Magufuli ni Rais muoga haijawahi tokea katika nchi hii

Magufuli ni Rais muoga haijawahi tokea katika nchi hii

Adui akishafahamu udhaifu wako ulipo basi watakutesa kama mtoto mdogo na usijue cha kufanya...

Kwa hili la magufuli, wapinzani washagundua ya kwamba magufuli hataki kusemwa vibaya, so na wao wanatumia udhaifu wake huu kumsema zaidi na hili magufuli asipikuwa makini na vile ni mtu wa hasira sana anaweza fanya tukio baya ambalo litamuondosha madarakani kwa nguvu...

Na watu wenye tabia kama zake hawafai kupewa nchi maana atatengeneza makundi mengi katika utawala wake na hadi tunavyoongea ni kwamba kuna watu ndani ya chama chake wanatamani apoteze maisha kabisa maana washamchoka sema tu ndio hivyo ni nani wa kumfunga paka kengele...
 
Ulianza vizuri sana mwaka wa kwanza na nusu ya uongozi wako, you were the model of good African leadership and everyone was in love with you
Alianza vizuri na bado anaendelea vizuri tu kwan unadhan kwanini kama muswada sio wa haki mbona umepitishwa na bunge, wewe ni nani ulione bunge halina akili kuukubali na kuupitishwa muswada huo?? na by the way everyoneis still in love with him ( am talking about people who are not delusional)
 
Ukishapita muswaada wa Miaka 7 utafuata muswaada wa kutokuwa na ukomo kutawala milele, ili yatimie aliyonena itatawala milele
Ashasembeko umeandika kwa hisia sana, ila tunakoelekea Mungu ndio anajua, kwanza Jeshi, puli bunge na juzi tumehitimisha na juma wa mahakama tunamaliza na msajili then tunapeleka muswada wa kuongeza muda wa urahisi , tunaondoa ukomo maana sioni kama kuna mtu atakuja kuziweza changamoto zilizopo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa kukariri maisha. Kila sikumaisha yanabadilika na unatakiwa ni jinsi gani unaweza kukabiliana nayo. Bajeti ya ulinzi enzi za nyerere haitaweza kulikana na ya awamu ya 4,5 hata ya 10. Teknolojia ya enzi zile si ya sasa. Uzalendo wa Tz wa miaka ya 70, 80 hautakuwa wa miaka ya 2000’s ndo maana unaona hata ulinzi upo tofauti.
Unafananisha maendeleo ya vitu ambayo ni direct proportional na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya tabia ya watu?

Watu hua hawabadiliki kwa generation moja au mbili,sayansi inasema walao miaka 1000!

Sasa kutoka Nyerere mpaka Magufuli kuna miaka 1000?

Hoja yako ya ulinzi ni ya kipumbavu maana Waziri Mkuu wa Sweden au Switzerland anaenda kazini kwa mguu na hana ulinzi wa aina yoyote!Halafu Sweden na TZ ipi imeendelea?

Yaani nchi zimekua na kuvuka stage ya ya u-savage na kwenda ustaarabu!

Tabia ya fujo,ulinzi,majeshi,kuuana,kuumizana,etc ni tabia bado za savage animals.

Sasa wakati dunia inatoka huko kwenda kwenye ustaarabu,wewe na jamaa zako mnaona ndio wakati wenyewe hasa wa mafujo na maulinzi ya kipumbavu,etc!
 
Alianza vizuri na bado anaendelea vizuri tu kwan unadhan kwanini kama muswada sio wa haki mbona umepitishwa na bunge, wewe ni nani ulione bunge halina akili kuukubali na kuupitishwa muswada huo?? na by the way everyoneis still in love with him ( am talking about people who are not delusional)
Majority ya wabunge wa chama tawala bungeni ndio inafanya wabunge wote waonekane wa hovyo. Unakumbuka suala la kikokotoo? Ndivyo ilivyotokea kwa muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa. Wabunge wa CCM wakishaitwa kwenye caucus hawana usemi kbs kwa mwenyekiti wao
 
Unafananisha maendeleo ya vitu ambayo ni direct proportional na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya tabia ya watu?

Watu hua hawabadiliki kwa generation moja au mbili,sayansi inasema walao miaka 1000!

