Magufuli ni Rais muoga haijawahi tokea katika nchi hii

Magufuli ni Rais muoga haijawahi tokea katika nchi hii

Ashasembeko

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
225
Reaction score
910
Ninaandika ujumbe huu kwa huzuni sana kwasababu kati ya viongozi ambao nilikuwa ninaamini genuinely wangeweza kuleta mageuzi katika nchi hii Magufuli alikua namba moja.

Nilikua shabiki yake toka alipokua Waziri wa Ujenzi na hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais bado nilimpenda kwa dhati. Ni kiongozi ambae amenifanya niwe na keen interest na maswala ya kisiasa.

Jana nilipatwa na hasira nilipoona kwenye habari kuwa Bunge limepitisha Muswada kandamizi wa vyama vya siasa. Haiitaji rocket science kujua kwamba ule Muswada umeandaliwa kwa dhumuni kubwa la kudhibiti vyama vya upinzani. Hapa ndipo nilidraw the line na kugundua kuwa Magufuli si kiongozi mzuri kama nilivyomdhani.

Nilijiuliza swali la msingi; Kwanini huyu Rais anatumia nguvu nyingi kunyamazisha dissenting voices? Ni kweli kwamba kwenye siasa kuna propaganda, uzushi na uongo mwingi sana lakini hiki hakipaswi kuwa chanzo cha Serikali ya Magufuli kuweweseka.

Utawala wa Mhe. Kikwete, wapinzani walishamiri na kupinga masuala mbalimbali katika Serikali lakini hatukuona utawala wa Kikwete unatumia resources nyingi kucrackdown wapinzani. Si muwaache waongee, kwani ni lazima wasikilizwe.

Hii inadhihirisha kuna mambo mengi yanafichwa ndani ya Serikali ya Magufuli maana haileti maana wewe kuzuia watu wenye mawazo tofauti na yako kuongea.

If anything, this proves that Magufuli ni kiongozi insecure sana. Wapinzani walimsema Kikwete kwamba ni kiongozi dhaifu, ila ukweli mchungu ni kwamba Magufuli ni dhaifu zaidi. Utaona kwa jinsi tu anavyotumia nguvu nyingi katika ulinzi wake. He is the most protected President in our country's history. Amemwaga sana hela kwenye Usalama wa Taifa kwa ajili tu ya ulinzi wake. 80% ya staff wa TISS wamebadilishwa katika uongozi wake na anaweka vijana wadogowadogo wasio na experience wala mafunzo ya kutosha, mwishowe wanaishia kuteka na kutisha watu.

Kwa wakazi wa Kijitonyama wataelewa ni kwa namna gani wanashuhudia miili ya watu iliyotupwa kwenye viroba kila kukicha.

Tusipokuwa makini na kutafuta mbinu za kumdhibiti huyu Rais ambaye anajiiona ni invicible, itakuja kutucost when it is too late.

Najua anatabia ya kusema "pesa zipo" ila Serikali sasa hivi haina pesa. Development partners are pulling out aid and funding of projects kwa sababu ya sheria kandamizi na ukiukwaji wa haki.

Ni kwa sababu hii huoni sikuhizi kwenye speech zake akiwasema vibaya hawa wahisani maana wamemshika pabaya. The government is really broke na hizi sheria kandamizi zinazoendelea kutungwa haziisaidii nchi kabisa.

My advice to the President:

Ulianza vizuri sana mwaka wa kwanza na nusu ya uongozi wako, you were the model of good African leadership and everyone was in love with you. Sijui ni nini kilitokea baada ya hapo sababu wewe ni Kiongozi ambae ungeweza kuwa zaidi ya Nyerere but you ruined it.

Mimi nakushauri uwaachie watu wazungumze bila kuwaekea vikwazo, sio lazima uwasikilize. Huwezi kuongoza kwa kujenga mazingira ya hofu, hata mawaziri wako wanakuogopa.

Umekuwa Waziri wa kila wizara, they cant make decisions sababu wanaogopa jinsi ulivyo unpredictable. Wewe na mpwa wako mmejimilikisha hazina ya nchi, yule Waziri mpango yupo pale kama pambo, hana nguvu kabisa.

