Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Mkuu Richard wanaosaini mikataba yote ya TANESCO si watendaji wakuu wa TANESCO bali ni viongozi wa juu Serikalini. Kumbuka Net Group Solutions, Richmond/Dowans, IPTL, Symbions, Escrow yote hii haikusainiwa na watendaji wa TANESCO. Cha kustaajabisha wote hawataki kuigusa hii mikataba ya kifisadi ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha TANESCO kushindwa kufanya kazi kiufanisi na kuwa na madeni makubwa sana kutokana na mikataba iliyojaa ufisadi wa kutisha.

*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Kutoka Richmond hadi Symbion Power
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 June 2011

Tuseme Ukweli
KAMPUNI ya Marekani ya Symbion Power, imezuia chombo chochote kuchokonoa, kuchunguza na kutoa habari kuhusu mkataba wake wa ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans Costa Rica.

Symbion Power inasema imepewa nguvu za kisheria ya kuzuia mtu kupewa siri za ndani za mipango hiyo bila idhini yake. Kwa hiyo, Symbion Power hawataki waandishi wa habari wadadisi ukweli wa mkataba huo ambao ama utawanufaisha au utawanyonga. Pia inataka wote waridhike kufungiwa mbuzi kwenye gunia na kukubali matakwa yao.
Wanaogopa nini? Kama wamepewa nguvu za kisheria, aliyewapa ni nani? Kwa nini wanaanza kwa kujihami? Kama Symbion Power ni halali kama ilivyo kwenye tovuti, vizingiti vya nini?

Mambo kadhaa yanasababisha watu kutilia shaka. Mathalani wakati inatangaza kuwa imenunua mitambo hiyo hawakuwepo wawakilishi wa kampuni ya Dowans iliyokuwa inamiliki.
Mmiliki wa mitambo hiyo ilielezwa kuwa ni Brigedia Jenerali Mstaafu wa Oman Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi, lakini aliyepewa mamlaka ya kisheria kusimamia mitambo hiyo duniani kote isipokuwa Costa Rica ilikoandikishwa ni Rostam Aziz, mfanyabiashara na Mbunge wa Igunga.

Katika hili, waandishi na Watanzania wanataka kujua Symbion Power imezungumza na nani na wamekamilisha ‘dili’ kwa kiasi gani. Kampuni imewaficha habari waandishi wa Tanzania lakini, mtandao wa www.garp.org umefichua mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa mg 120 imeuzwa kwa dola 120milioni sawa na Sh. 180 bilioni.
Wakati kampuni haitaki watu wajue undani wake imekimbilia kufanya mazungumzo na Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) ili liingie mkataba wa kuuza umeme.

Uharaka huu wa nini? Kwa nini TANESCO inajitia kitanzi cha mazungumzo bila kufuata utaratibu wa awali wa kuitisha zabuni? TANESCO haioni kuwa uwazi unahitajika zaidi kwa sasa hasa kwa mitambo hiyo yenye historia chafu iliyosababisha serikali kuvunjika Februari, 2008?

Jumamosi ya Mei 21, 2011 Symbion Power wanatangaza kununua mitambo ya Dowans na wanadai kuwa wameanza mazungumzo na TANESCO.
Jumatatu ya Mei 23, 2011 Meneja Mawasiliano wa TANESCO, Badra Masoud anatangaza kuwa wameanza mazungumzo na Symbion Power.

Siku inayofuata kamati ya Nishati na Madini inaikaanga serikali na TANESCO kwa kuchukua hatua za kinyonga katika kulipatia ufumbuzi tatizo sugu la umeme.
Vyombo vya habari vinamnukuu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema serikali itaipa Symbion Power ushirikiano kuhakikisha inawasha mitambo hiyo kwa maelezo “tunataka umeme, tunataka maendeleo kwa watu wetu”.

Watanzania wameumwa na nyoka hivyo lazima washtukie kila unyasi ukiwagusa. Richmond Development LLC ni kampuni ya Marekani tena ilishinda zabuni, lakini baadaye ilionekana kuwa feki na kwa hiyo hata mkataba iliopewa ulikuwa batili.
Baadaye Watanzania wakaelezwa Dowans imepewa mkataba wa kufua umeme uliokuwa wa Richmond lakini ukafutwa na kusababisha Dowans kukimbilia Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC). Tatizo si ubora wa kampuni bali usiri katika kuingia mikataba.

