Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Kuna issue hii ya uchaguzi wa 2019. Tusiondoshwe ktk mjadala huu kupitia "remote factors". Rais hawezi kulalamika na kutafuta huruma ktk kipindi hiki na kuelekea 2020 kupitia mambo ya kihistoria.

Kama amejirizisha na jambo ni wakati wake wa kutenda ili haki yote ipatikane. Taasisi ya Urais ituambie tumefikia wapi na mchakato wetu wa uchaguzi 2019. Kujaribu kututoa ktk mjadala huu, itakuwa ni kutotendea haki umma wa Watanzania.
Ushindi wa kishindo wamepita bila kupingwa wewe uko wapi
 
macho_mdiliko,
Mambo yaliyokuwa yamejificha yamezidi kufunuliwa. Kwa mfano, sasa tunajua bila ya shaka yoyote kwamba 'sponsor' wa Magufuli kwenye kinyang'anyiro cha urais 2015 hakuwa mwingine bali Mkapa. Kikwete hakuwa na njia ya kuzuia hili.

Kikwete alikuwa Waziri wa Mkapa kwa miaka 10. Mkapa hakuwa na njia na uwezo wa kumzuia Kikwete kuingia Ikulu wakati huo. 'Sponsor' wa Kikwete alikuwa nani? MTANDAO!
 
Wewe mhehe Wa Miyomboni Iringa ndiye unaona huyu ni chaguo la mungu sijui wale wahindi Wa Shree Hindu Mandal wanaoabudu ng'ombe wakisema huyu chaguo la ng'ombe sijui utabishaje
 
Sifahamu lakini wakati ule nakumbuka hapa JF tuliliongelea na alikwenda kutibiwa kwenye one of the Scandinavian countries. Kama sikosei Mzee Mwanakijiji vile vile aliligusia. Lakini hatukujua kama alipewa sumu, hilo linashtusha ndio mfahamu siasa zetu za Tanzania zilivyo. Mwenyezi Mungu atakulinda tu hata kama mafisi yako porini yanakusubiri.

Last time tuliongelea kutoruhusu kila Tom Dick and Harry kutaka kusalimiana na rais, ifike mahali huo mtindo uachwe maana waovu huwa hawana sura. Nimeshangaa leo hata Zito kajitokeza ambaye alivumisha ule udaku wake, the boy is not ashamed? Hivi Wizara ya Mambo ya Ndani imechukua hatua gani? Au walitaka kuchukua hatua akifa? Haya mambo ni lazima sasa yachukuliwe kwa upana na ukubwa wake. As a Country we need to act now.

Kama shambulio la Lissu, tena hilo sio la sumu bali risasi, hapo ndio utajua mwenyezi Mungu analinda watu wema hata mafisi wenye madaraka wakitaka kukuua
 
Na Mimi nimeliona hilo na nimetishika sana. Kwa tabia zake tunazofahamu jee kama ni kweli waliofanya hivyo wako salama kweli?
Wawe salama ili iweje sasa? Maaduiwake wakiwa salama inamaana nayeye bado yuko exposed..tofauti itakuwa ugumu wa penetration.
 
Tukianza kutaja changamoto na kuwa ukipata changamoto unakua kiongozi asilimia kubwa tungekua marais, bora yeye walimlisha sumu na hasiowajua wengine walikatwa mikono na miguu kwa sababu za kisiasa na watu wanaowaona na hakuna hatua zilizochukuliwa.
 
Kiukweli baada ya kusikiliza maelezo ya Rais Magufuli namna alivyopitia changamoto mbalimbali za kisiasa bila kukata tamaa hadi kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi, mimi Johnthebaptist ninasadiki kuwa kweli huyu ni chaguo la Mungu.

Kwa namna mkono wa Mungu ulivyomlinda katika safari yake ya kisiasa hata kuwalegeza wale wenye nia ovu waliojaribu kumdhuru, mimi ninasadiki huyu ni chaguo la Mungu.

Mungu endelea kumbariki Rais Magufuli

Maendeleo hayana vyama

Amina!
Hata mie nilinyweshwa sumu ya mamba hakika na mimi ni chaguo la Mungu
 
binti kiziwi umeona hapa walitarget moyo, hakika alikuwa na bahati kwelikweli mpenzi
 
Kama shambulio la Lissu, tena hilo sio la sumu bali risasi, hapo ndio utajua mwenyezi Mungu analinda watu wema hata mafisi wenye madaraka wakitaka kukuua
FYI wewe ndio unasema wema na wabaya. Mwenyezi Mungu wote tupo sawa kwake kwa sababu yeye ndio katuumba wote. Anafahamu dhamira zote ambazo tumeficha mioyoni mwetu.
 
Back
Top Bottom