Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

Yaani kama alisema hayo maneno ikiwa kama sehemu ya kampeni kakosea sana. Alafu ni kama vile yeye ameshapita (uwakika, imeshapangwa kuwa ataendelea)🤔
Tunapoelekea zitahitajika busara za hali ya juu sana kuweka mambo sawa.
 
Lupa
 
Halafu bila aibu linasema Maendeleo hayana vyama
 
Haya bwana na kibao chao. Nimekuelewa lakini Nungunungu na miba zake bado wachumba wanamjia na mimba wanamdunga.

Watakaomtia mimba ni nungunungu wenzake. Wanajua staili zao. Peleka mkuyenge wako uone utavyochanwa! Hivyo, ukienda Roma jifanye Mrumi. Ni busara za kawaida. Magu hakujua hekima hii. Kaingia Mara kichwakichwa na kuwafedhehesha watu wa Bunda akidhani watafehedheka kumbe yamekuwa kinyume.
 
Jimbo la morogoro vijijini kuanzia ngerengere mpaka mkulazi mvua ikinyesha hakupitiki tena, mbunge na madiwani wote ni ccm tangu nchi hii ipate uhuru.
Jimbo la kipuuzi sana.
Kuanzia Kidugalo mpaka Kidunda na maeneo ya jirani, jimbo linanuka umasikini uliokithiri ingawa wana ardhi nzuri yenye rutuba na wamezunguukwa na pori la akiba la Selous.
CCM kila baada ya miaka mitano wanabadirisha mbunge lakini hakuna hata mmoja anayekerwa na umasikini wa kutisha uliopo eneo hilo.
 
Nimependa sana ujengaji hoja wako. Wakikujibu nitag.
Ukweli ndio huo uchumi labda ni wa watu wa Chato tu.
 
Ina maana Morogoro pamoja na kuwa na ardhi oevu sana, bado ni maskini?

Si wapo chini ya CCM miaka yote?
 
Watanzania tusifanya makosa kumrudisha mtu wa namna hii anasema kila siku maendeleo hayana chama wakati amenyima maendeleo Mara, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Kigoma kisa upinzani. Hafai kabisa.
 
Watanzania tusifanya makosa kumrudisha mtu wa namna hii anasema kila siku maendeleo hayana chama wakati amenyima maendeleo Mara, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Kigoma kisa upinzani. Hafai kabisa.
Mtwara huko na Lindi aliowanyang'anya korosho...

Wamemkosea nini...

Watu wameshindwa kupata hela ya kusomesha wanao chuo, na sekondari. Kisa korosho zimechukuliwa na jeshi.

Watu wakaishiwa kuambiwa korosho zao zilikuwa mbovu.
 
Uyo maboto hapati kitu hapa bunda kwanza watumishi hawatiki kumsikia, kampuni yake ya mikopo imeumiza sana watumishi
Kumbe Maboto ana kikampuni cha mikopo?

Kawafilisi watu, au?
 
Barabara ya kutoka Bunda hadi Kisorya haijakamilika kwa kipindi kirefu sana. Hiyo Barabara inapita katika majimbo ya Bunda, na Mwibara. Kwa mtizamo huu Barabara hiyo itakamilika huko Mwibara lakini kule Bunda hadi hapo watakapowachagua wale. Ama kweli maendeleo hayana chama.
 
Huu uzi huwezi kuwaona akina bia yangu..wakudadavua .. mgonjwa mtambuka..Mama ntilie wa kawe .. Pascal mayala ..sumve yao..mtashobya ..kipara kipya na USSR ...wanapita juu kwa juu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Labda hawajauona, ni vizuri tuwe tunawataarifu kwamba kuna mada inahitaji mchango wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…