Magufuli: No more education for girls who fall pregnant while at school.

Magufuli: No more education for girls who fall pregnant while at school.

The Tz govt should think thru this decision mazee. My heart is really crying out for those children and parents, the poor parents who cannot afford the private schools who have found themselves in this situation.

Jailing a schoolboy, an underage for 30yrs, just for impregnating a schoolgirl in what was a consensual hunky punky seems very punitive to me, I wonder if it is even consistent with the current Tanzanian laws, and definately it is not in tandem with the international laws protecting children.

They ought to be given a second chance at education. Many have talents and potential to add value to the Tanzanian society. How will the young lady raise her child without a good education to afford her a good job, and her child's father languishing in jail for 30odd years. Condemning this young lady and her baby to a life of penury; it is very unjust, inhumane.

And what if tge girl concieved her baby thru rape? It is so unfair.

I was I could tell Magu right on his face how stupid and unnecessary this law is.
And let the parents in question learn how to scold their children!

Tunakabiliwa na tatizo kubwa sana la wanafunzi kupata ujauzito kizembe kizembe tu! Hii itawanyoosha sana! No mercy at all!

Subiri baada ya mwaka mmoja utaona idadi ya watoto wanaopata ujauzito inapungua tu yenyewe!

Kwa hili naunga mkono kabisaaaaaaaaaaa!


A girl should learn to choose wisely, either being a mother or a student! Lazima mwanafunzi ajue kuwa the moment anafanya unprotected sex, the moment she becomes a mother
 
Imagin, serekali imekunyima elimu, alafu ukipata kazi serekali inamshika alie kupa kazi kwa tuhuma za "child labour" . Ukijipatia kazi mwenyewe yani self-employed, serikali hio hio iko mlangoni kwako ikidai kodi ili isomeshe watoto elimu ya bure ilihali walikifukuza.. Hio haiwezekani! No no.

Pesa ua kusomesha watoto sio pesa ya Magu au nyanyake, ni mali ya uma ! Yani hii kitu imeniudhi kabisa ninavyozidi kufikiria.

Basic education is a right, and as such a basic right it is unconditionally guaranteed by the state. It is not a privilege, its a right...That means whether you are albino, blind, deaf, have skin disease, have HiV/Aids , you are entitled to basic education guaranteed by the state! Whether you are male,female,blue or black, old or young.... You still have your right no discrimination..

Alafu eti mvulana atafungwa 30years! What??? We are in 21st century bana! Mvulana na msichana wote wako na akili sawa, mwanzo sikuhizi wasichana wengine hutongoza wavulana ... Mbona umwadabu mvulana zaidi, this is gender discrimination! Alafu hauwezi kumfunga mtu bila evidence, je mtahakikishaje mvulana flani ndo baba? Hii inamaanisha italazimu mfanye mandatory DNA testing kwa mtoto mchanga na pia mshukiwa ambayo ni kinyume na haki (unless ni kesi ya ubakaji au mzazi amekibali) .Mbali na hivyo, ni hospitali ngapi za serekali tz ziko na uwezo wa kufanya full DNA testing? Hii inamaanisha si wavulana wengi watafungwa, ni wanawake wajawazito ndo wataonewa tu, wakishafukuzwa shule kesi inaishia hapo
Kwani lazima usome bure? Vya bure vina masharti yake, na ndo hayo, hakuna ujauzito!

Ukitaka ujauzito nenda private schools, au kwenye vituo vya elimu ya watu wazima, mbona inawezekana tu kusoma!
 
Does't make sense, na wale wanaume wanao pachikana mimba wakiwa shule je? Hapo Rais amenoa kabisa.
Wote wanafukuzwa shule na mwanaume anafungwa jela bila huruma, sheria inasema hivyo. Class mate wetu walitiana mimba miaka hiyo mwanaume akafungwa nafikiri mwaka mmoja. Siku hizi anaweza kufungwa miaka hadi 30 kwa ubakaji.
 
Busara itumike, hii sio sawa kabisa, kumkatia mtu elimu ni jambo mbaya sana, mwache alee mwanaye na aendelee kupata elimu kwa ajili ya maisha yake ya kesho.
La sivyo mtaendelea kujawa na vilaza kwenye jamii, watu wasiojua kusoma au kuandika kisa walitupwa nje wakiwa wadogo baada ya kupata mimba, kumbuka mnamfunga mvulana miaka 30, hivyo mvulana pamoja na msichana watakua wanaongeza idadi ya mazezeta kwenye nchi yenu.

Ni kawaida mtu kujikwaa kwenye jamii, lakini unapoanguka unafaa kunyanyuka na kuendelea, hata huyo rais wenu Magufuli kabla awe rais, na kabla hata afikie chuoni, nina uhakika ana makosa mengi lazima aliyafanya akiwa kijana lakini hakukata tamaa, sasa leo iweje yeye awahukumu vijana kihivi.

Maisha ni safari, tunakwenda tu kwa hali zote, kwa masumbuko, kwa mahangaiko na kubanana hadi tufike.
Vitu vya bure vina mashariti. Yeye akitaka kusoma elimu ya bure basi hakuna kuzaa hadi umalize shule. Lakini huo sio mwisho wa kusoma anaweza kusoma private school hakatazwi.
 
