Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Niliwahi kushauri humu, maadam JPM ameisha tangulia mbele ya haki, mwacheni baba wa watu apumzike, na kama ni kumkumbuka, tumkumbuke kwa mema!, huo ndio Uafrika, hatuwasemi vibaya marehemu wetu, wala hatuwakumbuki kwa ubaya.Raisi Magufuli tatizo lake mmoja hakuwa rafiki mzuri kwa wale watu ambao wamemjua kabla hata ya siasa.
mifano miwili
1. Kuna mtu ambaye yeye ndiye alimshauri Magufuli agombee kwa CCM, yeye ndiye aliyempa teksi ya kwanza kwenda kuchukuwa form ya kugombea miaka hiyo ya mkapa. Mzee yule ambaye alikuwa afisa wa Polisi huwezi kuamini mwaka 1996-1997 huyo huyo Magu ndiye alikuwa wa kwanza kumgomea kumuuzia nyumba aliyokuwa anakaa ya serikali obay wakati yeye mwenyewe alijiuzia nyumba. Huyu mzee hata baba mkwe wake yeye ndiye aliyempandisha cheo Polisi huko kanda ya ziwa!.
2. Charles Kitwana alikuwa rafiki wa kweli wa Magu kuanzia chuo kikuu lakini aliacha hata kumpigia simu baada ya kuwa Raisi!!
Famila sasa inajiuliza marafiki wapo wapi maana kuna marafiki fake walikuja baada ya kuwa Raisi lakini ni yeye ndiye aliwasahau marafiki wa kweli wa zamani. Haya ni mapungufu yake makubwa.
Somo ukipanda na watu watakuwepo pale usipo kuwepo lakini ukipanda mwenyewe utashuka mwenyewe
Mimi ni mmoja wa wana jf niliyemuandika sana JPM humu jf, mabandiko ni zaidi ya 100, Magufuli hakuwa malaika, ni binadamu kwenye binadamu hakuna mkamilifu, kuna mema ametenda na kuna mabaya amefanya, kwenye hukumu mema na mabaya yanapimwa kwenye mzani, mema yakizidi. Unaenda peponi, JPM mema yamezidi.
Mimi pia ni muumini wa karma, kutwaliwa kwake ni karma, ukisha hukumiwa kwa hukumu ya karma, dhambi zako zote zinafutwa, yanabaki mema yako tuu. The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!
Kwasasa JPM yuko mbinguni kwa Baba yake yuko na Baba yake Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
Mwacheni Baba wa watu apumzike!.
P