Magufuli siyo shujaa wa Afrika, Kikwete ni shujaa wa Afrika

Labda kisukuma yule mutu hakujua kiswahili kwa kwel
 
Ndo ushangae kwa namna gani alifanya Kiswahili kianze kufundishwa na kutumika kwenye mikutano ya AU.
kweli kabisa yaani wasukusu kiswahili chao utacheka mpaka ukae chini halafu yale majamaa hayonagi aibu!! Ni full confidence!!!

Likikosea linaendelea tu.km jiwe alivokuwa vilevile!!

Mtu hujui unachotaka watu wajue sasa huyo si mjinga???
Mtu anae kubali ujinga anaitwaje??.....
 
Hapa sio kundi sogozi. Chukua maarifa sepa.
 
1. Kwa upande wa Africa, Magufuli hakufanya chochote! Kikwete kafanya madogo, hayawezi kutosha kuitwa shujaa.

2. Kwa Tanzania, Magufuli ni Maarufu sana kwa mema na mabaya.

2.1 Ukweli ni kwamba Magufuli alifanya mengi mazuri makubwa kwa Tanzania (ni mengi yanajulikana sina haja kuyataja).

2.2 Lakini, kiutu, Magu alifanya mambo mengi ya laana na kuumiza watu. Mambo hayo yanafuta mema mengi aliyofanya (sala nyingi za majonzi huenda ndo sababu ya kifo cha Magu). Watanzania wengi (a.k.a wanyonge) wanamshabikia sana Magu lakini hawachambui kwa undani:-

a) Tumbua tumbua ya Magu ukichunguza kwa undani utakuta imejaa double standards na uonevu mkubwa. Kuna watu walitumbuliwa kwa makosa madogo ya kuonywa, wengine kwa makosa ya kudhaniwa, wengine kwa kudhaniwa ni network ya fulani, etc, lakini wako wengi waliteuliwa na kulindwa kwenye nafasi zao hata kama mienendo yao ilikuwa wazi kuwa ni ya kifisadi na dhuluma na uenevu kwa watu. Kubomoa makazi ya watu bila fidia, kufukuza watu wenye vyeti vyenye kasoro, akimwacha Bashite, n.k.

b) Kuna kundi dogo lilipiga sana ufisadi kipindi cha Magu. Magufuli alikuwa muongo sana, aliaminisha watu kuwa anapambana na ufisadi (huku akikumbatia genge la mafisadi wachache aliokuwa anakula nao).

c) Magufuli alikuwa muongo sana, alijua kucheza na akili za wanyonye (wasiojua kuchambua akawaaminisha kila kitu). Unakuta kuna watu wanajua kabisa ukweli wa jambo, lakini utashangaa Magufuli anasimama hadharani au wakati mwingine dhabahuni Kanisani kabisa anasema uwongo, kuna wakati alikuwa anamkufuru sana Mungu. Mfano, Magu anajua kabisa Serikali inafanya direct borrowing kutoka kwenye mabenki ya kibiashara ya kutoka nje kugharamia miradi mikubwa ambayo, mwisho wa siku tutalipa tu kwa kodi zetu kwa vizazi vijavyo, lakini anadanganya eti ni makusanyo ya ndani ya TRA. TRA kwa mwezi inakusanya fedha zinazoweza kulipia public wage bill, public debt service na OC- tena OC ya kiwango cha mil. 2 kwa ofisi ya DC kwa mfano.

d) Magu alianzisha miradi na mikataba mikubwa bila kuwepo kwenye bajeti, na bila idhini ya Bunge, na hakukuwa na uwazi wowote katika mikataba. Alijua atakufa na kutuachia mzigo wa madeni. Mfano, aliaminisha Taifa mradi wa Bagamoyo ni wa kifisadi wakati issue ni masharti ya financing ambayo ukiona hayafai unaacha, unatafuta financing nyingine, lakini yeye aliaminisha Taifa mradi haufai. Masharti aliyozungumzia yalibaki tu kwenye speech yake, hayakuwekwa wazi mfano Bungeni, kwa hiyo hatuwezi kujua ukweli, kisa kujustify miradi ya Chato ambayo siyo strategic.

e) Magu alifunga midomo watu wote, aliua utafiti, vyuo vikuu vilizibwa midomo hakuna ushauri wa kitaalamu, na alitoa wataalamu wazuri wa kufundisha vyuo vikuu akawapeleka Serikali na kuanza kuwatukana!

