Magufulification of Kenya Ruto ana-challange mfumo?

Magufulification of Kenya Ruto ana-challange mfumo?

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Kama mchambuzi wa siasa ndani ya Afrika mashariki unaweza kutoa opinion gani kwa yale yanaoendelea kutokea nchini Kenya?

Willium Ruto ameamua kuwa jeuri na nyang'au na hivyo kuiondoa kenya kwenye wimbi la muda mrefu la ufisadi na uhuni uliokuwa umekithiri nchini Kenya?

Je, Ruto ameamua kuwainua wakazi waliochoka wa Mitaa ya kibera dhidi ya matycoon wachache waliowezeshwa na walami?

weka tafakari yako hapa...bila matusi wala kebehi.

KWA HISANI YA WATU WA KENYA!!
 
Kivipi? Mapambano ya Kenya ni juu ya kabila gani lidominate mfumo wa utawala. Wala sio juu ya maendeleo ya nchi na wananchi.

Wameshindwa kutengeneza mfumo wa kupunguza ukabila Kenya.

Kuna miiko wameshindwa kujiwekea.
 
Katiba mpya haijasaidia?
 
Katiba mpya haijasaidia?
Wakenya wanaona hiyo katiba yao kama karatasi tu. Ndio maana kila kukicha wanataka kuibadiliaha. Ukiona hivyo ujue tatizo sio katiba. Tatizo makabila.

Na kule kiongozi hana aibu kubagua kabila lingine wazi wazi na hata kupeleka maendeleo maeneo kwa kuegemea makabila.

Wakenya wametekwa na mfumo wa makabila na wanashindwa kujinasua.
 
Willium Ruto ameamua kuwa jeuri na nyang'au na hivyo kuiondoa kenya kwenye wimbi la muda mrefu la ufisadi na uhuni uliokuwa umekithiri nchini Kenya?

wakazi waliochoka wa Mitaa ya kibera dhidi ya matycoon wachache waliowezeshwa na walami?
Sielewi maana ya matusi na kebehi, tena baada ya kusoma na kufanya tafakuri ya maandishi yako.
 
Uchaguzi umepita toka 2022, Sasa unatakiwa Uwe ni Wakati Wa Kuchapa Kazi Kuleta Maendeleo Ya Kenya.

Sasa Kwa Upuuzi Wa Viongozi vyama vya Siasa Wanaitumia 'Katiba' kuleta Maandamano Yenye Vurugu.

Waafrika Tunahitaji ukombozi Wa Fikra Kwanza kuliko 'KATIBA Mpya'..!
 
Ruto kaamua kupambana na mafisadi na waporaji wa maliasili za nchi, lakini anapaswa awe imara sana maana atatikiswa na wakora.

Mkora namba 1 ni kiongozi wa ODM ambaye anatumiwa na wakora wengine wamejificha.

Ruto akitaka kuinyoosha Kenya kamwe asiwe na muhali kuchukua hatua kwa yeyote yule hata kama alikuwa rafiki yake.
 
Ruto ni kama Magufuli ndio, wote ni matapeli, wezi na wauaji wanaojinasibu kama rafiki wa masikini.

Huku akigawa vyeo kwa loyalists wake na kuwagawia mamilioni
 
Kivipi? Mapambano ya Kenya ni juu ya kabila gani lidominate mfumo wa utawala. Wala sio juu ya maendeleo ya nchi na wananchi.

Wameshindwa kutengeneza mfumo wa kupunguza ukabila Kenya.

Kuna miiko wameshindwa kujiwekea.
Swadaqta!! zile hisia ni za kikabila kama ile 2007 na watamalizana sana kwa hapa bongo tusichekee ukabila una hisia sana na ni hatari tusiuweke mbrlr
 
Ruto kaamua kupambana na mafisadi na waporaji wa maliasili za nchi, lakini anapaswa awe imara sana maana atatikiswa na wakora.

Mkora namba 1 ni kiongozi wa ODM ambaye anatumiwa na wakora wengine wamejificha.

Ruto akitaka kuinyoosha Kenya kamwe asiwe na muhali kuchukua hatua kwa yeyote yule hata kama alikuwa rafiki yake.
Kazini kuna kazi
 
Wakenya wanaona hiyo katiba yao kama karatasi tu. Ndio maana kila kukicha wanataka kuibadiliaha. Ukiona hivyo ujue tatizo sio katiba. Tatizo makabila.

Na kule kiongozi hana aibu kubagua kabila lingine wazi wazi na hata kupeleka maendeleo maeneo kwa kuegemea makabila.

Wakenya wametekwa na mfumo wa makabila na wanashindwa kujinasua.

Katiba imewasaidia sana .

Kama sio katiba kenya sasa hivi ingekua na umwagaji mkubwa sana wa damu .

Walipotoka ni mbali sana .

Tanzania ni Nyerere tu alituwekea mifumo bora ya kisiasa lakini kuna uhuni mwingi kama ilivyo Kenya na nchi za kiafrika zinaongozwa na wahuni . CCM ni kichaka cha kuficha na kutetea wahuni na uhuni lakini pia kuna Uhuni unaotokana na wizi wa mapato wa wazi wazi kwa Watawala kuteuana kwa ajili ya kuchota fedha za umma.

Kuna hizi bodi zinazoundwa na rais hazina tija kabisa zaidi ya kichaka cha kuiba fedha za umma. Soko huria bodi za nini kama sio uhuni ?
 
Back
Top Bottom