Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana!

Pascal wataanza kukuelewa na mwisho watashindwa kukuvumilia, sio kwamba hawana akili kabisa. Anyway lugha ina utamu wake
 
Watu wanalalamika kua katiba imempa madaraka na nguvu kubwa sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Lakini husikii kelele kwenye kupinga sheria mbaya zinazompa DPP uwezo wa kumnyima mtu dhamana kwa kupeleka hati ya kiapo

Pia husikii kelele za kupinga sheria mbaya ambazo zinatoa mwanya wa kuweka watu mahabusu kusubiria kesi zao hata kwa miaka kumi, kesi ambazo hata mtu akikutwa na hatia adhabu yake hua ni kifungo gerezani kisichozidi miaka mitatu au mitano. Mpaka mtu yamfike ndio utaona anapiga kelele

Mzee Kitilya alipokua Kamishna Jenerali wa TRA mwaka 2010 alitokea kwenye vyombo vya habari wakati huo akiwa anasema kuna jamaa wamekamatwa wakihujumu mapato ya TRA na akasema hawapeleki polisi bali TAKUKURU maana wale jamaa hawana mchezo. Na kweli kina Dickson Mbetwa, Samuel Renju, Eric Rugeleka na Hagai Mwatonoka walikaa ndani zaidi ya miaka mitano huku kesi yao ikiunguruma hadi waliposhinda mwaka 2015

Miezi michache baada ya jamaa hao kua wameshinda kesi Harry Kitilya akakamatwa na kushtakiwa kwa kosa kama la wale aliowazungumzia 2010 kua wamefanya uhujumu wa uchumi na kama wale jamaa wangeendelea kukaa ndani kidogo wangekutana mahabusu na Bwaba Kitilya ambae sasa na yeye anakata miaka kwa sheria ileile aliyotumia kuwasulubu wengine

Tunaoneana kwa kauli za wenye mamlaka lakini pia tunaoneana kwa sheria zilizotungwa bila tafakuri ya kina au zilitungwa wakati fulani ili kuwakomoa watu fulani. Hatujui mtego wa panya huingia walokuwemo na wasokuwemo
Yah right. What goes around ... comes around.
 
Huwezi jua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had,
Yes indeed, the best one who ever attempted to assassinate Tundu Lissu! Au sijakuelewa kaka? Mimi imani yangu imenifundisha dhambi kama hiyo haisameheki!
 
Walio huru uraiani hawakumbuki wanaonyea ndoo mahabusu/gerezani.

Nimeona umevaa viatu vyao na kwa unyenyekevu mkubwa umemuomba baba mwenye nyumba awafikirie na afanye jambo kwa uliowataja kupitia DP.

Ombeni nanyi mtapewa, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa na tafuteni mtapata.

Andiko hili na liwe sala/dua kwa wote wanaotumikia kifungo.
Amina. Amina. Amina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo, kuna watu humu wana allergy kila rais Magufuli anapongezwa kwa mazuri yoyote au mafanikio yoyote. Ukimpongeza tuu rais Magufuli kwa lolote, utawasikia kuwa huku sii kupongeza bali ni kuusaka u-DC mara hizi ni njaa tuu za jina la Mayalla!!. Naomba kusisitiza kuwa mimi sina chama wala sisaki uteuzi, siku nikijiunga CCM, halafu bado nikakosa uteuzi, ndipo mtakuwa na haki kunituhumu kusaka uteuzi, lakini mtu asiye na chama kutuhumiwa kuusaka uteuzi, sio kumtendea haki!. Mimi siku zote ni mkweli daima, siegemei upande wowote, na nazidi kuusitiza ule wito wangu wa kwenye mazuri tupongeze, kwenye mapungufu tushauri na kwenye mabaya ndipo tukosoe, bandiko hili ni la pongezi.

As days goes by, this man is getting, better and better, he is changing for the better!.

Leo nimemsikiliza rais Magufuli akihutubia kutokea Ukerewe, kiukweli kabisa, nimekuwa very impressed!, haswa alipozungumzia, uzalendo, kuwa wakweli na kusisitiza maendeleo hayana vyama, akampongeza mbunge wa Ukerewe ambaye ni wa Chadema, na akatoa fursa kwa wana CCM wanaotaka kwenda upinzani, hakutokea mtu, akasema nikiuliza wapinzani wanaotaka kujiunga CCM, wengi watakuja, lakini siulizi kwa sababu huu sio mkutano wa CCM ni mkutano wa serikali!. This is good!.

Big up kwa rais wetu Magufuli kuanza kutenganisha shughuli za kiserikali na shughuli za chama. Kama tulimlaumu rais Magufuli kutumia state platforms kufanya siasa za CCM ikiwemo kupokea wanachama wapya, na leo amesema wazi, hatumii mikutano ya kiserikali kuigeuza ya CCM, ni jambo jema.

