Nilivyo elewa Mimi ni kwamba, ukitaka au ukiona haja ya kumsifia mtu basi msifie kwa watu atafurahi na mtajenga mahusiano mazuri, ila yule unaetaka kujenganae uhusiano mwema lakini unataka kumkosoa jambo ili uhusiano wenu udumu ndo mkosoe sirini. Haina mana kuwa hana hiyo sifa ,ila msifie tu hadharani au mwingine anafanya jambo baya una mshautia mbele za watu, hamtajenga mahusiano mema kwani hata badilika kutokana na kiburi cha macho ya watu.
Lakini haya yote na kwampenda amani na staha. Mfano kumtumbua mtu mkutanoni, kumuumbua mtu asiye weza kujitetea. Ni bora umuite faraghani kama muungwana atajirekebish.
Ila hapa petu TZ imefikia sasa tusipo waeleza watu ubaya wa mtu hadharani, huyo mtu ataendekea kupotisha watu kwani anafanya kusudi unafiki. Huyo anastahili kusutwa hadharani.