sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Kwanza nataka niwaambie watoto mliovamia siasa kaeni mjifunze kuhusu nchi yetu ya Tanzania muielewe vizuri. Shida kubwa ya vijana walio na mzuka na siasa hawajui kabisa kuhusu nchi wala game ya siasa inavyokwenda duniani kote. Kubwa zaidi hawaijui dunia.
Niende moja kwa moja kwenye hoja sasa. Mungu alituletea Magufuli ambae kwangu mimi ndio the best president kutokea na uhenda asitokee kama yeye kwenye taifa letu.
Kwa nini kwangu ni the best ever?
Ndio Rais aliyejaribu kuubadili mfumo wetu wa nchi.
Ndio Rais aliyethubutu kugusa maeneo ambayo kinadhalia tuliamini yakiguswa basi tutapata ahueni kwenye maendeleo ya nchi yetu.
Ndio rais alikuwa anauchungu na raslimali za nchi yetu na alifanya lolote analoweza kuzilinda.
Ndio Rais aliyesimama na tabaka la watu wa chini (wanyonge) kwa vitendo.
Mungu ampe mapumziko mema huko alipo.
Pamoja na jitihada na kujitoa kwake, japo alifanya mengi kwa kipindi kifupi lakini bado yalikuwa hayatoshi. Sisi tunaona ni mengi tukilinganisha na Marais waliomtangulia ila kama nchi bado tuliitaji zaidi ili tutembee kifua mbele tukisema sasa tunauaga umaskini.
Kwa nini ni ngumu sisi kupata Rais wa kututoa hapa tulipo hatimaye tupige hatua kubwa za kimaendeleo?
Au niseme kiufupi kwa nini tutaendelea kuwa maskini kwa vizazi vingi vijavyo?!
Kwanza sisi ni maskini wa kiasili, umaskini wetu ni sehemu ya utamaduni wetu kwa hiyo ili tuondoe umaskini lazima tuachane na tamaduni zetu. Je, tutaweza? Haiwezekani.
Pili, maendeleo ni mchakato wa taratibu sana. Lazima tukubali kujipa miaka at least 150 tangia uhuru ili tufikie level tunazoota za maendeleo. Nchi zote zilizoendekea zina historia na maendeleo. Maendeleo hawakuyaanza juzi wana miaka mamia kwa maelfu kwenye safari yao ya maendeleo. Wenzetu walianza kujenga majumba vizazi vya kina Yesu (sisi tukiishi juu ya miti)...walikuwa wanaandika vitabu na mfumo wa elimu miaka ya kina Musa...wanatembea kwa meli enzi za kina Nuhu...wewe from nowhere unataka uwafikie haiwezekani.
Tatu, maendeleo ni maumivu. Hakuna njia rahisi kwenye kuyasaka maendeleo. Nchi zote duniani zenye maendeleo makubwa zimepitia maumivu ikiwemo vita, vifo, uporaji, sadaka nk. Sisi tunadangayana maendeleo yetu yataletwa na katiba nzuri au demokrasia, HOW??!!! ni uongo tumepigwa.
Nne, hatuna raslimali za kiasi hicho tunachoaminishana. Kuna nchi zimebarikiwa raw materials ndio maana mzungu alipita tu hapa akaenda America huko mpka Australia sababu hakuona cha maana kwetu. Hata raslimali tulizonazo ili kuzibadili ziwe utajiri unahitaji pesa. Una gesi mtwara uwekezaji wake unataka trillion 80 wewe makusanyo yako kwa mwezi ni trillion 2 hapo ukivunja rekodi hiyo hiyo upeleke kwenye huduma muhimu, uhendeshaji wa serikali, maendeleo nk. Kwa hiyo hatujiwezi kabisa.
Mwisho, maendeleo yanahitaji kiongozi mwenye vision na apewe muda mrefu. Magufuli alikuwa na vision kubwa japo kuna watu hawakuwa wakimwelewa na walimchukulia poa. Kiongozi mwenye vision aachwe atawale kwa muda mrefu sio huu uongo wetu wa mihula miwili. Ni taifa gani duniani lilipata maendeleo kwa kuwa na kiongozi aliyetawala miaka 10? Hakuna, huu ni mfumo wa ajabu na utaendelea kutuzamisha kwenye umaskini.
Kwa hiyo nachotaka kuwaambia mashabiki wa siasa. Maendeleo ni mchakato na ni mchakato unahoitaji pesa za kutosha.
Vyanzo vyetu vya mapato vinafahamika na havibadiliki sana sio kwa sababu hatuna watu wabunifu no ni sababu sisi ni maskini mno tukiongeza wigo wa mapato tutalia kilio kikubwa sana na inaweza kutokea crisis (mfano tozo). Kwa hiyo the easy way ni kukopa tu.
Hakuna kiongozi wa kizazi hiki anaweza kufanya miujiza kama wanavyohubiri kwenye majukwaa. Miujiza yote alijaribu Magufuli hakubakisha kitu.
Akitokea mwanasiasa anasema tupeni nchi tuwaonyeshe tutavyobadilisha mambo. Muulizeni hela mtatoa wapi za kufanya hayo maajabu?
Kama ni mpinzani muulize kwenye bajeti zenu mbadala mliokuwa mnawasilisha bungeni mbona zilifanana kila kitu na serikali? Vyanzo vyenu vya mapato vya kuwa na bajeti ya trillion 60 kwa mwaka zitatoka wapi?
So guys, lets chill tule maisha mdogo mdogo tusijpe stress. Magufuli alimaliza kila kitu haya mengine ni porojo tu za wanasiasa kujaribu nao wapate ugali.