo inaendelea hadi hii leo. Bila kupambana na hiyo mikataba ya kifisadi utendaji wa TANESCO utaendelea kuyumba kwa miaka mingi sana ijayo.

Mkuu tuna hasara tena kubwa tu kuwa chini ya hawa watu.Ni vigumu hata kuelewa ni nini wanachosimamia.
 
nisha amin watanzania n wazembe sana wakufatilia mambo nyeti,kosa la huyo jamaa kufukuzwa kwanza n m2 wa kaskazn na ukoo wa akina mramba,pili katangaza bei ya umeme hazaran na hapo walikuwa wanamtafutia timing ya kumdisco,lkn pia alipaswa kupandisha bei ya umeme kimya2 kama ilivyopanda awali bila wananch kujua na ninajua wananch wa tanzania walivyokuwa wazembe hawajui mpaka leo bei ya umewe ilishapanda muda mrefu toka pale walipoondoa service charge ndo walipopgwa changa la macho watanzania!

Ili kuweka sawa leo h m2 wa kawaida nenda kanunue umeme wa buku 2 utajua kama bei ilishapanda au la ila kwa kuwa watanzania weng n mazezeta hlo hawatalikubali!

Umeme unit moja kwa sasa n tsh 400 na point kwa m2 anaenunua kwa matumiz ya kawaida hata kama hutakubalina na mimi.

Kilichofanyika ni kuwaingiza wachache kwenye huduma ya REA il kuuaminisha umma kuwa umeme kwa matumiz ya kawaida unit n tsh 100, lkn wanaolipa gharama h n wachache sana il weng wao wanapigwa unit moja kwa tsh 400.

Simu yangu 2 haipigi picha ningeweka hapa risiti!
 
Mabadiliko ya kweli nchii hii ni mpaka pale CCM watakapotoka madarakani.Haya yote ni maigizo tu na wala hakuna la maana hapa wanalolifanya.
 
Acha unafki wewe, unajua process za kupandisha bei ya umeme, mkuu anatafuta kiki tuu ili tubadilishe mawazo kwamba anatujali kumbe ni kitu imetengenezwa, ewura wasingeweza kupandisha umeme bila waziri na ikulu kupitisha.
 
HAPPY NEW YEAR mramba hakika Hii zawadi ni Mbaya sana kwl siku ya Mwazo wa Mwaka watu wamekula kichwa
 

acha ukuda wanajua official kwa barua au mtaani
 
Afadhari ya huyu alichukua mshahara wake wa Dec lkn wale wengine waliomwaga katikati ya mwezi wanagugumia machungu tuu..
 
Mimi nadhani umefika wakati wa viongozi wa serikalini waanzishiwe kozi maalum chuo cha taifa cha uongozi Monduli nasemea hilo kwa sababu nimegundua
kuna kasoro za utendaji na utoaji amri kuhusu kutenguliwa Ukurugenzi wa Mramba kuna makosa yamefanyika kama kuna makosa ambayo alikuwa amyeyalimbikiza hilo sitakuwa na hoja lakini kama ni hili la umeme kwa alivyokuwa amefanya siyo kosa lake bali ni kosa la ambaye hakumshirikisha waziri Mramba aliwajibika kwa kiwango cha mamlaka yake na kupeleka kwenye ngazi ya juu yake baada ya kupokea ikaanza mchakato kwa wadau ikapingwa ewura wamekaa kwa kulewa madaraka wakaamua kutangaza kwa mbwembwe huku waziri akishuhudia sisi tusiokuwapo huko tukajua serikali imebariki sasa ninachoshangaa waliotangaza kwa faida ya asilimia moja tunayowachangia kila tunaponunua umeme wameachwa waendelee kutafuna hiyo asilimia ametoswa mtu aliyepeleka maombi ambayo yangekubaliwa au kukataliwa unajua nataka nimfananishe Mramba na koplo anayekusanya shida za askari na kuzipeleka kwa sajenti wakati wa gwaride la asubuhi itakuwa ni ajabu mkuu wa kombania baada ya kupokea shida za askari na kuamuru koplo apewe adhabu kwa kupokea hizo shida ndiyo yaliyotokea kwa Mramba kama sababu itakuwa hiyo mkuu kateleza kidogo itabidi abatilishe kama alivyofanya kwa DCI
 
hakuna md aliyeimudu tanesco kama mramba wakati utasema

Sio kweli mkuu. Kuna jamaa alikuwa MD wa Tanesco, alikuwa anaitwa Salvatory Mosha, alishakuwa marehemu huyu. Huyu alikuwa mchapa kazi kwelikweli! Alikuwa na wasaidizi wake akina marehemu Wililo na Iranga! Uliza mkongwe yeyote wa lile Shirika, utapata habari yao!
 