Usiri umewaumiza Watanzania kuanzia wakati serikali ilipotia saini kuingiza IPTL huku ikijua athari zake. Baadaye viongozi walewale waliingiza kitapeli na kuipa mkataba kampuni ya Richmond.
Bila aibu viongozi haohao wakaingiza kitapeli Dowans na sasa inakubali wananchi wazuiwe kupata habari juu ya Symbion Power kuhusu dili la mitambo ya Dowans na inavyohaha kuhuisha mkataba wa kuzalisha umeme ambao utauzwa kwa Watanzania.

Power Symbion wanaweza kujitetea kuwa wao wamenunua mitambo na siyo kampuni. Ni kweli, lakini ieleweke kuwa hata Dowans haikununua kampuni ya Richmond. Tatizo ni namna kampuni husika inavyoingia mkataba. Mifano ipo.
Mwaka 1994; Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini aliingiza IPTL, mkataba huo unaitesa TANESCO hadi leo.

Mwaka 2006; Waziri mkuu, Edward Lowassa, alipanda pipa hadi Thailand kuomba mvua. Serikali ikaacha mradi huo ikabariki Richmond/ Dowans iliyosumbua nchi.
Mwaka 2007; Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliruka na mafaili ya mgodi wa Buzwagi hadi Uingereza kutia saini hotelini, tena usiku.

Kila likitokea tatizo la umeme nchini, serikali kwa kushirikiana na TANESCO huandaa mazingira kushinikiza jamii iridhike hatua za kutumia mitambo ya Dowans. Halafu akaletwa Al Adawi kujitambulisha kwamba yeye ndiye ‘Mr Dowans’.
Huyo ndiye alitumiwa kuwaambia waandishi wa habari kuwa yuko tayari kupunguza au kufuta deni lote isipokuwa gharama fulani muradi tu kampuni yake ikubaliwe kuingia mkataba mpya wa kufua umeme.
Al Adawi alitembelea mitambo ile iyoko Ubungo, akakutana na uongozi wa TANESCO na alikwenda ikulu ambako alikutana na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Katika siku ya pili ya ziara yake, TANESCO ikawasha mitambo ile kumpa matumaini Al Adawi kwamba wataunganisha umeme kwenye gridi ya taifa. Suala hilo liliibua mgogoro mwingine.
Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba alivalia njuga mitambo hiyo iwashwe. Mitambo hiyo imo kwenye mapendekezo ya kamati yake kwa serikali.

Baada ya mpango huo kugonga mwamba, wakatumia jumuiya ya wafanyabiashara kupiga kelele juu ya uhaba wa umeme na kushinikiza mitambo ya Dowans iwashwe. Kelele hizo hazikuzaa matunda.
Hapo ndipo Chama cha Wafanyabiashara (TCIA) kikatangaza kununua mitambo hiyo ili wafanye biashara na TANESCO.

Mpango huo ukakwama pia kwa maelezo wamiliki wa Dowans walikuwa wanajigeuza sura.
TANESCO wakabuni tatizo la umeme kwamba katika muda wa siku 10 hivi kuanzia Mei 19, 2011 mgawo utakuwa mkali kwa vile mitambo ya umeme inayotumia gesi Ubungo itafungwa kwa matengenezo.

Siku tatu baadaye, Watanzania walioambiwa na Mahakama Kuu kwamba yasifanyike mazungumzo yoyote kuhusu mitambo ya Dowans bila kujulishwa, kampuni ya Symbion Power ikajitokeza kusema imenunua mitambo hiyo na haraka, serikali inatangaza kuisaidia iwashe mitambo izalishe umeme.

Tuko pamoja mkuu.

Ndiyo maana ilikuwa ni kosa kwa Mramba kuendeleza mazungmzo na Symbion wakati raisi na timu yake bado hawajapitia huu mkataba wa sasa.

Si unafanya kitu kimoja baada ya kingine au?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia
Huyu Mramba walishapanga kumfukuza! Ila pia walitaka kuvuna kutoka kwake! Political gain! Sasa wameandaa movie na kuicheza ili kutupumbaza! Tanzania yetu!
 
Asante mkuu. Kadiri ya maelezo yako umeme bado utakuwa hautoshi hasa kama tume address mahitaji ya sasa na siyo ya miaka mitatu mbele. Na deni pia litaendelea kukua. Ng'ombe wa maskini hazai.

Siyo kwamba umeme hautoshi bali unafanywa uonekane hautoshi ili kampuni binafsi za kuzalisha umeme ziwe zinafanya biashara na tanesco kwa kutumia mgongo wa mtanzania wa kipato cha kati na cha chini.
 
