Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
TAZARA haina hali nzuri. Na sababu kubwa ni kwamba utegemezi wa Zambia kwa TAZARA umepungua sana. Kwa sasa Zambia inaweza kupitisha mizigo yao sehemu nyingine zaidi ya Dar es Salaam, kutia ndaniMsumbiji na Afrika Kusini. Lazima tuseme ukweli Wazambia kwa sasa hawana shida sana na TAZARA, japo wao ndio wanatoa Mkurugenzi Mkuu, kosa tulilofanya huko nyuma.
Sasa ili kuinusuru TAZARA, jambo kubwa la kufanya ni kuiunganisha na Malawi kupitia Mbeya pale au Tunduma. Ukifanya hivyo TAZARA itakuwa na umuhimu mkubwa kwa Malawi na kuipa uhai mpya!
Kwa upande wa Malawi, tayari wanafikiria kujenga reli kati ya Central Region na Northern Region, na tayari wana wazo la kuunganisha hiyo reli na TAZARA kama Tanzania watakubali. Kwa hiyo wazo kwa Malawi lipo ni suala la Magufuli kukubaliana na Raisi wa Malawi mradi huo uanze mara moja.
Malawi wanataka sana kuunganishwa na TAZARA kwa sababu ya mradi wao wa makaa ya mawe wa Mchenga Coal Mine sehemu inaitwa Rumphi, mradi wa miti na mbao pale Chikangawana pia uranium pale Kayelekera. Na pia tusisahau suala la mafuta Ziwa Nyasa, yanayoweza kutoa umuhimu wa pekee kwa TAZARA .
Tukikataa kuunganisha TAZARA na Malawi, Malawi wanafikiria kutafuta namna ya kutumia mito Shire na Zambezi ili kufikia Bahari ya Hindi, kwenye mradi utakaoitwa Shire-Zambezi Waterway (SZW). Wakifanya hivyo wataacha kabisa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Hivyo basi, ni vema Tanzania kuwafuata Malawi na kujadiliana nao juu ya kuunganisha reli zao na TAZARA
Tanzania inaweza pia kufikiria uwezekano wa kui-divert TAZARA ili ipitie Morogoro na Iringa mjini. Sijui tulitumia akili gani kuwakubalia Wachina wasipitishe TAZARA mjini kwenye mikoa hii. Ni gharama kubwa kufanya hivyo, lakini itakuwa investment itakayolipa sana tu, kama vile SGR!