Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

mkuu ungeuliza kwanza huo uamuzi sio wa mramba ni baada ya kamati ya majadiliano kati ya wafanyakazi kupitia tuico na bodi then wizara ikathibitisha so uamuzi wa unit 700 sio wa mramba
Watu wanahitaji kufatilia vitu.. la sivyo hili jukwaa litakuwa kama fb.. asante kwa ufanunuzi mzuri
 
Sasa kama hilo ongezeko lilikuwa linaongeza ubora wa huduma, je njia mbadala itakuwa ni ipi ya kupata fedha ili kufikia huduma bora iliyolengwa? Itakuwa sawa kutoongeza bei ya umeme kama isingesaidia kwa namna yoyote kuongeza ubora.
Leo 1.1.2017 Prof. Muhongo amehojiwa na Radio One na kueleza sababu za kusitisha mpango wa EWURA wa kupandisha bei ya Umeme kwa 8.5% kama ifuatavyo: -
1. Kwenye mikutano ya 'public hearing' nchini kote wadau walipinga myongeza ya bei;
2. hadi jana 31.12.2017 EWURA, kinyume na matakwa ya sheria, haikuwa imepeleka ripoti ya uamuzi wake kwa waziri mwenye dhamana, kujadiliwa na kupitishwa/kuthibitishwa kabla ya kutangazwa kwa pendekezo la bei mpya;
3. Ufumbuzi wa matatizo ya kifedha (madeni) wa TANESCO hauwezi utatuliwa kwa kupandisha bei ya Umeme. TANESCO inatakiwa kuwa na mkakati wa ku-improve efficiency kwenye management yake badala ya kuongeza bei ya Umeme; na
4. Wakuu wa TANESCO hawawpaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme. Hii inamaanisha kuwa wananchi wakamuliwe ili ipatikane pesa ya mabosi wa TANESCO kulipana bonus! Prof. Muhongo amesema ameagiza hata hiyo bonus isilipwe au irudishwe kwa waliokwisha kulipwa.
 
Nadhani labda ni kutangaza hadharani kwa wananchi kuwa umeme utapanda.
Nadhani kupanda umeme utapanda tu ila kimya kimya.

Kama ilivyokuwa kwenye Suala la kukatwa VAT 18% wakati wa kuweka vocha kwenye mitandao ya simu.
Serikali ilikanusha sana kuwa 18 % haitamuhusu mtumiaji simu lakini ilianza kukatwa kimya kimya.
Unafahamu ulichokiandika au unajamba tu? Hakuna badiriko lolote ls airtime kwenye vocha unayonunuwa zaidi ukiingiza kuonesha statement ya vat ambayo zamani kampuni za simu walikuwa wanakula wao.
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia

Mkuu, Kheri ya mwaka mpya.

Umeme hauwezi kupanda.

Kwanini gharama za umeme ziwe juu wakati kuna gesi vyanzo vingine ambavyo sasa hivi vimejaa maji kama kule Ruvu?

Unakumbuka raisi JPM alisema kule Ruvu kuna watu walikuwa wakipunguza kina cha maji kwa makusudi?

Hivi mnafikiri raisi JPM hafahamu mambo yalokuwa yakifanywa na mtandao wa mafisadi katika nchi hii?
 
Ahsante Copenhagen DN,

Huo ndio ukweli wenyewe wa kutaka kudumaza akili za watu! Na kwa hakika tumedumazwa na kudumazika na hadi miaka 5 inaisha, Tanzania itaongoza kwa kuwa na mataila ambao ni matokeo ya kuwa conditioned!
 
Ila kuna jambo hapa ambalo sijaelewa... naomba wajuvi wanijuze! Hivi unachomoa vipi Mwalimu wa Chuo kuwa Managing Director wa shirika lenye changamoto lukuki?! Hivi PhD inaweza ku-solve changamoto za TANESCO pasipo na kuwa na uelewa kwa mapana na marefu ya changamoto za TANESCO na energy sector kwa ujumla?! Au Mheshimiwa Daktari alitokea private/public commercial sector kabla hajawa Mhadhiri?
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia

naona TANESCO team mmeanza kulalama!

lazma mtaisoma namba na nyie! mnatakiwa mpate unit 100 tu bure sio 700 nyambafu!
bonus ndo msahau maisha
 
Mkuu, Kheri ya mwaka mpya.