Nnachofahamu ni kwamba bwana Mramba amekiuka taratibu na hakushauriana na walo juu yake akbla ya kwenda EWURA.

Hata kama alikosea kutia saini mkataba na Symbion mwaka juzi lakini hiyo sio sababu afanye maamuzi ya liwalo na liwe.

Wanaoelewa hili jambo hawana shida nalo.
Naona kuna mabadiliko ya tune hivi sasa...

Tune ya sasa naona imekuwa "...hakufuata taratibu... hakuwashirikisha wale walio juu yake!"

Tune hii imeanza kusikika kwa Mwele Malecela!

Hebu nisaidie jambo moja! Hapa chini ni sehemu ya tangazo la EWURA juu ya nia ya TANESCO kupandisha bei ya umeme!
EWURA.png

Tangazo ni la Octoba 04, 2016. Na kwa kumbukumbu zangu kupitia kipindi cha Kipima Joto ITV, hili suala lilijadiliwa na wadau! Hilo ni takwa kwa mujibu wa sheria za EWURA kama wanavyothibitisha wenyewe kwenye tangazo husika:

EWURA1.png

Now tell me: Unataka kuniambia wakato yote hayo yanafanyika wazi wazi bado serikali ilikuwa haifahamu nini kilikuwa kinaendelea? Kama ilikuwa haifahamu; kuna maana gani basi ya kuwa na serikali isiyofahamu hata kinachoendelea ndani ya taasisi zake?!

Au ni kwamba serikali ilikuwa inafahamu kilichokuwa kinaendelea lakini badala ya kuzuia from the beginning wakaamua kuacha kiendelee ili ipate justification za kutumbua?!

I am sorry to say kwamba Meneja bora hapimwi kutokana na uwezo wake wa kutimua wafanyakazi walio chini yake bali anapimwa kutokana na uwezo wake wa kuzuia crisis zinazoweza kusababisha kupoteza timu yake!

Ikiwa aina yenyewe ya uongozi ndio huu wa kuliana timing uharibu ili utumbuliwe basi nasikitika kusema kwamba for the time being, hii nchi ina uongozi mbovu ambao haujapata kutokea tangu tupate uhuru!

Huwezi kuacha watu wavunje sheria ili tu hatimae upate sababu ya kutumbua... this's totally administrative failure!

Kama hoja ni kwamba Mramba hakufuata taratibu; serikali walikuwa na uwezo wa kupiga stop kabla hata hao EWURA hawajapoteza raslimali kuitisha vikao!

Na kama ni kutumbuliwa; basi hao akina Mramba wangetumbuliwa baada ya serikali kupiga stop lakini wao wakaendelea! Tena wangetumbuliwa tangu mara baada ya kuitisha Mkutano ITV lakini inaonesha wazi serikali wasingekuwa na grounds za kufanya hivyo kwahiyo wakawaacha waendelee ili hatimae wapate cheap grounds zitakazo-sound kwa wananchi kwamba wamewatumbua kwa sababu wamepandisha bei ya umeme!!!

This's totally cheap politics!
 
Sawa Mkuu nakuelewa sana. Kuna uzi mmoja humu nimekuCC utauona baada ya muda si mrefu.

Symbion Power yamkosoa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felchesmi Mramba

Ndugu Mramba hakusema sitisha kutoa umeme na hajawahi kufanya hivyo. Alisema kuwa alikuwa ameagizwa na Mheshimiwa Rais wa Tanzania; alisema katika mtazamo wake nyaraka za PPA zilikuwa sawia na faida za Kitaifa na alisema kuwa alimdhirishia hilo kwa kuzingatia na bei nafuu ambazo kampuni ya Symbion inauza umeme wake.

Kampuni ya Symbion ilichukulia kama utaratibu wa kawaida wa Serikali mpya kupitia mikataba yote ya Serikali kwa vile ilikuwa imetajwa kwenye baadhi ya ripoti za vyombo vya habari Vikimnukuu Waziri Mkuu kwamba Makubaliano mengi na Wawekezaji yanapitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuona kama zina maslahi ya Kitaifa. Hatukuwa hata mara moja kufikiria kuwa tutaweza kukumbana na jaribio la upande mmoja kusitisha mkataba miezi sita baadaye. Kama TANESCO ilikuwa ikifikira kuhusu hili na hawakuwahi kufikiria nyaraka za PPA kuwa na tija kwanini waliendelea kuchukua umeme wetu bure? Huu ni ukosefu wa Uaminifu kwa kiwango cha juu.