f) Magu alifanya siasa za chuki na uonevu wa wazi na kuligawa Taifa kwa misingi ya vyama, dini na ukanda (badala ya mbinu zingine nzuri za kupambana na upinzani- zipo mbinu nyingi za kistaarabu), halafu anasimama kanisani eti tusibaguane kwa vyama wala dini, dahhh- alijitoa ufahamu sana.
g) Magu aliondoa uwazi (transparency) katika utawala wake, alichukua mrengo wa udikteta (RCs, DCs na Watendaji wengine walijiewekea walinzi na ulinzi bila kustahili), kuzuia bunge live, vyombo vya habari vilipiga tu pambio za kuisifu Serikali, magazeti yalibakia na habari za michezo ndo angalau ununue usome. Kwa ujumla, mrengo wa udikteta, kutokuwepo kwa uwazi na uanzishwaji wa miradi mikubwa bila mpango mara nyingi ni dalili kubwa za Serikali inayokula rushwa na kuitafuna nchi na kundi dogo.

Mpaka leo, kuna watu hawajajua kuwa Magu alikuwa na magumashi mengi! R.I.P, wenye akili hasa viongozi wajifunze kuishi vizuri na watu, watende haki, utawala wako hautadumu milele, Tanzania itadumu. Ukiamua kunyoosha nchi, nyoosha kwa uwazi na bila double standards, hata ukifa uheshimiwe na wote, siyo usifiwe na baadhi na ulaaniwe na baadhi.
 
Kikwete pia si shujaa wa Africa kwa lipi hasa? Shujaa wa Africa ni Baba wa Taifa pekee yake.

Kama alivyoainisha BAK, shujaa wa Afrika ni Baba wa Taifa peke yake kwani alikuwa na vision ya wapi bara letu linatakiwa liende! Kikwete alikuwa na vision gani? Kikwete alikuwa anaongozwa na ideology ipi? Huyu ni mtawala aliyependa starehe na ndio maana alikuwa anaabudu fedha zaidi kuliko utu!!! Enzi ya utawala wake nchi iliibiwa sana maliasili zake kwa yeye kushirikiana na mafisadi wa nje na ndani ya Nchi. Tanzania Ndio Ikawa kinara wa biashara ya madara ya kulevya na marafiki zake ndio wakisimamia biashsra hiyo. Kiongozi kama huyo hawezi kuwa shujaa wa Africa.
 
Reactions: BAK
Watu mtaumia sana kumaliza Mambo ya Magufuli ila amini nawaambia ameacha legacy pia hajafa yupo mioyoni mwa watu muda utaongea katika hili
Ni kweli yule Pimbi ameacha Legacy ya Akina Sabaya na Makonda na ndio maana tunawashughulikia na Mungu akaona yeye apelekwe moja kwa moja kuzimu kwa kuwa uovu wake hauvumiliki machoni kwa Mungu
 
Mbona marehemu anawahangaisha sana? Mbona mnahangaika kuua legacy ya magufuli? , mtu ameshafariki bado roho zinawauma au mlitakaje sasa? Si alikua dictator? C ameshakufa? Ni nini kinawawasha kila siku kumtaja?
 
Mbona marehemu anawahangaisha sana? Mbona mnahangaika kuua legacy ya magufuli? , mtu ameshafariki bado roho zinawauma au mlitakaje sasa? Si alikua dictator? C ameshakufa? Ni nini kinawawasha kila siku kumtaja?
Tena huwa wanasema sasa hivi analiwa na funza!

Mara sijui ‘dead and buried’.

Lakini bado tu wanamuwaza. Amewakaa akilini na hawawezi kujizuia kumuwaza na kumtaja taja!

SMH
 
Nishauliza hilo swal kwa wazee wa legacy kila mmoja anaingia mitini 🤣🤣🤣🤣
 
Ni kweli yule Pimbi ameacha Legacy ya Akina Sabaya na Makonda na ndio maana tunawashughulikia na Mungu akaona yeye apelekwe moja kwa moja kuzimu kwa kuwa uovu wake hauvumiliki machoni kwa Mungu
Mungu kamwaachia Shetani hadi leo na anamvumilia ndio ashindwe kumvumilia huyo Jiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…