Sasa kutoka Nyerere mpaka Magufuli kuna miaka 1000?

Hoja yako ya ulinzi ni ya kipumbavu maana Waziri Mkuu wa Sweden au Switzerland anaenda kazini kwa mguu na hana ulinzi wa aina yoyote!Halafu Sweden na TZ ipi imeendelea?

Yaani nchi zimekua na kuvuka stage ya ya u-savage na kwenda ustaarabu!

Tabia ya fujo,ulinzi,majeshi,kuuana,kuumizana,etc ni tabia bado za savage animals.

Sasa wakati dunia inatoka huko kwenda kwenye ustaarabu,wewe na jamaa zako mnaona ndio wakati wenyewe hasa wa mafujo na maulinzi ya kipumbavu,etc!

Sawa mm ni mpumbavu ila wewe mwenye hekima umeshindwa kujielewa n kutofautisha kati ya jamii moja hafi nyingine. Ulinzi na ujuzi wa sweden utaulinganisha na wa Tz? Ustaarab wao na maendeleo yao yanafanana na ya Tz? Ndo maana nimekuambia acha kukariri maisha.
 
Mkuu hongera sana kwa mada nzuri na ukweli mchungu kwa misukule,Tanzania hatuna rais tuna viroja .Vitendo vinavyofanyika Tanzania ni vya ajabu sana awamu hii ,Hata waliomuweka madarakani mkapa ,kikwete ,mwinyi wanajuta .
 
Majority ya wabunge wa chama tawala bungeni ndio inafanya wabunge wote waonekane wa hovyo. Unakumbuka suala la kikokotoo? Ndivyo ilivyotokea kwa muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa. Wabunge wa CCM wakishaitwa kwenye caucus hawana usemi kbs kwa mwenyekiti wao
sio kweli, kwahyo unataka kusema wabunge wa CCM hawana uwezo wa kuona kwamba hicho kitu wanachokubali kupitisha kitakua na effect kwao hapo mbeleni? kiasi kwamba wakubali tu kisa wameambiwa na mwenyekiti wao? am sure hata wapinzani wapo walioafiki vizur sana na ndio mana umepita bila wasiwasi
 
sio kweli, kwahyo unataka kusema wabunge wa CCM hawana uwezo wa kuona kwamba hicho kitu wanachokubali kupitisha kitakua na effect kwao hapo mbeleni? kiasi kwamba wakubali tu kisa wameambiwa na mwenyekiti wao? am sure hata wapinzani wapo walioafiki vizur sana na ndio mana umepita bila wasiwasi
Wao CCM wanaamini kwamba wataongoza milele. Hawaamini kwamba akili za wananchi inaadilika kutokana na kizazi, wanayoyaona yanafaa leo huenda yasifae miaka 10 ijayo. Hilo wao hawalioni ndio sababu wanapitisha takataka nyingi sana bungeni kwa sababu ya wingi wao. Haimannishi kwamba natete kila wanachopinga wapinzani, nao kuna mahali wanakosea sana tu. Wengi wape, lakini wachache wasikilizwe. Kumbuka ya mchakato wa katiba, nani walipinga katiba ya tume ya Warioba?
 
Mkuu umetoa ukweli mchungu sana!

Huko PM usikubali kumpa mtu namba yako ya simu,wala usikae u-reveal your identity to anyone humu!

Pia kuna watu watajifanya mademu watakufuata kua wanakupenda wataomba mawasiliano yako,usitoe kabisa!

Na pia,usijibu even their PMs.

Ignore them 100%!

Serikali oga sana hii,watajifanya wanatumia honey pot kukutafuta,they are stupid to the core!

Kama kweli ile idara nyeti inatumia kodi za watanzania kusaka wakosoaji tena wanaokosoa kistaarabu na kwa kusema kweli, basi ujue kuna tatizo na inatakiwa ijitathimini kwa kina. Kama waliomfuata Zitto na kumtisha kumuua wanatoka huko pia, ni wazi kuwa kuna shida na weledi na utendaji umepwaya sana.

Idara ile haiko kwa ajili ya maslahi ya mtu au kikundi cha watu bali kwa maslahi mapana ya taifa bila kujali dini, rangi, itikadi wala kabila.
 
