TAZARA haina hali nzuri. Na sababu kubwa ni kwamba utegemezi wa Zambia kwa TAZARA umepungua sana. Kwa sasa Zambia inaweza kupitisha mizigo yao sehemu nyingine zaidi ya Dar es Salaam, kutia ndaniMsumbiji na Afrika Kusini. Lazima tuseme ukweli Wazambia kwa sasa hawana shida sana na TAZARA, japo wao ndio wanatoa Mkurugenzi Mkuu, kosa tulilofanya huko nyuma.
.......,
Tanzania inaweza pia kufikiria uwezekano wa kui-divert TAZARA ili ipitie Morogoro na Iringa mjini. Sijui tulitumia akili gani kuwakubalia Wachina wasipitishe TAZARA mjini kwenye mikoa hii. Ni gharama kubwa kufanya hivyo, lakini itakuwa investment itakayolipa sana tu, kama vile SGR!
Mimi nafikiri tatizo ni kuwa either
tumebanwa sana na mkataba wa TAZARA hivyo wafanya maamuzi ya kitaifa wanaona ni bora kuipotezea au,
wafanya /mfanya - maamuzi ya kitaifa hawana interest na TAZARA kwasasa / milele -> basi tusubiri atakaye kua na interest ( Waliopita nafikiri walitaka kuwarudishia Wachina) au,
tuna wafanya maamuzi ambao wako vizuri sana kichwani na kimikakati na hivyo kuna jambo jema kitaifa wanalipika linalohitaji kuipotezea TAZARA kwasasa, iliije kushghulikiwa ipasavyo baadae, au etc
Vinginevyo ningeshahuri;
1. Ndoa ya TAZARA ivunjike au irekebishwe kwa makubaliano ili TZ imiliki na kuendesha reli upande wa TZ na Zambia wafanye upande wao ili kila nchi iwajibike kwa matendo yake.
2. Then itengenezwe dry port inayofaa pale Tunduma ili mzigo unaenda au kupitia Zambia usogezwe hapo kutoka Dar port bila kuwepo any unnecessary delays. Treni au malori ya mizigo ya Zambia/Tanzania/DRC yatachukua mizigo kutoka hapo. Abiria wa Zambia-Dar vice versa wata transit hapo mpakani baada ya kupitia immigration.
3. Vituo vya treni upande wa TZ vikarabatiwe na makaumpuni ya ndani chini ya usimamizi makini. Watu wasiohusika wasiruhusiwe kuingia vituoni badala yake kuwe na sehemu za kupokea abiria nje ya vituo.
4. Mabehewa ya abiria yaboreshwe, na daraja la chini kabisa liwe la kukaa bila kuzidi idadi ya viti. wafanyakazi wa ndani ya treni wawe na ujuzi na tabia inayotakiwa kuhudumia abiria.
5. Kuwe na vituo vya kuuza ticket zaidi ya vile vilivyopo katka vituo vya treni. Utatatibu uwe ni wa anayekuja kwanza anapata huduma kwanza. Mfumo wa kuuzia ticket uweze kuhudumia wauzaji wa ticketi nchi nzima bila kuchanganya. Hivyo iwezekane kununua ticket kwa mifumo kama ya Mobile money na katika tovuti.
6. Huduma ya mzigo ya ndani ya nchi iboreshwe kwa kuhakikisha mizigo haipotei na haichakachuliwi. kuwe na maenoeo ya kuchuliwa (pickup) na kufikishwa (delivery) katika maeneo mbali mbali ya miji - isiwe tu katika vituo vya treni. Bei za usafirishaji wa mizigo ziwe rafiki - lengo liwe kutoa huduma endelevu (sustainable) na sio kutengeneza super profit. shirika linaweza kwenda mbele zaidi na kuweka mfumo wa tracking ya mizigo kwakutumi technology kama ya RFID au nyinginezo.
7. Waajiriwe wafanyakazi sahihi na Ratiba ya Treni ifwate wakati uliopangwa bila kukosa.
8. Naamini yakifayika marekebisho haya shirika litaanza kutengeneza pesa kuelekea kupata faida hivyo hata kulipia gharama za marekebisho haya wakati likiendelea kulipa mkopo kwa Wachina..
9. Ikianza kupatikana faida uanzishwe utaratibu wa Hisa ile sehemu ya kampuni imilikiwe na WATANZANIA binafsi wakati serikali ikishikiria kuwa majority share holder. Pesa zinazopatikana kutokana na uuzwaji wa share zitumike kimkakati ilikuongeza mapato zaidi ya kampuni.
10. Shirika liwe na utaratibu wa lazima wa ukarabati wa miuundo mbinu na treni zote bila kusubiri kuharibika. Shule ya msgundi wa treni Mbeya iboreshwe na ikiwezeka ishirikiiane na chuo cha Reli cha Tabora ilikutoa au kunoa wafanyakazi bora wa Shirika.
Mwisho, nilitegemea TAZARA na Reli ya Kati viwe ndio fundisho na/au chachu ya mradi wa Reli (SGR) mpya. Kwamba hapa tulikosea, turekebeshe ilituone matokeo au hapa tumefanya vizuri sasa tuongeze na kupanuka au tuwe wa kisasa zaidi. Lakini sijaliona hilo.
Je tumeshaelewa wapi tumekwama katika TAZARA na Reli ya kati? Je hatutarudia makosa?