Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Ndo yaleyale ya kuamini Ryoba anaweza kuibadili TBC kwa sababu ya kuwa mwalimu wa waandishi wa habari, leo TBC ni absolute toilet kuliko alivyo Magufuli!
We acha tu ndugu yangu... ndo kuna mdau mmoja hapa kasema "...si ataenda kupatia uzoefu huko huko!"
 
Kuandika Barua haitoshi Ewura na Tanesco kabla ya kutangaza bei mpya walipaswa kusubiri majibu na Kikao pamoja na Serikali. Huwezi kufanya unavyotaka Jambo kubwa kama hili linalo gusa Uchumi wa Nchi na madhara kwa Wananchi.
 
Nashangaa anayeteuliwa anakubali. Ingekuwa mimi, namkatalia. Maadm nipo kwenye kazi nyingine
 
Watumiaji wadgowa umeme tunaumia sana magufuli nia yake kwa wananchi ni nzuri sanaaa tatizo kila anaepewa sekta anataka atengeneze maisha yake kwanza hivyo mm nampongeza sana rais wangu.

Sent from my GT-I8190 using JamiiForums mobile app
 
Anaefuata ni wa EWURA mkuu anasubiri weekend huwa hatumbui katikati ya week coz wengi tutakuwa job.
 
Rais Magufuli na Buhari watajwa kama marais walioangusha matumaini ya wananchi::

Wakitoa tathimini ya mwaka 2016 kuelekea mwaka 2017, Redio ya idhaa ya kiswahili ya ujerumani DW wamewataja marais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Buhari wa Nigeria kuwa ni marais walioangusha matumaini ya wananchi wao hasa vijana na ikizingatiwa kuwa ni marais walioingia kwa mbwembwe nyingi na kutoa matumaini mapya ya mafanikio.

Wakimzungumzia Rais Magufuli, walisema wanachi wengi walitegemea hali zao za uchumi zikiimarika lakini badala yake wamejikuta katika hali ngumu zaidi, huku vijana wakikata tamaa pale wanapowaona watangulizi wao wakitopea katika lindi la umasikini wa kutupwa.

Wakizungumzia demokrasia walisema rais ameshindwa kabisa katika nyanja hii, anaiendesha nchi kwa mkono wa chuma, matumizi mabaya ya madaraka na upendeleo, kuwakamata na kuwatia ndani wakosoaji wake, kusitisha taasisi mbalimbali, uhuru wa habari na kujieleza umebinywa na kuwafanya hata viongozi wa dini waliokua wanakosoa pale wanapoona hapaendi sawa ku kaa kimya.

Upande wa elimu, vijana wengi waliokua wanashangilia leo wanalia kwa kuwanyima mikopo watoto wa masikini, ajira hakuna, walimu wanayimwa stahiki zao, ufukuzaji usiofuata sheria na maslai duni. Elimu inayotolewa bure imeshindwa kukidhi matarajio.

Uchumi walisema hali ni mbaya sana, masoko yamedorora, biashara zinafungwa,ajira zinapunguzwa hali ambayo haitii matumaini kwa vijana, kodi kubwa ambazo haziendani na kipato halisi cha biashara.

Walimalizia kwa kusema hali ya matumaini kwa wanachi wa Tanzania imefifia sana na ukataji wa matumaini ni mkubwa sana hivyo inahitajika mabadiliko chanya ya kiuchumi na kisera.

Chanzo : DW

DW ni wapuuzi tu. Walishaonesha upuuzi wao msimu wa kampeni walipofanya mchezo kama wa Ben Saatisa kwa mtangazaji wao yule wa kike wa Zanzibar.

Ni bora wahangaike na Kansela wao Anjela anayeivuruga Ujerumani kwa kuruhusu wahamiaji zaidi ya milioni moja kuingia nchini humo.
 
Ndugu yangu Richard,

Hebu nisaidie na hapa!! Habari zinazo-trend hivi sasa ni kwamba sababu kubwa ya kutumbuliwa Mramba ni kwa sababu hakufuata taratibu!

Nikaamua kupekua pekua na hatimae kukutana na taarifa hii ya TANESCO:
EWURA6.png

Nikaona hawa TANESCO wasitufanye watu hatuna akili... Agizo la Kubadilisha Bei za Umeme la Mwaka 2016 ni dubwasha gani hilo tena! Nikaamua kutafuta ukweli ambao ndani ya dakika moja nikakutana nao kwenye tovuti ya Wizara ya Nishati na Madini ambalo sehemu yake linasema:
EWURA7.png

SWALI 1: Ikiwa serikali hawakushirikishwa; nini maana ya hicho kifungu #4 hapo juu?! Serikali inaweza vipi kuzungumzia kusitishwa kwa jambo wasilolifahamu?

Hebu tuambieni ukweli... hivi tatizo ni kwamba serikali haikufahamu au ndo ile kuliana timing uingie kwenye 18 wakutumbue?! Au tatizo ni kwamba walichelewesha... badala ya August 31, 2016 wao wakawasilisha:
EWURA9.png

Mbona hatuelewi elewi?!
 
Eti "vitu rahisi"; my foot! Man go back to prep school, Mramba out, hatarudi tena, he has never been indispensable, hata kama amekua collateral damage, mwendo mdundo kusaka watu wote walioumbwa kwa mfano wa shetani wanaowatesa wananchi wanyonge walioumbwa kwa mfano wa Mungu na kuwatumbulia mbali.
 
Vitu vidogo sana hivi ndugu yangu! Inawezekana Richard ni baba wa familia tena mwenye madaraka kwenye serikali ya JPM!

Trust me, watu wa aina hiyo hawawezi kuvumilia criticism!! Na ni social factor kamwe huwezi kuwalaumu!

Sasa hebu pata picha Kamanda IGP Ernest Mangu anaingia JF kwa jina la chige... hivi unadhani atavumilia criticism? THUBUTU...! Hata kama anajiita chige but still yeye ni Mangu; baba wa familia na Mkuu wa Jeshi la Polisi!!!

Kwahiyo hilo la kutoka nje mara moja moja wala lisikupe shida; msisitizo uwe ni kwenye kutovuka mipaka!!!!
wapo wengi humu wa mfano huo mkuu.....[emoji45] [emoji45] ....!!..
 
Back
Top Bottom