Ninaandika ujumbe huu kwa huzuni sana kwasababu kati ya viongozi ambao nilikuwa ninaamini genuinely wangeweza kuleta mageuzi katika nchi hii Magufuli alikua namba moja.

Nilikua shabiki yake toka alipokua Waziri wa Ujenzi na hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais bado nilimpenda kwa dhati. Ni kiongozi ambae amenifanya niwe na keen interest na maswala ya kisiasa.

Jana nilipatwa na hasira nilipoona kwenye habari kuwa Bunge limepitisha Muswada kandamizi wa vyama vya siasa. Haiitaji rocket science kujua kwamba ule Muswada umeandaliwa kwa dhumuni kubwa la kudhibiti vyama vya upinzani. Hapa ndipo nilidraw the line na kugundua kuwa Magufuli si kiongozi mzuri kama nilivyomdhani.

Nilijiuliza swali la msingi; Kwanini huyu Rais anatumia nguvu nyingi kunyamazisha dissenting voices? Ni kweli kwamba kwenye siasa kuna propaganda, uzushi na uongo mwingi sana lakini hiki hakipaswi kuwa chanzo cha Serikali ya Magufuli kuweweseka.

Utawala wa Mhe. Kikwete, wapinzani walishamiri na kupinga masuala mbalimbali katika Serikali lakini hatukuona utawala wa Kikwete unatumia resources nyingi kucrackdown wapinzani. Si muwaache waongee, kwani ni lazima wasikilizwe.

Hii inadhihirisha kuna mambo mengi yanafichwa ndani ya Serikali ya Magufuli maana haileti maana wewe kuzuia watu wenye mawazo tofauti na yako kuongea.

If anything, this proves that Magufuli ni kiongozi insecure sana. Wapinzani walimsema Kikwete kwamba ni kiongozi dhaifu, ila ukweli mchungu ni kwamba Magufuli ni dhaifu zaidi. Utaona kwa jinsi tu anavyotumia nguvu nyingi katika ulinzi wake. He is the most protected President in our country's history. Amemwaga sana hela kwenye Usalama wa Taifa kwa ajili tu ya ulinzi wake. 80% ya staff wa TISS wamebadilishwa katika uongozi wake na anaweka vijana wadogowadogo wasio na experience wala mafunzo ya kutosha, mwishowe wanaishia kuteka na kutisha watu.

Kwa wakazi wa Kijitonyama wataelewa ni kwa namna gani wanashuhudia miili ya watu iliyotupwa kwenye viroba kila kukicha.

Tusipokuwa makini na kutafuta mbinu za kumdhibiti huyu Rais ambaye anajiiona ni invicible, itakuja kutucost when it is too late.

Najua anatabia ya kusema "pesa zipo" ila Serikali sasa hivi haina pesa. Development partners are pulling out aid and funding of projects kwa sababu ya sheria kandamizi na ukiukwaji wa haki.

Ni kwa sababu hii huoni sikuhizi kwenye speech zake akiwasema vibaya hawa wahisani maana wamemshika pabaya. The government is really broke na hizi sheria kandamizi zinazoendelea kutungwa haziisaidii nchi kabisa.

My advice to the President:

Ulianza vizuri sana mwaka wa kwanza na nusu ya uongozi wako, you were the model of good African leadership and everyone was in love with you. Sijui ni nini kilitokea baada ya hapo sababu wewe ni Kiongozi ambae ungeweza kuwa zaidi ya Nyerere but you ruined it.

Mimi nakushauri uwaachie watu wazungumze bila kuwaekea vikwazo, sio lazima uwasikilize. Huwezi kuongoza kwa kujenga mazingira ya hofu, hata mawaziri wako wanakuogopa.

Umekuwa Waziri wa kila wizara, they cant make decisions sababu wanaogopa jinsi ulivyo unpredictable. Wewe na mpwa wako mmejimilikisha hazina ya nchi, yule Waziri mpango yupo pale kama pambo, hana nguvu kabisa.

Hii nchi ni yetu sote, tuvumiliane. Angalia mfano wa mwezako wa Ethiopia, hata rafiki yako Kagame ameanza badilika. Its the 21st century, the age of the internet, huwezi kuongoza with an iron fist na ukawa successful ipo siku itakucost.

