Nikichogundua kwenye msiba wa Magufuli ni kwamba maadui wa JPM hadi leo hawaamini mtu waliemchukia anaweza kuombolezwa na kuliliwa na watu wengi kiasi kile ndani na nje ya nchi hususa ni Afrika.
Waafrika wengi walipenda staili yake ya uongozi ya kukemea mambo ya ovyo hadharani bila kumuonea mtu aibu. Alikuwa ni mtu mwenye maamuzi na alichukia watu wazembe, Wala rushwa, mafisadi na wahujumu uchumi. Ilifikia hatua hadi Wakenya wanaomba wamuazime Magufuli kwa mwezi mmoja tu ili apambane na ufisadi.
Jina la Magufuli haliwezi kuisha midomoni mwa watu ukizingatia alama alizoacha kwa mengi aliyofanya kwa miaka mitano pekee achilia kazi ya ujenzi wa miundo mbinu aliyofanya kwa miaka 20 akiwa waziri wa ujenzi.
1. Kwa upande wa Africa, Magufuli hakufanya chochote! Kikwete kafanya madogo, hayawezi kutosha kuitwa shujaa.
2. Kwa Tanzania, Magufuli ni Maarufu sana kwa mema na mabaya.
2.1 Ukweli ni kwamba Magufuli alifanya mengi mazuri makubwa kwa Tanzania (ni mengi yanajulikana sina haja kuyataja).
2.2 Lakini, kiutu, Magu alifanya mambo mengi ya laana na kuumiza watu. Mambo hayo yanafuta mema mengi aliyofanya (sala nyingi za majonzi huenda ndo sababu ya kifo cha Magu). Watanzania wengi (a.k.a wanyonge) wanamshabikia sana Magu lakini hawachambui kwa undani:-
a) Tumbua tumbua ya Magu ukichunguza kwa undani utakuta imejaa double standards na uonevu mkubwa. Kuna watu walitumbuliwa kwa makosa madogo ya kuonywa, wengine kwa makosa ya kudhaniwa, wengine kwa kudhaniwa ni network ya fulani, etc, lakini wako wengi waliteuliwa na kulindwa kwenye nafasi zao hata kama mienendo yao ilikuwa wazi kuwa ni ya kifisadi na dhuluma na uenevu kwa watu. Kubomoa makazi ya watu bila fidia, kufukuza watu wenye vyeti vyenye kasoro, akimwacha Bashite, n.k.
b) Kuna kundi dogo lilipiga sana ufisadi kipindi cha Magu. Magufuli alikuwa muongo sana, aliaminisha watu kuwa anapambana na ufisadi (huku akikumbatia genge la mafisadi wachache aliokuwa anakula nao).
c) Magufuli alikuwa muongo sana, alijua kucheza na akili za wanyonye (wasiojua kuchambua akawaaminisha kila kitu). Unakuta kuna watu wanajua kabisa ukweli wa jambo, lakini utashangaa Magufuli anasimama hadharani au wakati mwingine dhabahuni Kanisani kabisa anasema uwongo, kuna wakati alikuwa anamkufuru sana Mungu. Mfano, Magu anajua kabisa Serikali inafanya direct borrowing kutoka kwenye mabenki ya kibiashara ya kutoka nje kugharamia miradi mikubwa ambayo, mwisho wa siku tutalipa tu kwa kodi zetu kwa vizazi vijavyo, lakini anadanganya eti ni makusanyo ya ndani ya TRA. TRA kwa mwezi inakusanya fedha zinazoweza kulipia public wage bill, public debt service na OC- tena OC ya kiwango cha mil. 2 kwa ofisi ya DC kwa mfano.
d) Magu alianzisha miradi na mikataba mikubwa bila kuwepo kwenye bajeti, na bila idhini ya Bunge, na hakukuwa na uwazi wowote katika mikataba. Alijua atakufa na kutuachia mzigo wa madeni. Mfano, aliaminisha Taifa mradi wa Bagamoyo ni wa kifisadi wakati issue ni masharti ya financing ambayo ukiona hayafai unaacha, unatafuta financing nyingine, lakini yeye aliaminisha Taifa mradi haufai. Masharti aliyozungumzia yalibaki tu kwenye speech yake, hayakuwekwa wazi mfano Bungeni, kwa hiyo hatuwezi kujua ukweli, kisa kujustify miradi ya Chato ambayo siyo strategic.
e) Magu alifunga midomo watu wote, aliua utafiti, vyuo vikuu vilizibwa midomo hakuna ushauri wa kitaalamu, na alitoa wataalamu wazuri wa kufundisha vyuo vikuu akawapeleka Serikali na kuanza kuwatukana!
f) Magu alifanya siasa za chuki na uonevu wa wazi na kuligawa Taifa kwa misingi ya vyama, dini na ukanda (badala ya mbinu zingine nzuri za kupambana na upinzani- zipo mbinu nyingi za kistaarabu), halafu anasimama kanisani eti tusibaguane kwa vyama wala dini, dahhh- alijitoa ufahamu sana.
g) Magu aliondoa uwazi (transparency) katika utawala wake, alichukua mrengo wa udikteta (RCs, DCs na Watendaji wengine walijiewekea walinzi na ulinzi bila kustahili), kuzuia bunge live, vyombo vya habari vilipiga tu pambio za kuisifu Serikali, magazeti yalibakia na habari za michezo ndo angalau ununue usome. Kwa ujumla, mrengo wa udikteta, kutokuwepo kwa uwazi na uanzishwaji wa miradi mikubwa bila mpango mara nyingi ni dalili kubwa za Serikali inayokula rushwa na kuitafuna nchi na kundi dogo.
Mpaka leo, kuna watu hawajajua kuwa Magu alikuwa na magumashi mengi! R.I.P, wenye akili hasa viongozi wajifunze kuishi vizuri na watu, watende haki, utawala wako hautadumu milele, Tanzania itadumu. Ukiamua kunyoosha nchi, nyoosha kwa uwazi na bila double standards, hata ukifa uheshimiwe na wote, siyo usifiwe na baadhi na ulaaniwe na baadhi.