Rais Magufuli na Buhari watajwa kama marais walioangusha matumaini ya wananchi::
Wakitoa tathimini ya mwaka 2016 kuelekea mwaka 2017, Redio ya idhaa ya kiswahili ya ujerumani DW wamewataja marais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Buhari wa Nigeria kuwa ni marais walioangusha matumaini ya wananchi wao hasa vijana na ikizingatiwa kuwa ni marais walioingia kwa mbwembwe nyingi na kutoa matumaini mapya ya mafanikio.
Wakimzungumzia Rais Magufuli, walisema wanachi wengi walitegemea hali zao za uchumi zikiimarika lakini badala yake wamejikuta katika hali ngumu zaidi, huku vijana wakikata tamaa pale wanapowaona watangulizi wao wakitopea katika lindi la umasikini wa kutupwa.
Wakizungumzia demokrasia walisema rais ameshindwa kabisa katika nyanja hii, anaiendesha nchi kwa mkono wa chuma, matumizi mabaya ya madaraka na upendeleo, kuwakamata na kuwatia ndani wakosoaji wake, kusitisha taasisi mbalimbali, uhuru wa habari na kujieleza umebinywa na kuwafanya hata viongozi wa dini waliokua wanakosoa pale wanapoona hapaendi sawa ku kaa kimya.
Upande wa elimu, vijana wengi waliokua wanashangilia leo wanalia kwa kuwanyima mikopo watoto wa masikini, ajira hakuna, walimu wanayimwa stahiki zao, ufukuzaji usiofuata sheria na maslai duni. Elimu inayotolewa bure imeshindwa kukidhi matarajio.
Uchumi walisema hali ni mbaya sana, masoko yamedorora, biashara zinafungwa,ajira zinapunguzwa hali ambayo haitii matumaini kwa vijana, kodi kubwa ambazo haziendani na kipato halisi cha biashara.
Walimalizia kwa kusema hali ya matumaini kwa wanachi wa Tanzania imefifia sana na ukataji wa matumaini ni mkubwa sana hivyo inahitajika mabadiliko chanya ya kiuchumi na kisera.
Chanzo : DW