Hehehehe!! Aisei wewe ni kada damu, nilisubiri sana tamko lako kwenye hii issue, jameni hata kama tunawapenda marais wetu, tuwe na desturi ya kusema hapana pale wakikosea.

Mimi hapa ni shabiki wa rais Uhuru, na nitampa kura kwenye uchaguzi ujao, lakini itokee aibuke na upuzi kama huu, lazima nikatalie mbali.
Ha ha haaaa Eti unasubiri tamko langu! Kama unanifuatilia vizuri kuhusu mambo ambayo yanamhusu rais wangu, kuna vitu huwa namkosoa hadi hapa kwenye jukwaa la Kenya!

Nakumbuka last time kwenye issue ya TIC nilimkosoa sana rais wangu na wewe ulikuwa ukimtetea, kwa hiyo kutofautiana ni kitu cha kawaida kabisa!

Na kuhusu hili jibu nililotoa kwenye huu uzi ulioquote, hapo nimemjibu mtu alouliza kuhusu wanaume wanaosababisha ujauzito, kwa kuwa hiyo ni sheria hata kama hili suala ambalo ni tamko sio sheria ningekuwa silikubali, bado isingebadili ukweli kuwa sheria tayari ilishatungwa tena wakati wa kikwete!


Halafu kuniita kada, unakosea sana kuniita hivyo maana mimi ni mtu ambaye sipendi siasa hata kidogo! Jaribu kufuatilia mijadala yangu kama utakuta nachangia kule kwenye JUKWAA LA SIASA! Hutaniona hata siku moja huko au kwenye mijadala ya kichama au ya kutetea mtu! Watu wenye vyama vyao hutoleana mapovu huko na wanajuana!

Mimi huwa nachangia kwa mtazamo wangu binafsi bila chembe hata moja ya ushabiki!

Naamini umenipata, narudia tena hilo suala naliunga mkono kabisa, na kwa hapa nchi yetu ilipofikia inabidi tufanye hivyo!
 
Inabidi watanzania mjue nchi ipo under msukuma. So tabia za wasukuma si mnazijua. Itz like tunarudi miaka 40 nyuma
 
Lool as if the stigma that preceeds the pregnancy aint bad enough!!

So much for being the most educated president in EAC amejaa ujinga kwa kichwa !!
 
Inabidi watanzania mjue nchi ipo under msukuma. So tabia za wasukuma si mnazijua. Itz like tunarudi miaka 40 nyuma
"Tanzania aint tribal"

This is how anu tribalist Kenyan Talks


Nyani Kweli Hamuoni Kindule
 


Tanzania president H.E John Magufuli says we will not allow girls who fall pregnant while still at school to continue with their education.

I am sure you didn't get him right! What he said is no going back to public schools ( STD 1 to Form 6). We have system that supports these kind of people anyway! QT is there if they really want to continue with their Secondary education. Msitetee upuuzi. Hakikisheni mnawatunza watoto wenu wasifanye umalaya katika umri mdogo. Ni issue ya maadili. Tunao watoto wa kime na wamemaliza mpaka vyuo wengine na hawakufanya haya mambo. Mr. Presdent is right!
 
"Tanzania aint tribal"

This is how anu tribalist Kenyan Talks


Nyani Kweli Hamuoni Kindule
Mentioning someone's tribe hiyo sio tribal, but voting for someone just because his from same tribe as you that is tribal. Refusing someone a job, just because he/she is from different tribe, that's a big fat tribal.
 
Busara itumike, hii sio sawa kabisa, kumkatia mtu elimu ni jambo mbaya sana, mwache alee mwanaye na aendelee kupata elimu kwa ajili ya maisha yake ya kesho.
La sivyo mtaendelea kujawa na vilaza kwenye jamii, watu wasiojua kusoma au kuandika kisa walitupwa nje wakiwa wadogo baada ya kupata mimba, kumbuka mnamfunga mvulana miaka 30, hivyo mvulana pamoja na msichana watakua wanaongeza idadi ya mazezeta kwenye nchi yenu.

Ni kawaida mtu kujikwaa kwenye jamii, lakini unapoanguka unafaa kunyanyuka na kuendelea, hata huyo rais wenu Magufuli kabla awe rais, na kabla hata afikie chuoni, nina uhakika ana makosa mengi lazima aliyafanya akiwa kijana lakini hakukata tamaa, sasa leo iweje yeye awahukumu vijana kihivi.

Maisha ni safari, tunakwenda tu kwa hali zote, kwa masumbuko, kwa mahangaiko na kubanana hadi tufike.
Acha hizo wewe kufanya hivyo ni kuruhusu mimba mashuleni lazima uchague moja kuzaa au kusoma
 
No need to debate this, you cant cure stupid
 
Hakuna mtu amekataliwa kupata elimu! Alichokisema rais ni kuwa hao wanafunzi wakishapata ujauzito haearuhusiwi kusoma shule za serikali ambazo hapa tanzania elimu inatolewa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita! Yaani alichokikataa rais ni kutoa pesa za serikali kugharimia wanafunzi ambao wanaendekeza kujifungua!