Wote hao unawataja nawafahamu vizuri sana ingawaje sijawa mfanyakazi wa shirika sasa sijaelewa ulichojibu mbali na kutaja Mosha ,Wirilo na Iranga umeishia hapo
 

Nakubaliana na wewe kwa huyu D. Mhaiki. Huyu Bwana ni Engineer mzuri sana, alianzia SCADA huko mpaka kafikia hapo alipo, analijua vyema shirika hilo. Asingehitaji mda wa kujifunza uendeshaji na terminologies wanazotumia ndani ya hilo shirika! Wenyewe wanasema; he would have hit the ground running! Hilo la udini na ukabila I'm better than that. It's not my area of interest!
 
Hivi kosa ndio hilo la kuiomba EWURA ipandishe bei ili kuweza kujiendesha?au kuna mengine?
Nadhani labda ni kutangaza hadharani kwa wananchi kuwa umeme utapanda.
Nadhani kupanda umeme utapanda tu ila kimya kimya.

Kama ilivyokuwa kwenye Suala la kukatwa VAT 18% wakati wa kuweka vocha kwenye mitandao ya simu.
Serikali ilikanusha sana kuwa 18 % haitamuhusu mtumiaji simu lakini ilianza kukatwa kimya kimya.
 
Wote hao unawataja nawafahamu vizuri sana ingawaje sijawa mfanyakazi wa shirika sasa sijaelewa ulichojibu mbali na kutaja Mosha ,Wirilo na Iranga umeishia hapo

Nilikuwa namjibu huyo mtu aliyekuwa anambainisha Mramba kuwa ndie the best MD kati ya wote waliowahi kuwepo Tanesco!
 

Uko sahihi kabisa.
Mi nadhani EWURA ifutwe kabisa mana sioni sababu ya kuwa na bodi kila kona ya nchi.
Haya mabodi mabodi yaliundwa kifisadi sana kwa ajili ya kupeana ulaji wa kukaa bila kuzalisha halafu wanalipwa mabilioni.
Hakuna haja ya kuunda bodi ambayo inalipwa kupitia makato wanayokatwa watumiaji wa umeme.
Mtumiaji anawajibika vipi kumlipa mtu akambaye hajamuajiri na wala hana maslahi naye?
EWURA kama ina umuhimu basi iendeshwe kwa fedha za serikali na sio wateja wa TANESCO.
Napendekeza EWURA ifutwe au iendeshwe kupitia kodi anayokatwa mteja ya 18% na sio tena kumkata mteja Pesa kwa ajili ya EWURA.
Hapa ndipo tunapomnyonya mteja wa umeme.

Mramba hakuawa na kosa bali nibkutenguliwa tu ili wengine nao wapate chakula kinono.
Dawa ni kupunguza hayo mamishahara na marupurupu makubwa kupitiliza yanayotokana na wateja kununua umeme kwa bei kubwa.
 
Acha unafki wewe, unajua process za kupandisha bei ya umeme, mkuu anatafuta kiki tuu ili tubadilishe mawazo kwamba anatujali kumbe ni kitu imetengenezwa, ewura wasingeweza kupandisha umeme bila waziri na ikulu kupitisha.


Huyu jamaa anafikiri umeme hautapanda?
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Umeme utapanda tu japo haikuwa na maana yoyote kutangaza hadharani kwani inazidi kuchonganisha serikali na wananchi wake.
TANESCO kwa sasa bado haijaweza kujiendesha. Ndio maana hata umeme wa REA unachangiwa na wadau wengine kwenye ununuzi wa mafuta. TANESCO ili ijiendeshe yenyewe ni lazima ipite kwenye kopindi kigumu kwa muda ili baadae iweze kushusha bei moja kwa moja.
Kwa sasa kuna siasa nyingi.
Nadhani watapandisha tu ila kwa utaratibu fulani wa kimya kimya tu huko baadae.
 
Sasa kama hilo ongezeko lilikuwa linaongeza ubora wa huduma, je njia mbadala itakuwa ni ipi ya kupata fedha ili kufikia huduma bora iliyolengwa? Itakuwa sawa kutoongeza bei ya umeme kama isingesaidia kwa namna yoyote kuongeza ubora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…