Naona kuna mabadiliko ya tune hivi sasa...
Tune ya sasa naona imekuwa "...hakufuata taratibu... hakuwashirikisha wale walio juu yake!"
Tune hii imeanza kusikika kwa Mwele Malecela!
Hebu nisaidie jambo moja! Hapa chini ni sehemu ya tangazo la EWURA juu ya nia ya TANESCO kupandisha bei ya umeme!
View attachment 453187
Tangazo ni la Octoba 04, 2016. Na kwa kumbukumbu zangu kupitia kipindi cha Kipima Joto ITV, hili suala lilijadiliwa na wadau! Hilo ni takwa kwa mujibu wa sheria za EWURA kama wanavyothibitisha wenyewe kwenye tangazo husika:
View attachment 453188
Now tell me: Unataka kuniambia wakato yote hayo yanafanyika wazi wazi bado serikali ilikuwa haifahamu nini kilikuwa kinaendelea? Kama ilikuwa haifahamu; kuna maana gani basi ya kuwa na serikali isiyofahamu hata kinachoendelea ndani ya taasisi zake?!
Au ni kwamba serikali ilikuwa inafahamu kilichokuwa kinaendelea lakini badala ya kuzuia from the beginning wakaamua kuacha kiendelee ili ipate justification za kutumbua?!
I am sorry to say kwamba Meneja bora hapimwi kutokana na uwezo wake wa kutimua wafanyakazi walio chini yake bali anapimwa kutokana na uwezo wake wa kuzuia crisis zinazoweza kusababisha kupoteza timu yake!
Ikiwa aina yenyewe ya uongozi ndio huu wa kuliana timing uharibu ili utumbuliwe basi nasikitika kusema kwamba for the time being, hii nchi ina uongozi mbovu ambao haujapata kutokea tangu tupate uhuru!
Huwezi kuacha watu wavunje sheria ili tu hatimae upate sababu ya kutumbua... this's totally administrative failure!
Kama hoja ni kwamba Mramba hakufuata taratibu; serikali walikuwa na uwezo wa kupiga stop kabla hata hao EWURA hawajapoteza raslimali kuitisha vikao!
Na kama ni kutumbuliwa; basi hao akina Mramba wangetumbuliwa baada ya serikali kupiga stop lakini wao wakaendelea! Tena wangetumbuliwa tangu mara baada ya kuitisha Mkutano ITV lakini inaonesha wazi serikali wasingekuwa na grounds za kufanya hivyo kwahiyo wakawaacha waendelee ili hatimae wapate cheap grounds zitakazo-sound kwa wananchi kwamba wamewatumbua kwa sababu wamepandisha bei ya umeme!!!
This's totally cheap politics!