Umeme hauwezi kupanda.

Kwanini gharama za umeme ziwe juu wakati kuna gesi vyanzi vingine ambavyo sasa hivi vimejaa maji kama kule Ruvu?

Unakumbuka raisi JPM alisema kule Ruvu kuna watu walikuwa wakipunguza kina cha maji kwa makusudi?

Hivi mnafikiri raisi JPM hafahamu mambo yalokuwa yakifanywa na mtandao wa mafisadi katika nchi hii?
Tuanze na hilo gas... je, TANESCO nafasi yao ni ipi linapokuja suala la matumizi ya gas? Ni kwamba hawataki tu kutumia gas kwavile they're incompetent, au kivipi?

By the way, hivi unaamini kabisa kwamba as of now Tanzania tuna umeme wa kutosha? Hivi unaamini kabisa kwamba tuna surplus ya umeme?!

Unless you prove otherwise, ninachoamini na ndicho kilichopo ni kwamba bado tuna energy deficit. Kama ndivyo; hivi umeshajiuliza nini kinaweza kutokea endapo matumizi ya umeme yanaongezeka japo kwa 5%? And tell you what... umeme hautoshi wakati watu wanaogopa kutumia majiko na mabirika ya umeme! Ukitaka kugombana na wapangaji wenzako wakugundue kwamba unatumia jiko la umeme!!!

Be informed kwamba wakati mwingine bei inaongezwa just ku-balance matumizi ya umeme! Hata kama ulikuwa unatumia LUKU ya peke yako; bei ya umeme iki-shoot; wala hakuna atakayekuambia rudisha jiko lako la umeme store... wewe mwenyewe ndie utalipeleka store na kutafuta alternatives!

Kwahiyo bei haitapanda only if everything will remain constant or else; it's inevitable unless we want to play politics!!!
 
Tunaomba mwenye bili ya slip ya bili ya umeme tuone kabla ya lile katazo la kwanza la kupanda kwa bei kama kuna mabadiliko yoyote
 
Tuanze na hilo gas... je, TANESCO nafasi yao ni ipi linapokuja suala la matumizi ya gas? Ni kwamba hawataki tu kutumia gas kwavile they're incompetent, au kivipi?

By the way, hivi unaamini kabisa kwamba as of now Tanzania tuna umeme wa kutosha? Hivi unaamini kabisa kwamba tuna surplus ya umeme?!

Unless you prove otherwise, ninachoamini na ndicho kilichopo ni kwamba bado tuna energy deficit. Kama ndivyo; hivi umeshajiuliza nini kinaweza kutokea endapo matumizi ya umeme yanaongezeka japo kwa 5%? And tell you what... umeme hautoshi wakati watu wanaogopa kutumia majiko na mabirika ya umeme! Ukitaka kugombana na wapangaji wenzako wakugundue kwamba unatumia jiko la umeme!!!

Be informed kwamba wakati mwingine bei inaongezwa just ku-balance matumizi ya umeme! Hata kama ulikuwa unatumia LUKU ya peke yako; bei ya umeme iki-shoot; wala hakuna atakayekuambia rudisha jiko lako la umeme store... wewe mwenyewe ndie utalipeleka store na kutafuta alternatives!

Kwahiyo bei haitapanda only if everything will remain constant or else; it's inevitable unless we want to play politics!!!

Nnachofahamu ni kwamba bwana Mramba amekiuka taratibu na hakushauriana na walo juu yake akbla ya kwenda EWURA.

Hata kama alikosea kutia saini mkataba na Symbion mwaka juzi lakini hiyo sio sababu afanye maamuzi ya liwalo na liwe.

Wanaoelewa hili jambo hawana shida nalo.
 
Mkuu, Kheri ya mwaka mpya.

Umeme hauwezi kupanda.

Kwanini gharama za umeme ziwe juu wakati kuna gesi vyanzi vingine ambavyo sasa hivi vimejaa maji kama kule Ruvu?

Unakumbuka raisi JPM alisema kule Ruvu kuna watu walikuwa wakipunguza kina cha maji kwa makusudi?

Hivi mnafikiri raisi JPM hafahamu mambo yalokuwa yakifanywa na mtandao wa mafisadi katika nchi hii?
Ninachohitaji kujua, deni la Tanesco linatokana na nini? Wakilidhibiti hilo umeme hautapanda.
 