Hii nchi ni yetu sote, tuvumiliane. Angalia mfano wa mwezako wa Ethiopia, hata rafiki yako Kagame ameanza badilika. Its the 21st century, the age of the internet, huwezi kuongoza with an iron fist na ukawa successful ipo siku itakucost.

All the best katika majukumu yako!!
 
Naona unapiga mayowe yasiyoeleweka.

Inawezekana hata sheria ya vyama vingi iliyopitishwa hujaisoma lakini unakimbilia Jamiiforums kuja kupiga kelele ambazo hazieleweki badala ya kutumia muda wako kuisoma hiyo sheria.

Hujui kama sheria hii imebadilishwa mara sita tokea mwaka 1992 na sasa inakuwa ni mara ya saba kufanyiwa marekebisho.

Kama Rais ni dhaifu zaidi ya Kikwete, kwa nini sasa unalalamika?

Nani alikuambia Rais ndiye anaweka ulinzi wake?
 
Hakuanza vizuri,yale yalikuwa maigizo.Tatizo la wabongo wengi ni kushindwa kuwasoma wanasiasa na sitashangaa wewe ulichagua hata mbunge wa CCM in case ulipiga kura.
Hayakua maigizo... maana hiyo ndio ilikua his style of leadership toka alivokuwa waziri wa ujenzi....
 
Naona unapiga mayowe yasiyoeleweka.

Inawezekana hata sheria ya vyama vingi iliyopitishwa hujaisoma lakini unakimbilia Jamiiforums kuja kupiga kelele ambazo hazieleweki badala ya kutumia muda wako kuisoma hiyo sheria.

Kama Rais ni dhaifu zaidi ya Kikwete, kwa nini sasa unalalamika?

Nani alikuambia Rais ndiye anaweka ulinzi wake?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Nimeisoma vizuri sana, act baada ya act.... na kama na ww umeisma vizuri na bado unaiona ipo sawa basi ww ndio una matatizo
 
Mkuu umetoa ukweli mchungu sana!

Huko PM usikubali kumpa mtu namba yako ya simu,wala usikae u-reveal your identity to anyone humu!

Pia kuna watu watajifanya mademu watakufuata kua wanakupenda wataomba mawasiliano yako,usitoe kabisa!

Na pia,usijibu even their PMs.

Ignore them 100%!

Serikali oga sana hii,watajifanya wanatumia honey pot kukutafuta,they are stupid to the core!
 
Ashasembeko umeandika kwa hisia sana, ila tunakoelekea Mungu ndio anajua, kwanza Jeshi, puli bunge na juzi tumehitimisha na juma wa mahakama tunamaliza na msajili then tunapeleka muswada wa kuongeza muda wa urahisi , tunaondoa ukomo maana sioni kama kuna mtu atakuja kuziweza changamoto zilizopo

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi... this looks like a well choreographed and coordinated strategy
 
Hayakua maigizo... maana hiyo ndio ilikua his style of leadership toka alivokuwa waziri wa ujenzi....

Yah alianza kwa style kama alivyokuwa waziri baadae sana akagundua kuwa URAIS ni gemu tofauti na UWAZIRI akaamua kuachana na ile style ya uwaziri waziri!. Lakini kwa bahati mbaya jamaa hana KIASI yeye anajua ncha mbili tu ya ON and OFF, JUU na CHINI hana MIDDLE GROUND
 
Nimesoma, andiko hili, nimechanganya na speech ya jana ya Zitto Kabwe, nimerudi kwenye andiko la (dada wa Taifa) joke Mange kimambi.................nimechanganya ziara ya Tundu Lissu. Nasononeka sana najaribu kuwaza nani anamdanganya, narudi tena najiuliza why Mkapa, Kikwete na Mzee Mwinyi wako kimya? Anyway all in all tuzidi kutafakari, huenda Mungu anatupa njia rahisi zaidi.....

