Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Soma pia: Sheikh alia na hali mbaya ya vyoo Mbezi Magufuli stendi
Kufuatia malalamiko ya watumiaji wa stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam kuhusu ufinyu wa vyoo kwa abiria, Meneja wa stendi hiyo, Isaac Kasebo amesema vyoo vilivyopo vinatosha, ila tatizo abiria wengi hawajajua mazingira ya stendi hiyo.
“Tatizo ni kutoelewa tu mazingira, lakini vyoo vipo na vinatosha. Jengo la mbele lina vyoo na ndio vinatumika Zaidi, jingo la pili ambalo ni la kusubiria abiria pia kuna vyoo na sasa hivi tumefungua vyoo vingine ambavyo mtu akiingia anaweza kutoka nje ya stendi. Kwa hiyo vyoo vinatosha kabisa, tunachofanya sasa ni kuweka maelekezo ili abiria waelewe.”
Kuhusu abiria kulipishwa kiingilio na kisha kulipishwa huduma ya choo, Kasebo amesema hiyo ni kwa mujibu wa sharia ndogo zinazotungwa na halmashauri.
“Huo ni utaratibu uliowekwa kisheria, kwamba mtu analipa kiingilio halafu atalipa tena choo. Ila kama wanataka walipe maramoja ikiwemo huduma ya choo ni sawa, tumepokea mapendekezo tutayafanyia kazi.”
Faida ya kulazimisha mabasi yote kuingia stendi ya Magufuli
Akizungumzia operesheni ya kulazimisha mabasi yote kuingia katika stendi hiyo, Kasebo amesema imelifanya eneo hilo kurudisha mzunguko wa biashara, ikiwamo ya wahudumu 275 waliopewa vibali na Halmashauri ya Jiji.
“Vilevile kuna kikundi cha pikipiki 223, kuna bajaji 203, na kuna mama lishe na baba lishe 450, wote hao wananufaika na mzunguko wa biashara. Halafu mapato ya stendi yameongezeka kutoka Sh6 milioni hadi Sh18 milioni kwa siku,” amesema.
Ameongeza, “utaratibu huu umerahisisha ukaguzi wa mabasi, kwani mabasi mengi yalikuwa yanasafiri bila kukaguliwa, lakini baada ya ukaguzi kufanyika hapa stendi, ilibainika kuwa madereva wengi wameshabadilisha hadi madaraja yao waliyopewa. Pia ukaguzi huo umewezesha kuwabaini wageni wa nchi nyingine wanaoingia nchini kinyume cha sharia.”