Ninachohitaji kujua, deni la Tanesco linatokana na nini? Wakilidhibiti hilo umeme hautapanda.

Tanesco ina madeni mawili,

La kwanza ni hili la Symbion ambalo Tanesco kwa makusudi kabisa walidharau maagizo ya wizara (siyo chini ya Muhongo) pamoja na pengine huko juu na kuendelea kusaini mkataba ambao ni wa miaka 20.

Mkataba huu pamoja na mambo mengine unaitaka Tanesco kuendelea kuilipa fedha Symbion kila mwezi bila kujali kama Symbion wanazalisha umeme au hawazalishi.

Deni la pili ni la IPTL na zile fedha za Escrow ambazo zililiwa na mafisadi.

Tanesco hadi sasa inatumia kiasi cha shilingi bilioni 36 kwa mwezi au dola bilioni 16.76 kuwalipa hawa Symbion na wazalishaji wengine.

Symbion peke yao wanalipwa shilingi bilioni karibu 5 kila mwezi kwa kuwazalishia umeme Tanesco kupitia mitambo yake ya Dar-es-Salaa, Dodoma na Arusha.

Lakini kwa kuwa sasa ule mtambo wa Kinyerezi umekamilika ujenzi wake na una uwezo wa kutoa kiasi cha megawatts 150 utakuwa ukitumia gesi ya kutoka Mtwara na kuzalisha umeme ambao utaingizwa kwenye national Grid.

Tanzania inatakiwa kuzalisha umeme kiasi cha 1,226MW ambao unatakiwa kuwahudumia wananchi wote milioni 47

Halafu kuna 82MW zinazozalishwa na vituo kama Kidatu na vingine.
 
Tanesco ina madeni mawili,

La kwanza ni hili la Symbion ambalo Tanesco kwa makusudi kabisa walidharau maagizo ya wizara (siyo chini ya Muhongo) pamoja na pengine huko juu na kuendelea kusaini mkataba ambao ni wa miaka 20.

Mkataba huu unaitaka Tanesco kuendelea kuilipa fedha Symbion kila mwezi bila kujali kama Symbion wanazalisha umeme au hawazalishi.

Deni la pili la IPTL na zile fedha za Escrow ambazo zililiwa na mafisadi.

Tanesco hadi sasa inatumia kiasi cha shilingi bilioni 36 kwa mwezi au dola bilioni 16.76 kuwalipa hawa Symbion na wazalishaji wengine.

Symbion peke yao wanalipwa shilingi bilioni karibu 5 kila mwezi kwa kuwazalishia umeme Tanesco kupitia mitambo yake ya Dar-es-Salaa, Dodoma na Arusha.

Lakini kwa kuwa sasa ule mtambo wa Kinyerezi umekamilika ujenzi wake na una uwezo wa kutoa kiasi cha megawatts 150 utakuwa ukitumia gesi ya kutoka Mtwara na kuzalisha umeme ambao utaingizwa kwenye national Grid.

Tanzania inatakiwa kuzalisha umeme kiasi cha 1,226MW ambao unatakiwa kuwahudumia wananchi wote milioni 47

Halafu kuna 82MW zinazozalishwa na vituo kama Kidatu na vingine.
Asante mkuu. Kadiri ya maelezo yako umeme bado utakuwa hautoshi hasa kama tume address mahitaji ya sasa na siyo ya miaka mitatu mbele. Na deni pia litaendelea kukua. Ng'ombe wa maskini hazai.
 
Mkuu Richard wanaosaini mikataba yote ya TANESCO si watendaji wakuu wa TANESCO bali ni viongozi wa juu Serikalini. Kumbuka Net Group Solutions, Richmond/Dowans, IPTL, Symbions, Escrow yote hii haikusainiwa na watendaji wa TANESCO. Cha kustaajabisha wote hawataki kuigusa hii mikataba ya kifisadi ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha TANESCO kushindwa kufanya kazi kiufanisi na kuwa na madeni makubwa sana kutokana na mikataba iliyojaa ufisadi wa kutisha.

*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Kutoka Richmond hadi Symbion Power
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 June 2011

Tuseme Ukweli
KAMPUNI ya Marekani ya Symbion Power, imezuia chombo chochote kuchokonoa, kuchunguza na kutoa habari kuhusu mkataba wake wa ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans Costa Rica.