Sasa napata shida sana mno... ila niwaambie ndugu zangu wote giza likitanda sana jua kunakucha
 
Hata mimi nimeona hicho, huwa natamani kumshauri ila kwa sababu Sina tu nafasi ya kumpata huwa na mwomba sana Mungu roho fulanj ya hekima impate aache kuogopa. Raisi bado unafanya Kazi nzuri tu, no one is perfect under the sun ila mapungufu ni kitu cha kawaida sana. Sasa anapo react na kila negative issue juu yake au serikali hapo huwa ananiacha Hoi. I ignore watapiga kelele kwanza ni advantage kwake kujua what is going on na kimoyomoyo unakifanyia Kazi unawa shit tu
 
Mkuu hebu tuelekeze jinsi ya kutumia hiyo VPN na for browser

Mkuu achana na VPN,hua zinauzwa na zinablock PC yako nzima isionekane huko duniani unnecessarily!

Kwavile unataka JF tu wasichukue data zako za IP na usenge mwingine ,dawa yao ni simple tu,tumia TOR browser,basi!

Search Google,Tor browser,download,install kwenye PC yako,then fungua hiyo browser,type Url ya JF tu kama unavyofungua websites zingine kwenye browser yoyote!

Then you are done!

Tor browser itaficha IP zako zinazokupa internet connection,locations na browsing data zako zote hawa wapumbavu hawatakaa wazipate!

Tor itakua inawapa IP za Ulaya or elsewhere tu,na locations za Ulaya au elsewhere tu na sio TZ kabisa!

JF will never know who you are!
 
Amani ya dunia imeshikwa na mwanamke,mwanamke akizembea kwenye malezi asipomfundisha mtoto dini na Upendo, akiwa mkubwa atageuka laana Kwa wenzake,labda tu akipata uponyaji wa ndani. Atasababisha uchungu Kwa wenzie, maana Furaha yake ni kuona wengine wakiteseka, wakilia,wakiumizwa,wakiuwawa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaandika ujumbe huu kwa huzuni sana kwasababu kati ya viongozi ambao nilikuwa ninaamini genuinely wangeweza kuleta mageuzi katika nchi hii Magufuli alikua namba moja.

Nilikua shabiki yake toka alipokua Waziri wa Ujenzi na hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais bado nilimpenda kwa dhati. Ni kiongozi ambae amenifanya niwe na keen interest na maswala ya kisiasa.

Jana nilipatwa na hasira nilipoona kwenye habari kuwa Bunge limepitisha Muswada kandamizi wa vyama vya siasa. Haiitaji rocket science kujua kwamba ule Muswada umeandaliwa kwa dhumuni kubwa la kudhibiti vyama vya upinzani. Hapa ndipo nilidraw the line na kugundua kuwa Magufuli si kiongozi mzuri kama nilivyomdhani.

Nilijiuliza swali la msingi; Kwanini huyu Rais anatumia nguvu nyingi kunyamazisha dissenting voices? Ni kweli kwamba kwenye siasa kuna propaganda, uzushi na uongo mwingi sana lakini hiki hakipaswi kuwa chanzo cha Serikali ya Magufuli kuweweseka.

Utawala wa Mhe. Kikwete, wapinzani walishamiri na kupinga masuala mbalimbali katika Serikali lakini hatukuona utawala wa Kikwete unatumia resources nyingi kucrackdown wapinzani. Si muwaache waongee, kwani ni lazima wasikilizwe.

Hii inadhihirisha kuna mambo mengi yanafichwa ndani ya Serikali ya Magufuli maana haileti maana wewe kuzuia watu wenye mawazo tofauti na yako kuongea.

If anything, this proves that Magufuli ni kiongozi insecure sana. Wapinzani walimsema Kikwete kwamba ni kiongozi dhaifu, ila ukweli mchungu ni kwamba Magufuli ni dhaifu zaidi. Utaona kwa jinsi tu anavyotumia nguvu nyingi katika ulinzi wake. He is the most protected President in our country's history. Amemwaga sana hela kwenye Usalama wa Taifa kwa ajili tu ya ulinzi wake. 80% ya staff wa TISS wamebadilishwa katika uongozi wake na anaweka vijana wadogowadogo wasio na experience wala mafunzo ya kutosha, mwishowe wanaishia kuteka na kutisha watu.

Kwa wakazi wa Kijitonyama wataelewa ni kwa namna gani wanashuhudia miili ya watu iliyotupwa kwenye viroba kila kukicha.

Tusipokuwa makini na kutafuta mbinu za kumdhibiti huyu Rais ambaye anajiiona ni invicible, itakuja kutucost when it is too late.

