Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Kwa ufupi anachokifanya huyu Juma Poor Manager ni kuharibu na kuboronga tuh

Let say he is right kachukizwa na maamuz ya kupandishwa kwa bei ya umeme ni obvious kwamba Mramba hawez kufanya hivyo bila baraka ya bodi..sasa anaiachaje bodi na kumuondoa mramba.

Pili shirika kama Tanesco linahitaji taaluma ya uendeshaji na siyo kuchukua intruder ambae hata hafaham na hana taaluma hiyo na wala hana experience ya uendeshaji

Mfano Dr Idrisa Rashid ilimchukua muda sana hadi kuja kumaster challanges na kusonga mbele

Wapo watu hapo Tanesco wenye uwezo mkubwa tuh kama Engineer Nazir Kachwamba...Engineer Deklan Mhaiki...na kadhalika ambao may be wangeweza kumrith mramba

Sasa kukimbilia kufanya maamuz ya mlipuko kama hayo ni kutuaminisha kwamba kuna watu wake alishawaandaa na anawatafutia kazi...ma kututhibitishia kwamba katika awamu hii wachaga na waislam ni watu wa kuogopwa kama ukoma
Deklani Mhaiki ameshafariki na how unashauri Rubani ndio akawe boss wa Tanesco (UMEME)
 
Mkuu, kheri ya Mwaka Mpya.

Mramba hajaonewa ila naona huna facts kuhusu khasa kilichomtoa hapo Tanesco.

Inawezekana likawa ni suala la EWURA au pia tangu mwezi may alipoagizwa asitishe mazungumzo na Symbion kuhusu PPA (power production agreement) na serikali.

Lakini pia inawezekana na gharama kubwa ambazo Tanesco inalipa kwa IPP independent power producers.

Utakumbuka hotuba ya bajeti ya profesa Muhongo bungeni mwezi Juni alisema kwamba serikali ipo kwenye mchakato wa kuondokana na IPPs kwa kuwa sasa tuna hata gesi kutoka Mtwara.

Mramba ameagizwa na serikali kuangalai mikataba ambayo Tanesco ilisaini na hawa IPPs na khasa ule wa Symbion ambao wanalipwa kiasi cha dola bilioni 5 kwa mwezi kwa kuwauzia umeme Tanesco kwenye mikoa ya Dar, Arusha na Dodoma.

Jambo baya kabisa kuhusu huu mkataba wa PPA ni kwamba iwe umeme upo au hakuna lazima Tanesco wawalipe Symbion kasi hicho cha fedha kila mwezi.

Na tatizo Mramba alisaini mkataba huo harakaharaka kabla ya raisi JPM kuingia, hivyo unategemea nini hapo?
Tanesco is synonyms to Serikali unless you tell me otherwise. Nitashukuru kama utajibu hoja zangu zote kwani ndio tutaeleweshana more holistically.
 
Tulitarajia,bado yule wa NHC.Nawashauri watumishi wa umma kuepukana na madili,mtaumia huyu jamaa hatanii.Uongeze bei ya umeme,hela hakuna ,na viagenta vyako vya nyuma ya pazia ,wenzako wamekuruka kruuuuuuu....peke yako kwenye nyavu.
 
Hii hatari sasa
Hatari gani wewe chaliii yangu nchi mshaambiwa ya viwanda hala mnapandisha bei ya umeme na mablablaaa mengi huyo mwekezaji mtampatia wapi kwanini wasiende kujifunza nchi za wengine wanafanyaje umeme unakuwa mzuri watu tunaishi roho juu juu kama digi digi asante sana Rais Magufuli usisite kutumbua pale unapoona kuna mtu analeta masihara na uchumi wa nchi.
 
Duh...... Yaani siku ya kwanza tu ya mwaka 2017, tayari Magu kauanza kwa kutumbua mtu!

Basi tutarajie mwaka huu utakuwa wa utumbuaji wa kutisha zaidi .......
UNASHIDA YA KUTOTAMBUA UWAJIBIKAJI UNATAKAAENDELEE NA MAKOSA ? KAMA HANA MAKOSA SI AENDE MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE ? USIONYESHE CHUKI ZAKO BINAFSI KWENYE PUBLIC !
 
Ukiwa muongo unapaswa uwe na kumbukumbu Mhe. Anataka wasomi na kahaidi elimu bure lakini kila siku kazi kuchukua wahadhiri na kuwapa vyeo mi nadhani lengo lake wasomi wote anataka awape vyeo ili asiwepo wa kumpinga zamu yake ya kutumbuliwa itafika tu maana wanasema "anayeua kwa upanga atauawa kwa upanga"
 
Mhhh utumbuaji huu ila wa ewura naona kapona
Rais Magufuli leo ametengua rasmi uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO), Eng. Felchesmi Mramba.