Symbion Power inasema imepewa nguvu za kisheria ya kuzuia mtu kupewa siri za ndani za mipango hiyo bila idhini yake. Kwa hiyo, Symbion Power hawataki waandishi wa habari wadadisi ukweli wa mkataba huo ambao ama utawanufaisha au utawanyonga. Pia inataka wote waridhike kufungiwa mbuzi kwenye gunia na kukubali matakwa yao.
Wanaogopa nini? Kama wamepewa nguvu za kisheria, aliyewapa ni nani? Kwa nini wanaanza kwa kujihami? Kama Symbion Power ni halali kama ilivyo kwenye tovuti, vizingiti vya nini?

Mambo kadhaa yanasababisha watu kutilia shaka. Mathalani wakati inatangaza kuwa imenunua mitambo hiyo hawakuwepo wawakilishi wa kampuni ya Dowans iliyokuwa inamiliki.
Mmiliki wa mitambo hiyo ilielezwa kuwa ni Brigedia Jenerali Mstaafu wa Oman Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi, lakini aliyepewa mamlaka ya kisheria kusimamia mitambo hiyo duniani kote isipokuwa Costa Rica ilikoandikishwa ni Rostam Aziz, mfanyabiashara na Mbunge wa Igunga.

Katika hili, waandishi na Watanzania wanataka kujua Symbion Power imezungumza na nani na wamekamilisha ‘dili’ kwa kiasi gani. Kampuni imewaficha habari waandishi wa Tanzania lakini, mtandao wa www.garp.org umefichua mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa mg 120 imeuzwa kwa dola 120milioni sawa na Sh. 180 bilioni.
Wakati kampuni haitaki watu wajue undani wake imekimbilia kufanya mazungumzo na Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) ili liingie mkataba wa kuuza umeme.

Uharaka huu wa nini? Kwa nini TANESCO inajitia kitanzi cha mazungumzo bila kufuata utaratibu wa awali wa kuitisha zabuni? TANESCO haioni kuwa uwazi unahitajika zaidi kwa sasa hasa kwa mitambo hiyo yenye historia chafu iliyosababisha serikali kuvunjika Februari, 2008?

Jumamosi ya Mei 21, 2011 Symbion Power wanatangaza kununua mitambo ya Dowans na wanadai kuwa wameanza mazungumzo na TANESCO.
Jumatatu ya Mei 23, 2011 Meneja Mawasiliano wa TANESCO, Badra Masoud anatangaza kuwa wameanza mazungumzo na Symbion Power.

Siku inayofuata kamati ya Nishati na Madini inaikaanga serikali na TANESCO kwa kuchukua hatua za kinyonga katika kulipatia ufumbuzi tatizo sugu la umeme.
Vyombo vya habari vinamnukuu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema serikali itaipa Symbion Power ushirikiano kuhakikisha inawasha mitambo hiyo kwa maelezo “tunataka umeme, tunataka maendeleo kwa watu wetu”.

Watanzania wameumwa na nyoka hivyo lazima washtukie kila unyasi ukiwagusa. Richmond Development LLC ni kampuni ya Marekani tena ilishinda zabuni, lakini baadaye ilionekana kuwa feki na kwa hiyo hata mkataba iliopewa ulikuwa batili.
Baadaye Watanzania wakaelezwa Dowans imepewa mkataba wa kufua umeme uliokuwa wa Richmond lakini ukafutwa na kusababisha Dowans kukimbilia Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC). Tatizo si ubora wa kampuni bali usiri katika kuingia mikataba.

Usiri umewaumiza Watanzania kuanzia wakati serikali ilipotia saini kuingiza IPTL huku ikijua athari zake. Baadaye viongozi walewale waliingiza kitapeli na kuipa mkataba kampuni ya Richmond.
Bila aibu viongozi haohao wakaingiza kitapeli Dowans na sasa inakubali wananchi wazuiwe kupata habari juu ya Symbion Power kuhusu dili la mitambo ya Dowans na inavyohaha kuhuisha mkataba wa kuzalisha umeme ambao utauzwa kwa Watanzania.