All the best katika majukumu yako!!
Pamoja na kutubu kwako hadharani lakini Nasikitika kukuambia kwamba hauko makini kabisa ! Mtu yeyote aliyekuwa ana akili hata ya kuvukia barabara tu alitakiwa awe amemfahamu Magufuli tangu alipokuwa Waziri , Matendo yake ya nyumbani na ofisini , ikiwemo hata hotuba zake jimboni kwake akiwa mbunge ilikuwa ushahidi kwamba akiwa Rais atafanyaje
 
Pole sana kwa kukariri maisha. Kila sikumaisha yanabadilika na unatakiwa ni jinsi gani unaweza kukabiliana nayo. Bajeti ya ulinzi enzi za nyerere haitaweza kulikana na ya awamu ya 4,5 hata ya 10. Teknolojia ya enzi zile si ya sasa. Uzalendo wa Tz wa miaka ya 70, 80 hautakuwa wa miaka ya 2000’s ndo maana unaona hata ulinzi upo tofauti.
Pil usijidanganye kwa namna yeyote ile kuwa kuna kiongozi anapenda wapinzani. Hata hao wapinzani wakiwa madarakan hawatawapenda wale wasiokuwa ktk uongozi. Anzia ndani ya vyama tu, ukitaka ugomvi mpinge Mbowe, Lipumba nk utajua maana ya upinzani. Ugali mtamu bwana.
Kumuona kuwa ni mwoga nk nk ninsehemu ya maisha. Hata wewe una uoga wako sehemu fulan. Hata ukisikia demu wako yupo (kama wewe ni mwanaume)na njema, pressure itapanda na kushuka.
Soma alama za nyakati
Hamna anaesema apende upinzani.... lakini inabidi awavumilie maana walikuwepo, watakuwepo na walizidi kuwepo
 
Naona unapiga mayowe yasiyoeleweka.

Inawezekana hata sheria ya vyama vingi iliyopitishwa hujaisoma lakini unakimbilia Jamiiforums kuja kupiga kelele ambazo hazieleweki badala ya kutumia muda wako kuisoma hiyo sheria.

Hujui kama sheria hii imebadilishwa mara sita tokea mwaka 1992 na sasa inakuwa ni mara ya saba kufanyiwa marekebisho.

Kama Rais ni dhaifu zaidi ya Kikwete, kwa nini sasa unalalamika?

Nani alikuambia Rais ndiye anaweka ulinzi wake?
Mkuu this regime imeng'oa ubongo wako now wamekupandikizia kitu kingine kabisa kichawani pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu bwana hajawahi kuwa kiongozi mzuri hata mara moja. Tatizo kubwa la watanzania wanadanganyika na vitu vidogo sana vya hadaa.

Tangu akiwa waziri wa ualiendesha mambo yake kwa hadaa nyingi. Hivi mlikuwa hamshtuki akienda kumkaripia mkandarasi, vyombo vya habari vilikuwa vikisema, 'amefanya ziara ya kushtukiza na kumkaripia mkandarasi', lakini cha ajabu ni kuwa safari ni ya kushtukiza lakini vyombo vya habari vyote vipo!

Kiongozi anayewanunua wanahabari ili wote wawepo wakati anafanya tukio lolote lile, mwogope sana. Madikteta wote duniani huwa hawataki wasikie mtu mwingine yeyote anasikika kwenye vyombo vya habari, isipokuwa yeye tu. Alifanya hivyo Mobutu, Idd Amin, Nguema, Pinochet, Samuel Die na wengine wote.

Msisikilize mtu anachobena, bali yasimeni matendo na tabia zake. Hapa tunafiga bomu. Siku likilipuka hakuna cha CCM wala CHADEMA au mwingine yeyote, wote tutaangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anajithibitisha kupitia muswada huo - wakati Kingunge, Sumaye na Lowassa wakipitisha baadhi ya miongozo na sheria kadhaa kuhusu demokrasia nchini hawakujuwa kwamba mbeleni watakwaa kizingiti - tunaenda uchaguzi wa 2020 wabunge hao hao kitambo watajiona walivyokuwa wanazi

Amani ya nchi hii isichezewe - viongozi ondoeni hofu ya kupoteza nafasi
 
Back
Top Bottom