Tuko pamoja mkuu.

Ndiyo maana ilikuwa ni kosa kwa Mramba kuendeleza mazungmzo na Symbion wakati raisi na timu yake bado hawajapitia huu mkataba wa sasa.

Si unafanya kitu kimoja baada ya kingine au?
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia
God curse injinia! mtu mzima amesahau wahenga walisema "Ukimuona mwenzio ananyolewa, Wewe tia maji bichwa lako!"; Engineer Mramba should have borrowed a leaf from Dkt Mwele Malecela's book! Hii nchi kwa sasa sio ya kufuata sheria kama sheria per ce! lazima usome pia mazingira na alama za nyakati!
 
1. Yule jamaa hapokei cha juu hats siku moja
2. Ni mkweli na mcha Mungu.
3. Alikua anawazibia ulaji.
 
Naona kuna mabadiliko ya tune hivi sasa...

Tune ya sasa naona imekuwa "...hakufuata taratibu... hakuwashirikisha wale walio juu yake!"

Tune hii imeanza kusikika kwa Mwele Malecela!

Hebu nisaidie jambo moja! Hapa chini ni sehemu ya tangazo la EWURA juu ya nia ya TANESCO kupandisha bei ya umeme!
View attachment 453187

Tangazo ni la Octoba 04, 2016. Na kwa kumbukumbu zangu kupitia kipindi cha Kipima Joto ITV, hili suala lilijadiliwa na wadau! Hilo ni takwa kwa mujibu wa sheria za EWURA kama wanavyothibitisha wenyewe kwenye tangazo husika:

View attachment 453188

Now tell me: Unataka kuniambia wakato yote hayo yanafanyika wazi wazi bado serikali ilikuwa haifahamu nini kilikuwa kinaendelea? Kama ilikuwa haifahamu; kuna maana gani basi ya kuwa na serikali isiyofahamu hata kinachoendelea ndani ya taasisi zake?!

Au ni kwamba serikali ilikuwa inafahamu kilichokuwa kinaendelea lakini badala ya kuzuia from the beginning wakaamua kuacha kiendelee ili ipate justification za kutumbua?!

I am sorry to say kwamba Meneja bora hapimwi kutokana na uwezo wake wa kutimua wafanyakazi walio chini yake bali anapimwa kutokana na uwezo wake wa kuzuia crisis zinazoweza kusababisha kupoteza timu yake!

Ikiwa aina yenyewe ya uongozi ndio huu wa kuliana timing uharibu ili utumbuliwe basi nasikitika kusema kwamba for the time being, hii nchi ina uongozi mbovu ambao haujapata kutokea tangu tupate uhuru!

Huwezi kuacha watu wavunje sheria ili tu hatimae upate sababu ya kutumbua... this's totally administrative failure!

Kama hoja ni kwamba Mramba hakufuata taratibu; serikali walikuwa na uwezo wa kupiga stop kabla hata hao EWURA hawajapoteza raslimali kuitisha vikao!

Na kama ni kutumbuliwa; basi hao akina Mramba wangetumbuliwa baada ya serikali kupiga stop lakini wao wakaendelea! Tena wangetumbuliwa tangu mara baada ya kuitisha Mkutano ITV lakini inaonesha wazi serikali wasingekuwa na grounds za kufanya hivyo kwahiyo wakawaacha waendelee ili hatimae wapate cheap grounds zitakazo-sound kwa wananchi kwamba wamewatumbua kwa sababu wamepandisha bei ya umeme!!!

This's totally cheap politics!

Hapana, wewe ndiyo naona unaleta "cheap politics" katika maslahi ya taifa.

Umesoma EWURA Act na katika majukumu au "functions" zake kwenye issue ya majadiliano inasemaje?

Pitia tena halafu tuendelee.
 
It was staged na sarakasi nyingi na walijua tu watamfukuza. Umeme utapanda bei tuu, si tupo humu JF.

God bless you Injinia

Reasons za Muhongo umezisoma au unakurupuka tu?

Kama utapanda in future na upande kwa kufuata sheria na kanuni siyo kiholela tu.

Jamaa katumbuliwa.
 
