Elections 2015 Magufuli lugha za Kimataifa ni Kizungumkuti, wenye ufahamu tujadiliane

Hehehe mkuu unamlinganisha akili MaPadlock na EL, acha basi utani, EL hajakaribia IQ ya MaPadlock hata kidogo..

Hata miongoni mwa wasomi wa maigizo wenye uwezo wa kiakili Arusha (sio tz nzima) hawezi kuingia hata kwenye 100 bora. Huyo mshindanishe kwenye wapiga dili kwa vyeo vyao serikalini humkamati.
 
Nikimkumbukaga deputy minister Mulugo, huwa nabaki nacheka saaana!
 

Lugha inaweza kuwa kipimo sahihi cha uelewa. Haiwezekani mtu aliyesoma kwa kutumia lugha ya kiingereza toka primary school mpaka PhD leo hii lugha hiyo inampa shida. Kumpa Urais mtu asiye na exposure itatucost!!
 
Tunatafuta Rais wa Tanzania sio wa Kimataifa.
 
Tunatafuta Rais wa Tanzania sio wa Kimataifa.

Tunatafuta rais wa tz atakayetuwakilisha kimataifa pia. Magufuli ni zero kabisa. 40% ya bajeti yetu inategemea wenye lugha tofauti na kiswahili
 
Lugha inaweza kuwa kipimo sahihi cha uelewa. Haiwezekani mtu aliyesoma kwa kutumia lugha ya kiingereza toka primary school mpaka PhD leo hii lugha hiyo inampa shida. Kumpa Urais mtu asiye na exposure itatucost!!

Ni nani alikudanganya kuwa Magufuli "lugha hiyo" inampiga chenga?

Lowassa hana ujanja kwa Magufuli, Lowassa ana ujanja kwa wachagga tu na ujanja wake ni mdogo sana, pesa.
 
Unadhani ukiwa na PhD ndio una IQ kubwa? Vyeti na uwezo wa mtu kufikiri ni mambo mawili tofauti

Moja ya njia ya kuelewa mtu mwenye IQ kubwa ni kuweza kuongea (japo kwa kusalimiana) kwa lugha zisizopumnguwa 7.

Magufuli anayaweza hayo kwa lugha zaidi ya 20.

Isitoshe, Magufuli ana photographic memory, hiyo ni moja ya kukuelewesha kuwa ana IQ kubwa sana.

Hilo halina ubishi, tumemuona uwezo wake.

Vipi Lowassa IQ yake? Maana anasahau hata jina la mkewe.!
 



si kweli lazima completely ujue standard english ndo uwe na sifa ya kuwa rais {ENGLISH SI LUGHA YETU}, vip kuhusu wakalimani.....?

rais wa china yeye anapofanya ziara nje ya nchi utembea na wakalimani wake kwa nin rais wa tz iwe ni tatizo kama atafanya hivyo?.

huu ndo ULOFA WENYEWE.
 
Eti alisomea uingereza. Sijawahi kumsikia akitema yai na siku akitema yai litakuwa yau viza
 

Hivi Lowassa anao uwezo wa kuongea lugha ngapi za makabila ya Tz? make kama mwana sayansi anao uwezo wa kuclaim kuliko mwana sanaa basi huyu mwana sayansi ni bora zaidi ..Magufuri anastahili sifa zake
 
Lowassa anajua kuspik english vzr sana kuliko kiswahili. Huyu mwenzetu wa chato alikimbilia ualimu sjui kama ataweza kuomba hata maji akiwa usa
 
Kama karatasi tu anaita "RIKARATASI" unategemea nini...
 
Hiv rais wa china anajua hata english kweli?... mi nadhqn hiyo siyo ushu hasa kwa wazalendo...labda kuwe na sababu nyingine.....hasa yenye mashiko

China Taifa huru lililoendelea huwezi linganisha na hili Taifa lisilo na mbele wala nyuma
 

Msitake kujifanya manyani kwamba hamjui umuhimu Wa kingereza na kuishia kujifananisha na mchina au mjerumani au mfaransa ,pamoja na kuheshimu lugha zao ila nao wanaweka jitihada za wazi za kujifunza Kingereza
 
SEMINARI husifika kwa elimu bora Tz na huyu unayemsema hajui lugha ndo alisoma katoke miaka ya 70's.
Tupunguze ushabiki unless kama uko na speech ya JPM ya muingeleza uiweke apa ili tukosoe lugha but si kwa neno Fulani kutamkwa sivyo useme hajui lugha.
Pia kama mwalimu wa chemistry na maths matumizi ya lugha ni adimu.
Hope ata thesis yake ulimwandikia wewe.
Acheni dharau zisizo na tija mambo ya FB acheni kule kule FB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…