Aidha Rais amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kukaimu nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mwinuka alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

Mheshimiwa Raisi ungeenda mbali zaidi ya hapo na kuitupia uzito wa pekee hii EWURA,haiwezekani na haiingii akilini kwa taasisi nyeti kama EWURA kutumika kama muhuri wa kuhalalisha bei kandamizi kwa wananchi.Ikumbukwe wananchi tunailipa EWURA fedha nyingi sana kwa ajili ya kututetea,yaani kuhakikisha tunalipa tozo stahiki kutokana na gharama stahiki na si vinginevyo.
Kwa maantiki hiyo ni dhahiri EWURA wamekosa uhalali wa kuwa mtetezi wetu,hivyo ingekuwa ni busara hii taasisi yaani EWURA ingefutiliwa mbali au viongozi wake waandamizi kutumbuliwa.
 
Hatari gani wewe chaliii yangu nchi mshaambiwa ya viwanda hala mnapandisha bei ya umeme na mablablaaa mwengi huyo mwekezaji mtampatia wapi kwanini wasiende kujifunza nchi za wengine wanafanyaje umeme unakuwa mzuri watu tunaishi roho juu juu kama digi digi asante sana Rais Magufuli usisite kutumbua pale unapoona kuna mtu analeta masihara na uchumi wa nchi.
NDIYO HAPA KAZI TU !
 
Mheshimiwa Raisi ungeenda mbali zaidi ya hapo na kuitupia uzito wa pekee hii EWURA,haiwezekani na haiingii akilini kwa taasisi nyeti kama EWURA kutumika kama muhuri wa kuhalalisha bei kandamizi kwa wananchi.Ikumbukwe wananchi tunailipa EWURA fedha nyingi sana kwa ajili ya kututetea,yaani kuhakikisha tunalipa tozo stahiki kutokana na gharama stahiki na si vinginevyo.
Kwa maantiki hiyo ni dhahiri EWURA wamekosa uhalali wa kuwa mtetezi wetu,hivyo ingekuwa ni busara hii taasisi yaani EWURA ingefutiliwa mbali au viongozi wake waandamizi kutumbuliwa.
BILA RESEARCH USISEME HAYO NI MAONI YAKO TU YA BILA UCHUNGUZI WA KINA, MHE.RAIS HAKURUPUKI !
 
Tanesco is synonyms to Serikali unless you tell me otherwise. Nitashukuru kama utajibu hoja zangu zote kwani ndio tutaeleweshana more holistically.

Synonyms means - "the same or nearly the same".

Hivyo Tanesco ina ukaribu na serikali kwa maana ya kuisaidia au kufanya kazi kwa niaba ya serikali katika sera ya nishati kupitia wizara ya nishati na madini.

Lakini, hiyo haimaanishi kwamba Tanesco ndiyo serikali kwa maana kwamba wanaweza kujiamulia watakavyo.

Raisi JPM alipokuwa akifungua mtambo wa gesi wa Kinyerezi katikati ya mwaka jana alitoa agizo (directive) kwa Tanesco (Mramba) kwamba wasiingie mikataba ingine au mipya au kuiongeza muda kwa IPPs.

Na alisema wazi kwamba hii mikataba ni mwanya wa IPPs kuwakamua wananchi wa hali ya chini kupitia upandishaji bei ya umeme.

Sasa hata kama wewe ni CEO wa taasisi kama Tanesco, si lazima ukumbuke kuna Serikali?
 
Nimemuelewa Jenerali Ulimwengu aliposema tz sasa inaongozwa kwa milipuko tu.TANESCO ipo chini ya wizara ya Nishati na madini, ndio ilipendekeza kwa mamlaka ya EWURA kuomba kupandisha bei ya umeme. Baadae Waziri wa Nishati akasema hawezi kukubali EWURA kupandisha bei. lakin alikubali Tanesco kupendekeza bei ipande? au Tanesco haipo chini ya wizara yake? .Ewura isingetangaza bei kupanda kama Tanesco isingependekeza. Na msingi wa Tanesco kutaka bei ipande ni kwasababu ya gharama kubwa ya uendeshaji. Tanesco inadaiwa mabilioni na kampuni ya symbion iliyochukua mitambo ya kampuni ya kifisadi Dowans, Tanesco inadaiwa mabilion na kampuni ya kifisadi ya IPTL ambayo pamoja na misingi ya kuitaifisha na azimio la bunge kusisitiza, bado serikali imegoma kutekeleza tangu Nov2014 mpaka leo.Bei ya umeme isipopanda mnadhani Tanesco watatoa pesa wapi? jibu ni jepesi Hazina ya serikali. kwamba serikali itatumia pesa ambazo ingetumia kwenye dawa kuendelea kuibeba Tanesco. ndio matunda ya serikali butu ktk vita ya ufisadi kwenye sekta ya umeme......
 
Rais Magufuli leo ametengua rasmi uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO), Eng. Felchesmi Mramba.

Aidha Rais amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kukaimu nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mwinuka alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

"Wakuu wa TANESCO hawapaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme."

Next iwe board iliyoidhinia kulipana huko.
 
•••
NABARIKI EWURA IFUTWE HAINA TIJA KWA WATANZANIA WALALAHOI......ASANTE JPM
 
Back
Top Bottom