Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

ulipotangazwa kuwa umeme bei juu watu wa ndio kama kawaida walipongeza na kutunga sababu sasa hivi imesitishwa watu wa ndio wanapongeza na ukiongezeka tena watu wa ndio watapongenza tena.ila sisi kina gogo la shamba tutapongeza pale umeme utakaposhuka bei
 
Jana nimenunua umeme wa 7000, cost 5737.71 service charge 0.00,tax Tzs1262.29, unit 19.7kwh.kwahiyo ukifanya hesabu utaona unit moja ni Tzs 291.25431472 baada ya kutoa tax
 
Tunaomba mwenye bili ya slip ya bili ya umeme tuone kabla ya lile katazo la kwanza la kupanda kwa bei kama kuna mabadiliko yoyote
5bc0bfc40666a8472140d434c8979c0c.jpg
1483349586636.jpg
1483349586636.jpg
 
Ila kuna jambo hapa ambalo sijaelewa... naomba wajuvi wanijuze! Hivi unachomoa vipi Mwalimu wa Chuo kuwa Managing Director wa shirika lenye changamoto lukuki?! Hivi PhD inaweza ku-solve changamoto za TANESCO pasipo na kuwa na uelewa kwa mapana na marefu ya changamoto za TANESCO na energy sector kwa ujumla?! Au Mheshimiwa Daktari alitokea private/public commercial sector kabla hajawa Mhadhiri?
HAHAHA UMeNIFURAHISHA KWELIII..
UNAJUA KUNA WACHEZAJI CHELSEA WANA DEGREE ZAO NZURI NA WANACHEZA MPIRA SAFIKABISA BILA KUWA NA DEGREE YA MICHEZO

ONDOENI AKILI HIZO ATUTAFIKA
 
Daaaah yani hakuna watu wanafiki dunia hii kama UKAWA,nyie watu pepo hamtaiona kwa unafiki na uzandiki ulivoawakaa,mmepiga kelele hapa jf tangu jpm aingie madarakani kuwa tanesco ni jipu,tulitangaziwa kupanda kwa gharama za umeme mkasema jpm hana la kufanya tanesco imemshinda,jana kamtumbua mkaskazini mwenzenu mmeanza kumdhihaki jpm na mmekuwa upande wa tanesco,kweli hii mitandao izimwe nyie nyumbu tuwasikie kwa sauti zenu halisi
una pepopunda wew
 
Jana nimenunua umeme wa 7000, cost 5737.71 service charge 0.00,tax Tzs1262.29, unit 19.7kwh.kwahiyo ukifanya hesabu utaona unit moja ni Tzs 291.25431472 baada ya kutoa tax
UNATEGEMEA UKO KWENYE TARIFF GANI MKUU

WAPO WANAONUNUA 9000TZS NA KUPEWA UNIT 75...SO HILO HALINASHIDA KABISA

CHAMAANA ANGALIA TARIFF
 
[adeni ="Automata, post: 19120309, member: 277034"]EWURA si shida kivile, tatizo kuu ni TANESCO-ubunifu mdogo.
Tushawashauli sana wasikimbilie kuomba bei iongezwe badala yake tuliwashauli wasimamie upotevu wa umeme na wakakusanye madeni ili wafidie gharama za uendeshaji.[/QUOTE]
Madeni yao makubwa yako serikalini na taasisi za umma, maajabu gani unataka wafanye ili kukusanya hayo madeni. Acheni siasa kwenye vitu serious.
 
Ndugu yangu Richard,

Hebu nisaidie na hapa!! Habari zinazo-trend hivi sasa ni kwamba sababu kubwa ya kutumbuliwa Mramba ni kwa sababu hakufuata taratibu!

Nikaamua kupekua pekua na hatimae kukutana na taarifa hii ya TANESCO:
View attachment 453244
Nikaona hawa TANESCO wasitufanye watu hatuna akili... Agizo la Kubadilisha Bei za Umeme la Mwaka 2016 ni dubwasha gani hilo tena! Nikaamua kutafuta ukweli ambao ndani ya dakika moja nikakutana nao kwenye tovuti ya Wizara ya Nishati na Madini ambalo sehemu yake linasema:
View attachment 453255
SWALI 1: Ikiwa serikali hawakushirikishwa; nini maana ya hicho kifungu #4 hapo juu?! Serikali inaweza vipi kuzungumzia kusitishwa kwa jambo wasilolifahamu?

Hebu tuambieni ukweli... hivi tatizo ni kwamba serikali haikufahamu au ndo ile kuliana timing uingie kwenye 18 wakutumbue?! Au tatizo ni kwamba walichelewesha... badala ya August 31, 2016 wao wakawasilisha:
View attachment 453263
Mbona hatuelewi elewi?!
Sarakasi daily [emoji37]
 
You are right...

Alipaswa kusikilizwa...naskia kuna group liko nyuma ya hii kadhia ambayo hawakuwa wanampenda mramba aendelee kuwepo pale

Mramba ni mtu wa mungu na mwenye iman kali sana ya kilokole...

Therefore magumashi na madeal kwake ni Big No...

Hata kwenye seke seke la Escrow alitafutwa sana ili alambishwe ngawira ila akachomoa na kubaki salama na smart kama alivyo

Infact Mramba kaikuta Tanesco ya hovyo ile iliyoachwa na kina Mhando lakin akajitahid kuirekebisha na kuifanya angalau iwe na nafuu kuliko huko awali.

Juma Poor Manager ameendeleza maamuz yake ya mlipuko...
Nimekuwia radhi. Wamemsikiliza? Unaleta siasa kwenye scientific issues. Mambo ya kuwaza dhambi ni ya revelations not realistic, they do not abide by scientific principles. Huyu ni mtaalamu, angelisikilizwa, akaambiwa hapana hatukubali bei hii! Yaani ku propose bei ni kosa? Think deep! Ichukulie sawa na Judge anavyotoa hukumu ikatenguliwa Court of appeal!
Kwa taarifa yako, siko Tanesco na ninaumia sana kwa bei ya Tanesco, but we have to follow laws, procedure and all rules before us for guidence
 
Hivi ukifukuzwa kazi na mwajiri wako inakuwaje?? Unaendelea kuwa mfanyakazi au unakoma kuwa mfanyakazi?? Mkurugenzi aliajiriwa na Raisi na amefukuzwa na Rais na wala hajasimamishwa, kwahiyo hapo ni kuchukua kila kilicho chako na kuondoka, hakuna ajira hapo tena...

Sent from my SM-A710F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom