SoC04 Magufulication: Mahakama ya ufisadi iwekwe kisheria kulinda mali za umma na uwajibikaji

Tanzania Tuitakayo competition threads

WAPEKEE_

Member
Joined
May 23, 2024
Posts
21
Reaction score
28
Ni kama ndoto ya usiku wa manane, nazishuhudia zile siku nzito zisizosahaulika za kampeni za wabunge na urais mwaka 2015 , namshuhudia Hayati Dkt John Pombe Magufuli, akimwaga sera zake za kuomba kuchaguliwa kuwa rais, ana iahidi Tanzania na ulimwengu kuwa akichaguliwa tu, ataanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na wala rushwa.

Ni kweli wala sio porojo mwaka mmoja tu baada ya kuchaguliwa, mafisadi na wala rushwa walikiona cha moto, tayari alikuwa ameimarisha muhimili wa Mahakama kwa kutoa mabilioni ya shillingi kwenye ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama, malipo ya majaji na watumishi wa mahakama, pamoja na taasisi za sheria na haki jinai nchini.

Tayari mashauri na kesi nyingi zilikuwa zikisomwa na kutolewa hukumu kwa wakati na kuondoa mlundikano mahabusu na magerezani. Watumishi hewa, kesi za kubambikiwa, rushwa na mikataba mibovu ya rasilimali za nchi ikapitiwa upya na kutafutiwa ufumbuzi wake katika kuleta faida, usawa na tija za kimaendeleo Tanzania. Kesi za uhujumu uchumi na ufisadi zikasikilizwa kwa wakati na mabilioni ya fedha na mali zikataifishwa kulinda mali za umma huku dhana ya uzalendo ikitia mizizi zaidi na Muhimili wa Mahakama ukazidi kuaminika na kuimarika pia.

Serikali ikashirikiana na taasisi za kupambana na ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Mashirika ya umma yakabanwa, vigezo na upatikanaji wa madaraka na uongozi wa mashirika na taasisi za umma ukaongezwa. Mahakama ikapewa nguvu kubwa ya kushughulikia makosa ya ufisadi na rushwa. Tanzania ikanyooka kama rula pamoja na kuwa haikumaliza kabisa mafisadi na wala rushwa lakini hatua kubwa ilipigwa.

MCHAKATO KUKWAMA.
Pamoja na jitihada na shauku kubwa ya Hayati Magufufuli, mchakato wa uanzishwaji kamili wa makama inayojitegemea , ulihitaji baraka na taratibu za kisheria kupitia mihimili yote mitatu ya nchi yaani, Serikali, Bunge na Mahakama yenyewe.

Mpaka kufikia February 2021 kwenye ngwe ya pili ya uongozi wa awamu ya sita kabla ya kifo cha Hayati Magufuli, Jaji mkuu (Mstaafu) Mohamed Chande Othman, alisema suala la uanzishwaji wa Mahakama Maalumu ya kushughukia makosa makubwa ya ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi ndicho kipaumbele kikuu na cha kwanza kwa mahakama.

Mchakato ule ulikuwa ukifanywa na mahakama ikishirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali (CAG), Ofisi ya mkurugenezi wa Mashitaka (DPP), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) bila kusahau Jeshi La Polisi. Hivyo mpaka Hayati Magufuli anafariki, bado mahakama ya ufisadi ilikuwa ni Divisheni au Kitengo cha Makosa ya Rushwa na uhujumu Uchumi na sio Mahakama kamili inayojitegemea kwa uendeshwaji wake.

Hata mwaka 2023 February , Rais wa Zanzbar, Dk Hussein Ali Mwinyi alipongeza kamati ya wataalamu iliyoundwa kusimamia na kuratibu mchakato wa kuanzishwa kwa divisheni hiyo ya makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, huku akiwahimiza kuharakisha mchakato.

RAIS SAMIA NA TUME YA HAKI JINAI.
Mwaka 2023 Januari,Rais wa awamu ya sita Dk Samia, alizindua tume ya kuboresha Taasisi za haki jinai ili kubaini kasoro zilizopo kwenye utoaji wa haki kwa taasisi zote za haki ikiwemo TAKUKURU, Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Jeshi la Polisi, Magereza na Mahakama . Hiyo ilionesha dhahiri shauku ya viongozi wakubwa wa nchi kama Rais na wasaidizi wake kuimarisha mifumo ya haki na uwajibikaji kwenye nchi yetu ya Tanzania. Ikatoa matumaini kuwa mchakato wa Mahakama ya Ufisadi upo njiani kukamilika.

MAHAKAMA YA UFISADI KWA MIAKA 25 IJAYO.
Kwa miaka 25 ijayo kama taifa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mahakama ya Ufisadi iwe Mahakama kamili inayojitegemea kwenye uendeshwaji wake. Isiwe tu kitengo bali iwe Mamlaka kamili itakayogusa mihimili yote bila kuingiliwa ili kuongeza uwajibikaji na utoaji wa haki nchini.

Mahakama hii iwe na nguvu na mamlaka ya kuwadhibiti mafisadi wa ndani na nje ya nchi.Kuwashughulikia viongozi wanaofanya ubadhirifu wa mali za umma na kutumia mamlaka vibaya.

Kama taifa lenye Dira ya Maendeleo, lazima kuwe na mamlaka thabiti ya kulinda mali na maendeleo yake dhidi ya majangiri wa kiuchumi.

MKAKATI WA KITAIFA
Maono Kama haya hayapaswi kuwa ni mano ya mtu au kiongozi mmoja mmoja, bali ni maono ya kitaifa yatakayobebwa na taasisi za kitaifa ambazo zitawajibika kitaasisi na sio kama mtu mmoja. Huu uwe mkakati wa kitaifa utakaolindwa na kuendeshwa kwa sheria na katiba zaidi ili kila kiongozi anayekuja pamoja na mipango yake lakini, awajibike na mkakati wa kitaifa kama vile huduma za msingi zilivyo kwa Afya, Maji, Kilimo, Miundombinu na kadharika. Na Mahakama ya Ufisaidi iwe ni moja ya huduma za msingi kwa nchi kwenye sekta ya Mahakama.

MIHIMILI YA DOLA INAYOJITEGEMEA.
Mihimili ya dola inapaswa kujitegemea bila kuingiliana, kama vile bunge libaki kwenye kutunga sheria, serikali kwenye usimamizi na uendeshwaji wa shuguli za nchi huku mahakama ikitoa tafsiri ya sheria kwenye haki na migogoro ya jamii.

Uhuru utasaidia kutokuingiliana katika majukumu, ili kusaidia uwajibikaji wa nchi kwa ujumla wake. Na hii ndio itasaidia kupata Mahakama ya Ufisadi yenye Meno makali ya kumng’ata yeyote yule bila kujali cheo chake au anatoka kwenye muhimili gani wa dola, bali Mahakama itamshughulikia kwa mujibu sheria na taratibu za nchi.

KUENZI FALSAFA ZA WAKUU WA NCHI KWA VIZAZI VIJAVYO ( MAGUFULICATION )
Kama Taifa huru na historia yetu, tumekuwa na utaratibu wa kuenzi kwa kuziendeleza na kuzitunza falsafa za wakuu wa nchi kama Rais, Mawaziri na Viongozi maarufu kwa maslahi mapana ya historia na maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania. Hivyo iko haja kuenzi falsafa ya Hayati Magufuli Rais wa awamu ya tano , aliyekuja na maono ya Mahakama ya Ufisadi , iliyolenga kuleta uwajibikaji na ulinzi wa mali za Umma. MAGUFULICATION ni Falsafa ya kuendesha nchi kwa sheria na kanuni zinazomuwajibisha yeyote bila kujali nafasi au cheo chake na kuleta usawa katika jamii.

Kwa miaka 25 ijayo mpaka mwaka 2050, tutakuwa na taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi , kwani tutalinda utajiri wetu na kulinda watu wetu kwa miaka mingi ijayo.

Wenu kwenye ujenzi wa nchi yetu Tanzania.
WAPEKEE KEPHAS YOHANA.
SIMU: 0694 024 888 / 0674 968 400

ÙTR 9Y
Magufuli mahakama .jpg
 
Upvote 4

ÙTR 9YView attachment 3024971
Great article
 
Back
Top Bottom