Wanafunzi ambao wanapata ujauzito watatakiwa wasome shule za watu binafsi! Na hapo rais hajaweka mipaka! Tena kuna shule zinatoza gharama za kawaida kabisa! Hivyo wataenda kusoma huko lakini sio kutumia fedha za umma kuwagharamia!

Hata hivyo, sheria tahari ilishatungwa siku nyingi sana! Yeyote anayesababisha ujauzito kwa mwanafunzi pamoja na adhabu nyingine ambazo mahakama itatoa, lazima akatumikie jela miaka 30.


Hivyo wazo lako kuwa tutawapoteza wasomi wengi huo sio ukweli hata kidogo, badala yake tutaendelea kuwa na taifa linalojitambua la watoto kusubiri hadi miaka 18 ifike ndo waanze mambo hayo!

Kaka naomba ieleweke hakuna mzazi mwenye uwezo kifedha anaweza kumpeleka mwanaye kwenye hizo saint kayumba za serikali. Wengi wenye visenti vyao wanapeleka watoto kwenye shule zenye hadhi. Hivyo hao mnaowafukuza kisa wametungwa mimba, mara nyingi huwa wametokea kwenye familia duni kimaisha na hawana uwezo wa kuingia kwa shule bnafsi. Kwa kifupi maisha ya kimasomo kwa mtoto kama huyo yanakua ndio mwisho.

Sasa ukiwaza kwamba huyo binti tayari anapitia hali ngumu kimaisha, halafu uzingatie pia hilo la mimba linakua limempa msongo wa mawazo, wazazi pia wanampelekesha mwendo kasi kwa mitusi na vurugu, ukiunganisha masaibu yote haya na uongeze na hilo la kumtupia nje nje kimasomo na kumfunga jela miaka 30 aliyempachika mimba, yaani huyo mtoto anakua zombi kabisa. Na ndio maana wengi wanaishia kwenye kutoa mimba moja kwa moja. Wasiokua na uwezo huo basi inabidi wakumbane na mateso yote hayo.

Mimi hapa ni mzazi wa binti anayebalehe, naelewa ulezi wa kisasa ni tofauti na kipindi cha akina Magufuli ambapo mtoto alikua anapokea kichapo kwa kwenda mbele, binafsi nilipitia maisha hayo ya old school, tulikua tunapigwa kwa kila kosa. Kizazi cha leo hata kufokea mtoto inakua ni tatizo. Vitoto vimechepua kupita maelezo, vinafanya ngono zaidi ya watu wazima. Na kama akipata mimba halafu unamfanyia anavyosema Magufuli, huyo mtoto anaishia kuwa changudoa kitaa, na ndio maana ukienda kwenye vlabu unakuta wanaojiuza kuna wasichana wadogo ndani yao.

Dunia ya leo imebadilika, mambo hayafanywi kizamani zamani tena, inabidi kuwa makini na mwenye busara na sio kuongoza kwa matamko yenye mikwara na kufoka.
 
Washauri wa rais wetu mtukufu Mhe. JPM wamwambie ukwel rais wetu anapenda sana kuropokaropoka hovyo..
 
f911b9c56d248d09a66fa70c79db552e.jpg

Kwanini lakini?
 
Kwani lazima usome bure? Vya bure vina masharti yake, na ndo hayo, hakuna ujauzito!

Ukitaka ujauzito nenda private schools, au kwenye vituo vya elimu ya watu wazima, mbona inawezekana tu kusoma!
Hakuna kitu kama Elimu ya bure, Kila mwaka kuna bajeti inasomwa na Wizara ya elimu inatengewa pesa zake... Hizo pesa zimetoka kwa wananchi.... Serekali yenyewe iko madarakani na imepewa uongozi kwa niaba ya wananchi....
Kwahivyo hio unayoita 'elimu ya bure' ni ya wananchi na Soo ya serikali, kwahivyo ni wananchi ndo wanafaa kuamua nani anahaki ya kusoma na nani hafai kusoma na wenzake (e.g wahalifu).
Ukiangalia nchi za scandinavia (Netherlands, Switzerland...) utakuta karibu kila kitu ni bure, hata kufanya upasuaji, kutibu cancer, elimu bure hadi university, lakini ukiangalia kodi wanayolipa ni karibia 60% ya mapato... Kwahivyo serekali haina haki ya kinda kutoa masharti ya ni nani atasomeshwa bure wakati ni wananchi ndo wanalipia hio elimu
 
Kitu moja nimenotice wakenya Wengi wanaosapoti Jubilee ndio wanakomalia utadhani wao ndio wamepewa Mimba.

Hii kitu ni ya kimaadili zaidi,.Nimewahi kuwa Mwalimu, Najua vizuri Hulka za hawa Wanafunzi.
Magufuli is Absolutely right. Mtoto achague free education with Right Morals or Kushika Mimba and pay for expensive one.
 
Back
Top Bottom