Kutumia shughuli za kiserikali kupokea wanachama wapya wa CCM was wrong. Katika bandiko hili,
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums nilisema

Sisi jf japo tunalaumiwa na kulaaniwa kwa ukosoaji kwa rais Magufuli na Serikali yake kila inapoboronga, lakini kiukweli kabisa, wanaomkosoa rais Magufuli ndio wanaomsaidia zaidi kubadilika, changing for the better, kuliko wanaomsifia!.

Naamimi lile tukio la kupokea wanachama pale uwanja wa Sheikh Amri Abed, wakati wa kamisheni maofisa wapya wa jeshi, ni sisi JF pekee ndio tulikipinga, na leo kimezaa matunda.

Nimenote kupungua kwa vikao vya CCM kwenye ikulu yetu, sasa vikao vya CCM, vinafanyikia CCM Lumumba!.

Huwezi kujua, huenda hata ule uvunjaji wa katiba kuzuia mikutano ya siasa, soon utasitishwa only if atabaini, it was not right, kwa sababu rais wetu hana mamlaka hayo aliodhani anayo!.

Mnaweza msiamini, anaweza kuamua kuifumua Tume ya Uchaguzi NEC na kuunda tume huru zaidi ambayo ni inclusive!, kama ameweza kumchukua Prof. Kitila, na yule mama wa ACT, atashindwa nini kuifumua NEC ili uchaguzi wa 2020, uwe uchaguzi huru na wa haki kiukweli kweli!.

Nimemuona akihutubia kwa humility na genuinity, hivyo mnaweza kushangaa akasimamia kuhakikisha ofisi ya DPP inatenda haki kweli na haki ikaonekana inatendeka, hivyo wote wanaoozea kwenye mahabusu za nchi hii wengine kwa zaidi ya miaka 7 kama wakili Medium Mwale, na wale wanaozea Keko, Ukonga, Segerea na mahabusu nyingine kama Harry Kitilya, Sioi Sumari, Shose Sinare, kina Isaack Kasanga, kina Gonzaga, kina James Rugemalila na wengine wengi, wanatendewa haki, na haki kuonekana inatendeka!. Kuna watu wanaoshitakiwa kwa makosa ambayo ukikutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini mtu yuko mahabusu mwaka wa 7 sasa na kesi haijaanza kusikilizwa!, huu ni uchunguzi gani ambao haukamiliki, na hii ni haki ya aina gani?!.

Huwezi jua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had, na sisi Watanzania katika umoja wetu, tukamlilia aendelee na kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza katiba ibadilishwe, kipengele cha ukomo kieondolewe!.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up!.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!.
Paskali.
Rejea
Rais Magufuli Akifanya Mazuri, Apongezwe: Hotuba Yake Kuzima Mwenge, Ni One of The Best! - JamiiForums
Tusilalamike Tuu, Kulaumu na Kulaani Kila Kitu, Kwenye Mazuri Tupongeze, Rais Magufuli is Changing For The Better!. - JamiiForums
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!. - JamiiForums
kichaa chako kinafanana na changu CHAPA KAZI ila hakuna uteuzi
 
getting better kwa kuwalinda wakwepa kodi? Makonda na kind lake
 
Pascal nimekuelewa sana. Wewe ni philosophical figure. Nilikuwa nataka kuharubu na kiments kadhaa ila nikabaini busara ndani ya huu uzi. Nami nijifanye mwanafalsafa kidogo. Tutegemee mema. Rais anaanza kutambua sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sarcasm at its best............mumuelewe vizuri Pachal na aina ya uwasilishaji wake ili anendelee kuandika bila kukwaruzana na mamlaka.
Kazi nzuri bro
 
KILA SIKU MAANDIKO YAKO NI YA KUSIFU MAGUFULI TANGU UTOKE KUHOJIWA BUNGENI. MKUU WEWE NA TUMBO LAKO NA YA WATOTO WAKO MBAKI NAYO...TANZNAIA NI NCHI...OF COURSE SIO KILA MTU LAZIMA AWE MWANDISHI..ILA USITUMIKE KUPOTOSHA UMMA. RUBBISH KABISA...NILIKUWA NAKUHESHIMU SNAA
 
Kwani kutokuwa na chama kunazuia ww kusaka uteuzi au mteuwaji kutokukuteuwa na hasa ikitokea ww una viwango vya juu vya unafiki au kujitoa fahamu na kusifu kila kitu ata ujinga. Utateuliwa tu. TATIZO BW KAKA PASKALI WW NI VUGUVUGU, SI MOTO SI BARIDI. Na kwa siasa za kibongo lazima watu watake kujua umesimamia wapi, ww ni mwenzetu au si mwenzetu. ILA SIKU UKICHUKUA UPANDE UTASHIBISHWA ILA UTAPATA TABU SANA. Kwa sababu utakua na option mbili tu kukosoa tu au kujitoa fahamu na kushangilia kila kitu. Hakika utapata tabu japo sijui viwango vyako vya unafiki. Hahahaaa...
 
Back
Top Bottom