Power Symbion wanaweza kujitetea kuwa wao wamenunua mitambo na siyo kampuni. Ni kweli, lakini ieleweke kuwa hata Dowans haikununua kampuni ya Richmond. Tatizo ni namna kampuni husika inavyoingia mkataba. Mifano ipo.
Mwaka 1994; Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini aliingiza IPTL, mkataba huo unaitesa TANESCO hadi leo.

Mwaka 2006; Waziri mkuu, Edward Lowassa, alipanda pipa hadi Thailand kuomba mvua. Serikali ikaacha mradi huo ikabariki Richmond/ Dowans iliyosumbua nchi.
Mwaka 2007; Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliruka na mafaili ya mgodi wa Buzwagi hadi Uingereza kutia saini hotelini, tena usiku.

Kila likitokea tatizo la umeme nchini, serikali kwa kushirikiana na TANESCO huandaa mazingira kushinikiza jamii iridhike hatua za kutumia mitambo ya Dowans. Halafu akaletwa Al Adawi kujitambulisha kwamba yeye ndiye ‘Mr Dowans’.
Huyo ndiye alitumiwa kuwaambia waandishi wa habari kuwa yuko tayari kupunguza au kufuta deni lote isipokuwa gharama fulani muradi tu kampuni yake ikubaliwe kuingia mkataba mpya wa kufua umeme.
Al Adawi alitembelea mitambo ile iyoko Ubungo, akakutana na uongozi wa TANESCO na alikwenda ikulu ambako alikutana na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Katika siku ya pili ya ziara yake, TANESCO ikawasha mitambo ile kumpa matumaini Al Adawi kwamba wataunganisha umeme kwenye gridi ya taifa. Suala hilo liliibua mgogoro mwingine.
Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba alivalia njuga mitambo hiyo iwashwe. Mitambo hiyo imo kwenye mapendekezo ya kamati yake kwa serikali.

Baada ya mpango huo kugonga mwamba, wakatumia jumuiya ya wafanyabiashara kupiga kelele juu ya uhaba wa umeme na kushinikiza mitambo ya Dowans iwashwe. Kelele hizo hazikuzaa matunda.
Hapo ndipo Chama cha Wafanyabiashara (TCIA) kikatangaza kununua mitambo hiyo ili wafanye biashara na TANESCO.

Mpango huo ukakwama pia kwa maelezo wamiliki wa Dowans walikuwa wanajigeuza sura.
TANESCO wakabuni tatizo la umeme kwamba katika muda wa siku 10 hivi kuanzia Mei 19, 2011 mgawo utakuwa mkali kwa vile mitambo ya umeme inayotumia gesi Ubungo itafungwa kwa matengenezo.

Siku tatu baadaye, Watanzania walioambiwa na Mahakama Kuu kwamba yasifanyike mazungumzo yoyote kuhusu mitambo ya Dowans bila kujulishwa, kampuni ya Symbion Power ikajitokeza kusema imenunua mitambo hiyo na haraka, serikali inatangaza kuisaidia iwashe mitambo izalishe umeme.

Tanesco ina madeni mawili,

La kwanza ni hili la Symbion ambalo Tanesco kwa makusudi kabisa walidgarau maagizo ya wizara (siyo cini ya Muhongo) na kuendea kusaini mkataba ambao ni wa miama 20.
Mkataba huu unaitaka Tanesco kuendelea kuilipa fedha Symbion kila mwezi bila kujali kama Symbion wanazalisha umeme au hawazalishi.

Deni la pili la IPTL na zile fedha za Escrow ambazo zililiwa na mafisadi.

Tanesco hadi sasa inatumia kiasi cha shilingi bilioni 36 kwa mwezi au dola bilioni 16.76 kuwalipa hawa Symbion na wazalishaji wengine.

Symbion peke yao wanalipwa shilingi bilioni karibu 5 kila mwezi kwa kuwazalishia umeme Tanesco kupitia mitambo yake ya Dar-es-Salaa, Dodoma na Arusha.

Lakini kwa kuwa sasa ule mtambo wa Kinyerezi umekamilika ujenzi wake na una uwezo wa kutoa kiasi cha megawatts 150 utakuwa ukitumia gesi ya kutoka Mtwara na kuzalisha umeme ambao utaingizwa kwenye national Grid.

Tanzania inazalisha umeme kiasi cha 1,226MW ambao utawasaidia wananchi wote milioni 47

Halafu kuna 82MW zinazozalishwa na vituo kama Kidatu na vingine.
 
Back
Top Bottom