BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Wanazunguka zunguka tu Mkuu miaka nenda miaka rudi kubadilisha watendaji mbali mbali wa TANESCO, lakini tatizo la kweli la mikataba waliyoingia ya kifisadi hawataki kabisa kuligusa. Mikataba ya IPTL ambayo mpaka leo bado inaendelea. Mikataba mbali mbali na makampuni ya ufuaji wa umeme nchini kwa kutumia gesi ya nchini. Hawa wanatumia gesi ya Tanzania lakini cha kushangaza umeme wao wanawauzia TANESCO kwa bei kubwa sana tena kwa dollar! Yote hata wanayakwepa hawataki kabisa kuyagusa.
Watabadilisha watendaji wakuu wa TANESCO hata mara mia kwa mwaka lakini TANESCO tatizo lao kubwa ni mikataba ya kifisadi iliyosainiwa kuanzia awamu ya Mkapa, Kikwete na ambayo inaendelea hadi hii leo. Bila kupambana na hiyo mikataba ya kifisadi utendaji wa TANESCO utaendelea kuyumba kwa miaka mingi sana ijayo.

Mkuu tuna hasara tena kubwa tu kuwa chini ya hawa watu.Ni vigumu hata kuelewa ni nini wanachosimamia.