Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

CWR2016

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
2,773
Reaction score
6,349
Salaam wana JF...

Jana tarehe 04.09.2020 nikiwa nimetulia sehemu nilibahatika kufungulia TBC1 na kukuta kampeni za Dkt. Magufuli akiwa mkoani Mara.

Muda wa alasiri, alikuwa Bunda, badae akapita na kusimama Kiabakari, ni eneo la mnada wilayani Butiama.
Leo najua atakuwa na mkutano Musoma mjini.

Mambo niliyoshangaa kwa Dkt. Magufuli:-

1. Aliwaambia wananchi wa Bunda kwamba hakuwafanyia maendeleo yoyote, kwa sababu wao walichagua upinzani.

-Akawauliza "nyinyi hamjiulizi mko karibu na Ziwa lakini hamna maji?"
-Akawauliza "hamuoni wenzenu Lamadi (mpakani mwa Bunda, jimbo Busega) wana taa za barabarani, nyie hamna?!"
- Akawaambia, hata barabara nimeendeleza zinazowazunguka hapa nikawaruka.

Mwisho akaishia kuwaambia mnichagulie mbunge wa CCM, na madiwani wa CCM.

Nilishangaa hakueleza zaidi atawafanyia nn, ila aliwaahidi kuwa mkinichagulia mbunge wa CCM nitakuja kuwashukuru, na siku hiyo ndio ntakuja na mipango yote kuibadilisha Bunda.

Akawasisitiza wasichague maupinzani tena.

ETI HAWEZI KUACHA MTOTO WAKE, AKAMHUDUMIA WA JIRANI.

Nampa pole Dkt. Magufuli kwa haya na timu yake ya kampeni.

Inaelekea hajui vizuri watu wa Mara (hasa eneo la Bunda).

-Moja, sio watu wa kutishiwa vitu kabisa. Pole Dkt. Magufuli

Kwa hili, Bunda umepoteza.
Wale wamezoea kuishi na upinzani tangu Nyerere akiwa hai.

Unamtishia mwana Bunda (Mwikizu, Msizaki, Mzanaki, Mkurya, n.k) vitu?!!!! Eti ndio akuchague?

UME FAIL....

Hawakuchagui, watasema baki na taa zako za barabarani.

Wale ni kina LadyJaydee hawatishwi na hawapigi magoti.

Sijui huko usukumani labda wanapiga magoti.

- Mbili,
Ni uongo mkubwa kwamba Bunda haina maendeleo kisa kuwa upinzani.

Nikuulize leo upo Musoma mjini, ambayo ipo CCM awamu hii yako ya kwanza;

Mbona Musoma mjini imefubaa kuliko Bunda?, mji umepotea na biashara haziendi mpaka watu wameukimbia?! Mbona huko yupo mbunge wa CCM?

Haya BUTIAMA je?

Mbona siku zote wapo CCM. Tena wanapitaga bila kupingwa. Mbona BUTIAMA imechoka sana.

- BUTIAMA haina maji, lakini ipo CCM.
Mbunge CCM, Madiwani CCM.

- BUTIAMA kampuni yako ya Mayanga imeshindwa kujenga Barabara ya Butiama - Serengeti, na hela walilipwa, Mradi wa kumalizika 2015, mpaka leo umekufa.

Mbunge CCM, Madiwani CCM.

- BUTIAMA haina hospital ya maana, Haina sekondari ya maana, Haina soko la maana.

Mbunge CCM, Madiwani CCM.

ACHA HADAA, HAKUNA CHA CCM.

-HALAFU UNAJIITA KABISA RAIS WA MAENEO YA CCM TU.!!

2. AKIWA KIABAKARI.
Akiwa hapa alisema tatizo kubwa la Jimbo la BUTIAMA, ni ukabila.

Aisee you're very WRONG.

Butiama haina ukabila kabisa.
Ndio maana hata ulivyosema hivyo niliona kila mtu ananyamaza.

Sijui ulimaanishi nini. Ila umedanganywa pakubwa, matatizo ya BUTIAMA ni mengine kabisa.

Nakuhurumia sana.

Halafu mu MSHAURI JPM AACHE KUTISHA WAPIGA KURA kwamba hatawafanyia maendeleo kwa vile wanachagua upinzani.

Ni uongo mkubwa...

Haya ni majimbo ambayo yapo CCM, lakini ni maskini vibaya sana..

1. BUTIAMA
2. BUKOMBE
3. BUSEGA
4. MANYONI
5. MUSOMA VIJIJINI
6. KIBITI
7. RUFIJI
8. MKURANGA
9. MVOMERO
10. UKONGA
11. KAKONKO
12. MAGU
13. IRAMBA
14. MAKETE
15. NEWALA
16. MTAMA
17. KIVUU
18. SUMBAWANGA
19. NZEGA KASKAZINI
20. NZEGA KUSINI
21. SENGEREMA
22. CHATO
23. LONGIDO
24...........

Mwana JF...

Taja MAJIMBO mengine yaliyopo CCM lakini ni maskini vibaya mno...

Comment hapa Chini.....
 
Weka hapo Jimbo la Kongwa kule Dodoma kwa spika
Usisahau kwa Joseph musukuma Kule Geita vijijini. Hakuna barabara, shule watoto wanasomea chini, hakuna maji na ziwa Victoria limewazunguka, vijiji vya Nyamikoma, Kamwanga na Lwenge huku Geita vijiji hakuna maji, hakuna umeme, hakuna vituo vya afya, hakuna masoko, hakuna shule za msingi Wala sekondari na hakuna barabara hata ya moramu ya kupitisha gari. kule ni shida 100% . Alipata ubunge anasema yeye ni darasa la 7. Yule ni sawa na mganga wa kienyeji. Tunaomba Magufuli akifika Geita atembelee vijiji hivi ajionee maajabu ya dunia. Cha ajabu kabisa vijiji hivi vinazungukwa na mgodi mkubwa duniani, Geita gold mine, unaozalisha dhahabu Ila hauna msaada wote kwa wananchi wanauzunguka mgodi huo.
 
TBC ya nchi gani hiyo uloangalia hizo Kampeni? Au na wewe ni walewale Tia maji Tia maji
 
Halafu anasema maendeleo hayana vyama!Sasa tumueleweje?
Tunaomba Tindu Lisu akifika geita atembelee wilaya za Nyangwale, Bukombe, Mbongwe na Geita vijijini. Akiwa Geita vijiji atembelee vijiji vya Nyamikoma, Lwenge na Kamwanga atapata kura zote kabisa. Wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa. Kuna uwezekana hata magari ya VX V8 hayataweza kufikia hivyo vijiji na viko nchi kavu hakuna barabara kabisa. TL karibu mkoa wa Geita
 
Wiki juzi nilipita Butiama kwa kweli hauwezi amini kwamba ndiyo nyumbani kwa mhasisi wa Tanzania. Tatizo lingine kwa Butiama (limethibitishwa na wenyeji bila shaka yoyote) ni kwamba mkurugenzi wa halmashauri ya Butiama kashatengeneza makundi miongoni mwa watumishi hivyo kupelekea kazi kutofanyika. Kiufupi nilichongundua halmashauri ya Butiama ilishakufa.
 
Back
Top Bottom