nobodylikedme
JF-Expert Member
- Apr 5, 2018
- 741
- 768
Kuna kaka yangu mmoja mtoto wa mama mkubwa ni mkandarasi wenye uzoefu wake tu na yuko vizuri sana kiuchumi kwa level za kibongo bongo.Ubinafsi utaendelea kututafuna Watanzania.
Mwaka uliopita nilimuomba anikopeshe 2m hili kuongeza mtaji wa biashara niliyokuwa nimeiplan ya kusafarisha na kuingiza bidhaa nje ya nchi. "Aliniambia sina kitu dogo, hali ngumu" mwaka huu mwanzoni amemvalisha mchumba wake pete yenye madini ya tanzanite ambayo thamani yake ni 1.5m. Mwezi wa tisa anafunga ndoa alafu ananiambia eti nifanye juu chini nisikose kushiriki harusi yake.
Aloo mpaka hapa ninavyoandika hata namba yake ya simu tu nilishaga ifuta kwenye phone book yangu siku nyingi sana. Na sio yeye tu nimefuta namba za karibu ndugu wote wasiokuwa na faida kwenye maisha yangu.
Sisi wabantu umimi,ubinafsi,kujiskia na kufurahia matatizo ya wengine ndio tulichobarikiwa. Na ndio maana huwa tunaendeana kwa waganga sana hili tushushane.