Najua anatabia ya kusema "pesa zipo" ila Serikali sasa hivi haina pesa. Development partners are pulling out aid and funding of projects kwa sababu ya sheria kandamizi na ukiukwaji wa haki.

Ni kwa sababu hii huoni sikuhizi kwenye speech zake akiwasema vibaya hawa wahisani maana wamemshika pabaya. The government is really broke na hizi sheria kandamizi zinazoendelea kutungwa haziisaidii nchi kabisa.

My advice to the President:

Ulianza vizuri sana mwaka wa kwanza na nusu ya uongozi wako, you were the model of good African leadership and everyone was in love with you. Sijui ni nini kilitokea baada ya hapo sababu wewe ni Kiongozi ambae ungeweza kuwa zaidi ya Nyerere but you ruined it.

Mimi nakushauri uwaachie watu wazungumze bila kuwaekea vikwazo, sio lazima uwasikilize. Huwezi kuongoza kwa kujenga mazingira ya hofu, hata mawaziri wako wanakuogopa.

Umekuwa Waziri wa kila wizara, they cant make decisions sababu wanaogopa jinsi ulivyo unpredictable. Wewe na mpwa wako mmejimilikisha hazina ya nchi, yule Waziri mpango yupo pale kama pambo, hana nguvu kabisa.

Hii nchi ni yetu sote, tuvumiliane. Angalia mfano wa mwezako wa Ethiopia, hata rafiki yako Kagame ameanza badilika. Its the 21st century, the age of the internet, huwezi kuongoza with an iron fist na ukawa successful ipo siku itakucost.

All the best katika majukumu yako!!

Pole sana kwa kukariri maisha. Kila sikumaisha yanabadilika na unatakiwa ni jinsi gani unaweza kukabiliana nayo. Bajeti ya ulinzi enzi za nyerere haitaweza kulikana na ya awamu ya 4,5 hata ya 10. Teknolojia ya enzi zile si ya sasa. Uzalendo wa Tz wa miaka ya 70, 80 hautakuwa wa miaka ya 2000’s ndo maana unaona hata ulinzi upo tofauti.
Pil usijidanganye kwa namna yeyote ile kuwa kuna kiongozi anapenda wapinzani. Hata hao wapinzani wakiwa madarakan hawatawapenda wale wasiokuwa ktk uongozi. Anzia ndani ya vyama tu, ukitaka ugomvi mpinge Mbowe, Lipumba nk utajua maana ya upinzani. Ugali mtamu bwana.
Kumuona kuwa ni mwoga nk nk ninsehemu ya maisha. Hata wewe una uoga wako sehemu fulan. Hata ukisikia demu wako yupo (kama wewe ni mwanaume)na njema, pressure itapanda na kushuka.
Soma alama za nyakati
 
Ahahah jamaa wametutenda vibaya ili kuzima mjadala wa muswada wa hovyo wameamua kuweka bongo movie ya bundi,badala ya kujadili ili suala wanaharakat weanza mbwembwe zao mara bundi hivi mara bundi vile.Nonsense
 
Tatizo si JK wala JPM wala rais awaye yoyote aliyetangulia bali tatizo ni CCM, hiki ni chama ambacho Watanzania kwa makusudi kabisa walishindwa kukidhibiti tangu awali...

Mwisho wa siku kimejitwalia hati miliki ya taifa kiasi kwamba ukiwa mwanaCCM kwa ngazi yoyote ile unabaki kuwa untouchable...

JPM ataondoka kama walivyoondoka wengine, atakuja mwingine as long as ni mwanaCCM kitachobadilika ni jina tu la mtawala lakini si uvuli wa utawala utaendelea kuwa uleule (tabia ya uCCM itaendelea)...

Kwa sasa wewe unamuona JPM mbaya simply ni vile he has ile CCM effect within him, lakini mfano waliopo nje ya TZ wasiokuwa affected na CCM effect wanatamani JPM walau awe kiongozi wao hata kwa siku 1 tu...

CCM ni kama blackhole vile it would suck whatever comes/passes across, tena ni kama imani vile...kwa mwanaCCM yoyote kwao CCM ni kwanza pengine kuliko taifa
 
Back
Top Bottom