Jana nilipatwa na hasira nilipoona kwenye habari kuwa Bunge limepitisha Muswada kandamizi wa vyama vya siasa. Haiitaji rocket science kujua kwamba ule Muswada umeandaliwa kwa dhumuni kubwa la kudhibiti vyama vya upinzani. Hapa ndipo nilidraw the line na kugundua kuwa Magufuli si kiongozi mzuri kama nilivyomdhani
Aiseee, wewe ulichelewa sana kugundua
Niseme wazi, hata mimi nilikuwa kama wewe huko mwanzo; lakini niligundua mapema sana kuhusu udhaifu wake mkubwa alipoanza tu kutaka kuingilia mihimili mingine.
Hatua ya kwanza kabisa iliyonistua ni kumteua yule binti kuwa mbunge na kutaka agombee uspika. Taa yangu ya kwanza ya tahadhari ilianzia hapo. Na haraka haraka akalizima bunge lisionekane. Yote haya yaliongeza hofu yangu juu yake, ingawaje hayakuondoa matumaini yangu yote kwa wakati huo.
Ilipokuja kwenye "Makinikia" na mizengwe yote iliyofanyika nikajua dhahiri hapa tuna tatizo kubwa, na hasa alipoangukia kwenye kuwaweka ndani (mahabusi) kila aliyetofautiana na kauli zake. Akina Lissu wakawa na makazi mawili, lockup na nyumbani.
Lakini hadi wakati huo, matumaini yangu kwake yalikuwa bado hayajafifia sana kwani yalikuwepo matendo mazuri aliyoyafanya; kama kupambana na ufisadi, kurekebisha tabia za wafanya kazi, n.k.
Na hata hilo la "Makinikia" lilkuwa tendo zuri lililofanywa vibaya.
Ilipofikia hatua ya bei ya hayo mazuri kuwa ndio kiasi sahihi cha kuuza utu, haki za uTanzania wangu; mzigo nikautua!
Niseme wazi, isingekuwa haya ya ukandamizaji, uonevu, kunyima haki na matakataka nisiyoweza kuyaandika hapa, Magufuli angekuwa kiongozi mzuri sana na nchi yetu ingeweza kupiga hatua za maendeleo haraka sana.
Hapakuwa na sababu yoyote ya kuyaingiza haya mabaya kwenye utawala wake, kwani mazuri yalitosha kabisa kumjengea heshima kwa sisi raia wengi. Unapominya haki za watu, hata ufanye mazuri kiasi gani wapo watakaokupinga tu upende, usipende..