Retired inaonekana wewe ni tanesco masalia. Iko wapi sympathy yako kwa umma? Nikikueleza kuwa wewe ndiye walewale ntakosea? Kama nakosea, niwie radhi.
Hata tunapoungama na kujuta dhambi, hujuta pia dhambi tulizozifanya kwa njia ya kuwaza!
Unapo-propose kitu kwa ajili ya utekelezaji, wewe uliyebuni huitwa "master mind". Na kadhia yoyote inayopatikana kutokana na mawazo yako hayo lazima uwajibikie.
Kwanini Mramba asilambwe?
Nimekuwia radhi. Wamemsikiliza? Unaleta siasa kwenye scientific issues. Mambo ya kuwaza dhambi ni ya revelations not realistic, they do not abide by scientific principles. Huyu ni mtaalamu, angelisikilizwa, akaambiwa hapana hatukubali bei hii! Yaani ku propose bei ni kosa? Think deep! Ichukulie sawa na Judge anavyotoa hukumu ikatenguliwa Court of appeal!
Kwa taarifa yako, siko Tanesco na ninaumia sana kwa bei ya Tanesco, but we have to follow laws, procedure and all rules before us for guidence
 
Siyo kwamba umeme hautoshi bali unafanywa uonekane hautoshi ili kampuni binafsi za kuzalisha umeme ziwe zinafanya biashara na tanesco kwa kutumia mgongo wa mtanzania wa kipato cha kati na cha chini.
Serously unaamini umeme unatosha? SERIOUSLY?

Ngoja nikuulize jambo moja japo kwa kutumia common sense! Ni asilimia ngapi ya wateja wa TANESCO wana uwezo wa kununua majiko ya umeme lakini hawathubutu kuyanunua na kutumia kwavile tu wanaogopa gharama za umeme?!

Hivi umeshawahi kujiuliza what will happen endapo only 10% ya wateja wa TANESCO hatimae wanaamua kutumia majiko ya umeme?! Do you really believe likitokea ongezeko kama hilo bado TANESCO watakuwa na ubavu wa ku-accommodate hiyo power demand? Hivi hapa napo unahitaji kuwa mchumi kufahamu kwamba, moja ya sababu ya kufanya bei ya umeme kubwa kubwa ni ku-discourage matumizi makubwa ya umeme?!
 
What is your point!
 
Umeongea point kubwa sana na kingine tu niongezee hawa "Viongozi" wanataka kuonyesha kwamba TANESCO imeshindwa kazi ili wapate mwanya wa kuanzisha makampuni yao ya kuzalisha na kusambaza umeme nchini na si ajabu hata nchi za jirani. Kwa maoni yangu TANESCO bado inaweza kabisa kusambaza umeme nchini bila ya kusaidiwa na kampuni yoyote ile, tatizo siasa na ufisadi wa kutisha umeingizwa TANESCO kwa zaidi ya miaka 20 sasa kuanzia awamu ya fisadi Mkapa na kuendelea hadi hii leo.

Tatizo hakuna ambaye yuko tayari kuifanyia kazi hii mikataba mbali mbali ya kifisadi ambayo inaiangamiza TANESCO. Wanaogopa "kufukua makaburi ya zamani" hivyo ni bora gharama za uzalishaji umeme kupitia mikataba ya kifisadi ziendelee kuielemea TANESCO lakini mikataba ya kifisadi hakuna aliye tayari kuigusa Mkuu.

Siyo kwamba umeme hautoshi bali unafanywa uonekane hautoshi ili kampuni binafsi za kuzalisha umeme ziwe zinafanya biashara na tanesco kwa kutumia mgongo wa mtanzania wa kipato cha kati na cha chini.
 
Hapana, wewe ndiyo naona unaleta "cheap politics" katika maslahi ya taifa.

Umesoma EWURA Act na katika majukumu au "functions" zake kwenye issue ya majadiliano inasemaje?

Pitia tena halafu tuendelee.
Jibu swali wewe... unataka kuniambia serikali haikuona hayo wakati yanaendelea au walikuwa wanasubiri matokeo ili hatimae wapate grounds za kutumbua? That's one but second; wakati nazungumzia Tangazo la EWURA nimekuwekea tangazo husika!!!

Hivi hudhani badala ya kunihoji functions za EWURA ulikuwa na wajibu wa kuweka hizo fuctions za EWURA? Ili kutoufanya mjadala huu kuwa mrefu;
1. Nijibu swali langu la msingi
2. Weka hapa hiyo sheria ya EWURA na functions zake!!

Or else; CHEAP POLITICS kama nilivyosema hapo awali!!!
 
nisha amin watanzania n wazembe sana wakufatilia mambo nyeti,kosa la huyo jamaa kufukuzwa kwanza n m2 wa kaskazn na ukoo wa akina mramba,pili katangaza bei ya umeme hazaran na hapo walikuwa wanamtafutia timing ya kumdisco,lkn pia alipaswa kupandisha bei ya umeme kimya2 kama ilivyopanda awali bila wananch kujua na ninajua wananch wa tanzania walivyokuwa wazembe hawajui mpaka leo bei ya umewe ilishapanda muda mrefu toka pale walipoondoa service charge ndo walipopgwa changa la macho watanzania!

Ili kuweka sawa leo h m2 wa kawaida nenda kanunue umeme wa buku 2 utajua kama bei ilishapanda au la ila kwa kuwa watanzania weng n mazezeta hlo hawatalikubali!

Umeme unit moja kwa sasa n tsh 400 na point kwa m2 anaenunua kwa matumiz ya kawaida hata kama hutakubalina na mimi.

Kilichofanyika ni kuwaingiza wachache kwenye huduma ya REA il kuuaminisha umma kuwa umeme kwa matumiz ya kawaida unit n tsh 100, lkn wanaolipa gharama h n wachache sana il weng wao wanapigwa unit moja kwa tsh 400.

Simu yangu 2 haipigi picha ningeweka hapa risiti!
unapowadhihaki watz ni mazezeta.....kwani wewe ni m'bangladesh..??...[emoji57] [emoji57]
 
Umeongea point kubwa sana na kingine tu niongezee hawa "Viongozi" wanataka kuonyesha kwamba TANESCO imeshindwa kazi ili wapate mwanya wa kuanzisha makampuni yao ya kuzalisha na kusambaza umeme nchini na si ajabu hata nchi za jirani. Kwa maoni yangu TANESCO bado inaweza kabisa kusambaza umeme nchini bila ya kusaidiwa na kampuni yoyote ile, tatizo siasa na ufisadi wa kutisha umeingizwa TANESCO kwa zaidi ya miaka 20 sasa kuanzia awamu ya fisadi Mkapa na kuendelea hadi hii leo.

Tatizo hakuna ambaye yuko tayari kuifanyia kazi hii mikataba mbali mbali ya kifisadi ambayo inaiangamiza TANESCO. Wanaogopa "kufukua makaburi ya zamani" hivyo ni bora gharama za uzalishaji umeme kupitia mikataba ya kifisadi ziendelee kuielemea TANESCO lakini mikataba ya kifisadi hakuna aliye tayari kuigusa Mkuu.

Ukitaka kufahamu aina tofauti ya makaburi anza kulitafuta lile liloandikwa IPTL 1994 initiation stage.
 
Tuanze na hilo gas... je, TANESCO nafasi yao ni ipi linapokuja suala la matumizi ya gas? Ni kwamba hawataki tu kutumia gas kwavile they're incompetent, au kivipi?

By the way, hivi unaamini kabisa kwamba as of now Tanzania tuna umeme wa kutosha? Hivi unaamini kabisa kwamba tuna surplus ya umeme?!

Unless you prove otherwise, ninachoamini na ndicho kilichopo ni kwamba bado tuna energy deficit. Kama ndivyo; hivi umeshajiuliza nini kinaweza kutokea endapo matumizi ya umeme yanaongezeka japo kwa 5%? And tell you what... umeme hautoshi wakati watu wanaogopa kutumia majiko na mabirika ya umeme! Ukitaka kugombana na wapangaji wenzako wakugundue kwamba unatumia jiko la umeme!!!

Be informed kwamba wakati mwingine bei inaongezwa just ku-balance matumizi ya umeme! Hata kama ulikuwa unatumia LUKU ya peke yako; bei ya umeme iki-shoot; wala hakuna atakayekuambia rudisha jiko lako la umeme store... wewe mwenyewe ndie utalipeleka store na kutafuta alternatives!

Kwahiyo bei haitapanda only if everything will remain constant or else; it's inevitable unless we want to play politics!!!
Umeme hautapanda kwasababu tunarudi kwenye "command economy" yaani a centrally planned economy! Ambapo bei zitapangwa na tume ya bei ya taifa kwa sababu tunatetea "wananchi wanyonge" walioumbwa kwa mfano wa Mungu!!
 
What is your point!
Ikiwa umeshindwa kuona hoja basi inathibiisha wazi kwamba hii mada kwako ni mzito or else unahitaji hoja nyepesi nyepesi ndipo unaweza kufahamu kilichomo kwenye hoja husika!!!!
 
Back
Top Bottom